Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ushauri

Madhara ya Kutoa Ushauri Kienyeji na Kuugeuza Unasihi kuwa Ushauri

Picha
Utamaduni wa (kutoa na kuomba) ushauri umejengeka kwenye misingi ya hekima ya wazee walioona mengi, uzoefu wa mtu mzima unaompa uhalali wa kutoa mwongozo wa kufuata kwa anayemzidi.  Hata tunaposikia unasihi (counselling), aghalabu, mawazo yetu yanaenda kwenye taaluma ya kushauri watu na kuwaambia cha kufanya ili kutatua matatizo yanayowakabili. Wapo, tena wengi, wanaotafsiri ‘counselling’ kama ushauri. Counselling sio ushauri. Katika makala haya, ninajenga hoja kuwa kutoa ushauri ni jambo la hatari na kwamba linaweza kusababisha madhara makubwa kwa anayeshauriwa lakini pia hata anayeshauri.  Kadhalika, ninalenga kuonesha, japo kwa ufupi kuwa hata kwenye unasihi msingi wa kwanza wa kuzingatia kwa mtoa huduma (aliyefuzu) ni kuepuka kabisa kutoa ushauri kwa mtu. Nakusudia kuonesha nini hasa huwa ni malengo ya unasihi. stefanamer/Getty Images Ushauri ni nini?  Unaposema unamshauri mtu unakuwa na maana gani?  Ushauri, kwa kifupi, ni maelekezo mahususi unayompa mtu, maamuz...

Umuhimu wa Kumpunguzia Mtoto Shinikizo la Kufaulu

Picha
PICHA: Stressed Out Students Ufaulu wa mitihani umepewa nafasi ya pekee katika mfumo wetu wa elimu. Shule zetu, kwa hakika, hazina namna nyingine ya kumwelimisha mtoto zaidi ya kumtaka akusanye, akumbuke na kutumia maarifa aliyonayo kujibu maswali ya mtihani. Ingawa ustawi wa jumla wa mwanadamu hautegemei eneo hilo moja la ukusanyaji na utumiaji wa maarifa, shule zetu zinaonekana kuamini pasipo mtu kuwa na maarifa mengi hawezi kufanikiwa.

Ufanyeje Kijana Chipukizi 'Anapokata' Mawasiliano na Wewe?

Picha
PICHA:  Parent Pump Radio Kama nilivyoeleza kwenye makala yaliyopita, tofauti za kimtazamo kati ya mzazi na kijana anayechipukia ni hali zinazotarajiwa. Wakati mwingine tofauti hizi zinaweza kuonekana kama mambo madogo yasiyo na msingi. Lakini tofauti hizi zinazoonekana kuwa ndogo zisiposhughulikiwa zinaweza kukomaa na hatimaye kusababisha matatizo makubwa. Wazazi, mara nyingi, hatupendi kuzipa uzito tofauti hizi mara zinazopoanza kujitokeza. Kijana wako anaweza kuanza kuwa mkimya bila sababu za msingi, anaanza kukukwepa na hata kupunguza mawasiliano na wewe, lakini ukachukulia ‘kawaida.’

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Picha
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -2

Picha
PICHA: Shutterstock Katika makala yaliyopita tuliona mbinu tatu unazoweza kuzitumia kuelewa mambo unayojifunza. Kwanza, ni ‘njaa’ inayokusukuma kuelewa. Unapokuwa na ari ya kuelewa jambo, mara nyingi, utahamasika kulielewa bila kutumia nguvu nyingi. Pili, tuliona ni muhimu kutengeneza picha kubwa ya jambo unalojifunza kabla hujaanza kujifunza undani wa mambo madogo madogo ndani ya picha hiyo. Kwa mfano, unaposoma aina za vyakula, lazima kwanza uelewe vyakula. Uelewa wa jumla wa vyakula utakurahisishia kazi ya kuchanganua aina zake kwa sababu tayari unayo rejea utakayoitumia kuelewa zaidi. Mbinu ya tatu ni kukihusisha kitu unachokisoma na mambo unayoyafahamu tayari. Unaposoma aina za vyakula, kwa mfano, lazima uwe unafikiria vyakula mbalimbali unavyovifahamu katika mazingira yako. Unapojaribu kuhusianisha kile unachokisoma na maisha yako ya kila siku, unaurahisishia ubongo wako kazi ya kupokea kuliko kuingiza kitu kipya kisichohusiana kwa vyovyote vile na ...

