Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kazi

Ukishasahau ulikotoka huwezi kuwa mzazi mzuri

Picha
  Sijui kama umewahi kuwaza kama mimi. Je, mafanikio yetu yanawasaidia watoto kuwa binadamu timamu? Je, uwezo tulionao kiuchumi unawezesha watoto kujifunza tabia zitakazowafanikisha kiuchumi? Kuna namna ninaogopa kuwa huenda tunawanyima watoto wetu fursa ya kujifunza maisha katika uhalisia wake. Nafahamu wapo baadhi ya wazazi wamekulia kwenye familia zinazojiweza kiuchumi. Hata hivyo, hiyo haiondoi ukweli kuwa wengi wetu tumetoka kwenye familia masikini na tumekuwa kizazi cha kwanza kupambana na kuuweza umasikini. Je, tunawaandaa watoto wetu kujikwamua kama tulivyojikwamua sisi?   PICHA: Marlous de Milliano Tunafahamu namna umasikini unavyofedhehesha. Umasikini unafanya maisha yako yasiwe na uchaguzi. Umasikini unakufanya upate kinachopatikana na sio kile unachokihitaji.  Hili, pamoja na ubaya wake, kwa kiasi kikubwa limekuwa kichocheo cha wengi wetu kuwa na hasira kubwa kupambana na umasikini kwa nguvu zote. Bidii ya kazi unayokuwa nayo ni matokeo ya hasira kuwa usi...