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma

Picha
PICHA: Oxford Learning Kusoma kitu usichokielewa ni hasara. Mbali na kuongeza uwezekano wa ‘kupigwa chenga’ wakati wa mtihani, kutokuelewa kunaharibu dhima ya elimu. Mtu asiyeelewa kile alichojifunza, kwa mfano, hawezi kutumia maarifa aliyonayo kuleta tija kwa jamii.

Kinachofanya Wanafunzi Wasielewe Wanachokisoma

Picha
PICHA:  SciTech Daily Ujifunzaji (learning) ni mchakato wa kupata uzoefu mpya katika maeneo makubwa matatu. Kwanza, kubadili namna mtu anavyofikiri. Maarifa mapya huja na uzoefu mpya unaobadilisha uelewa wa mambo.

Mambo ya Kutafakari Unapoanzisha Uhusiano wa Kimapenzi Kazini

Picha
PICHA: Shalinii Choudhary   Sehemu kubwa ya maisha yako kama mfanyakazi unaitumia kwenye eneo la kazi. Ingawa inategemea na aina ya kazi unayoifanya, ni wazi muda mrefu kwa siku unaoutumia kutekeleza majukumu yako unakuweka karibu zaidi na wafanyakazi wenzako kuliko hata familia na marafiki. Mazingira haya ya ukaribu wa kikazi, wakati mwingine, yanatengeneza uwezekano wa uhusiano wa kimapenzi baina ya wafanyakazi.

Vigezo Vinne Unapotafuta Msichana wa Malezi

Picha
PICHA: Gumtree South Africa MALEZI katika enzi tulizonazo hayafanani na vile iliyokuwa hapo zamani. Mambo yamebadilika. Kwa mfano, zamani wazazi wetu hawakuwa na shida ya nani hasa abaki na mtoto nyumbani. Mama alikuwepo nyumbani. Kazi yake kubwa ilikuwa malezi. Hata katika mazingira ambayo mama hakuwepo, bado walikuwepo ndugu na jamaa walioweza kubeba jukumu hili kwa muda.

Namna Bora ya Kuwasiliana na Wafanyakazi Unaowaongoza

Picha
Maisha ya kazi kwa kiasi kikubwa ni mawasiliano. Karibu kila tunachokifanya kazini ni kuwasiliana. Tunawasiliana na wateja. Tunawasiliana na wakubwa wa kazi. Tunawasiliana na walio chini yetu. Kwa ujumla kazi ni mtiririko wa mawasiliano.

Mabadiliko ya Kijamii Yanavyoathiri Malezi -1

Picha
PICHA:  The Conversation TUNAISHI katika nyakati ambazo maarifa kuhusu malezi ya watoto vinapewa umuhimu. Sambamba na ongezeko la mijadala ya malezi katika majukwaa mbalimbali, malezi yamevutia hisia za watafiti wengi kuliko ilivyopata kuwa. Kila siku, kwa mfano, zinachapishwa tafiti nyingi kuchunguza changamoto za malezi ya watoto.

Unavyoweza Kumrekebisha Mtoto Mjuaji Anayejiona Bora

Picha
PICHA: Psychology Today Kujiona bora ni kujiamini kupindukia. Mtu anayejiamini kupita kiasi, mara nyingi, anaamini anazo sifa ambazo watu wengine hawana. Unapoamini unazo sifa za ziada kuliko wengine ni rahisi kuwa na kiburi. Kuamini watu wengine hawawezi kuwa bora kama wewe kunakufanya uwadharau.

Mwalimu Anavyoweza Kukuza Udadisi kwa Wanafunzi

Picha
PICHA: OBrown & Associates Education Consulting Mara nyingi tumesikia watu wakilaumu mtalaa wetu kwamba unafunga fahamu za wanafunzi wetu. Wenye madai haya wanafikiri bila mtalaa kufanyiwa marekebisho makubwa, haiwezekani elimu yetu ikamnufaisha mwanafunzi. Hata hivyo, tulisema wiki iliyopita, kazi ya mtalaa ni kutoa diraya jumla ya aina ya raia wanaotarajiwa kufundwa kupitia mtalaa husika.

Kumsaidia Mtoto Asiyejiamini, 'Anayeogopa' Watu

Picha
PICHA: Blend Images KUTOKUJIAMINI ni kutokuwa na ujasiri, kutokuwa na imani na uwezo wako mwenyewe. Mtu asiyejiamini anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vitu. Tatizo lake ni kujishuku. Vijana wa mjini wanaita ‘kujistukia.’ 

Tufanye nini Kukuza Udadisi kwa Wanafunzi Wetu?

Picha
PICHA: Fernando Díez Gallego UDADISI ni uwezo wa kuhoji mazoea. Udadisi ni kiu ya kujiuliza maswali yanayolenga kutafuta majibu ya changamoto zilizopo. Mtu mdadisi lazima atakuwa na uchunguzi ndani yake. Haiachi akili yake itulie. Haridhiki na majibu yaliyozoeleka. Mdadisi hupembua taarifa kumwezesha kuelewa ujumbe uliojificha kwenye taarifa hizo.

Ufanye Nini Mtoto Anapokuwa Mkorofi?

Picha
PICHA: JGI/Jamie Grill Pengine una mtoto unayefikiri ameshindikana. Unamwita mtundu, mtukutu, asiyeambilika, mbishi, mkaidi na majina mengine. Kikubwa ni tabia yake ya kupenda kushindana. Katika makala haya tunamwita mtoto mkorofi. Huyu ni mtoto anayeweza kukukatalia kitu bila kupepesa macho na ukajikuta ukifedheheka.

Ayafanyayo Mzazi Huamua Atakavyokuwa Mtoto

Picha
PICHA: Pinterest 'Mwanangu ni mtundu haijapata kutokea’ alilalamika msomaji mmoja wa safu hii. Sikuelewa ana maana gani aliposema mwanae ni mtundu. Nikaomba ufafanuzi. ‘Hasikii. Jeuri asikwambie mtu. Usipomfanyia purukushani huwezi kumwambia kitu akasikia.’ Kwa mujibu wa maelezo yake, kuna nyakati hubidi amtishe, amwadhibu vikali na hata kumtukana ikibidi.

Namna ya Kuutambua Wito wa Maisha Yako

Picha
PICHA: B aha'i Blog Umewahi kufanya kazi zenye heshima lakini hujisikii ridhiko ndani yako? Unapata kipato kizuri na watu wengine wanatamani kufanya unachokifanya lakini wewe mwenyewe hufurahii.  Unakuta umesoma vizuri lakini huoni thamani ya kile ulichokisoma. Zaidi ya kutaja chuo ulichosoma na ngazi ya elimu uliyofikia huoni namna gani elimu yako inakusaidia kutoa mchango kwa jamii.

Unahitaji Nidhamu ya Fedha Kujikwamua Kiuchumi

Picha
PICHA: usaa.com Juma lililopita tuliongelea uwezekano wa mfanyakazi kujikwamua kiuchumi . Kubwa ni nidhamu. Unapokuwa na nidhamu ya mshahara, unaongeza uwezekano wa kuwa na usalama wa kifedha. Swali linaweza kuwa, ‘Kinachomfanya mfanyakazi akose nidhamu ya fedha ni nini?’ ‘Inakuwaje mchuuzi mdogo wa bidhaa awe na nidhamu ya fedha kuliko Afisa wa Serikali?’

Wajibu wa Wamiliki wa Shule za Msingi za Bweni

Picha
PICHA: B ORGEN Magazine TUMESHAURIANA mambo kadhaa ya kuzingatia tunapolazimika kuwapeleka watoto wadogo kwenye shule za msingi za bweni. Kubwa zaidi ni mzazi kujiridhisha na namna shule inavyomwekea mtoto mazingira mazuri yanayofanana na yale ya nyumbani.