Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2012

Mitaa ya Nairobi kwa jicho langu

Picha
Foleni ya matatu, abiria wanaingia kwa utaratibu Alama ya jiji la Nairobi, land mark Iliko benki kuu ya kenya Mtaa wa Kimathi, Ofisi za Magazeti ya Nation Pilikapika za mtaa wa Tom Mboya Sanam ya shujaa Tom Mboya Alama za mitaa, zinaonekana uzuri

Mitaa ya Nairobi, 'Usomini UoN'

Picha
Chuo Kikuu cha Nairobi, kinachosemekana kuwa moja wapo ya vyuo bora Afrika Mitaa ya Chuo Kikuu cha Nairobi Ndani ya Chuo, karibu na duka la vitabu Bustani za wazi katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Nairobu Kama ni kweli, sehemu hii haihusiki basi sawa sawa Sijui nielekee wapi, huku au kule? Alama ya utambulisho wa Chuo Kikuu cha Nairobi

Nilipokutana na Mshairi Serina wa Upande Mwingine

Picha
Katika mkutano wa wanablogu na waandishi wa habari za kiraia uliofanyika Nairobi, Kenya, nimebahatika kukutana na mwanablogu niliyekuwa na hamu sana ya kuonana naye. Naye si mwingine bali, dada Serina Kalande, anayetuandikia kwenye blogu ya Upande mwingine . Na Serina Kalande, wa Upande mwingine. Picha: Deogratias simba Ni dada mkarimu, mpole, mwanana na mwema sana kuzungumza naye. Serina, asante kwa baraka ya kukuona.

Mgomo wa Mabasi ya Abiria Mjini Moshi

Picha
 Wakazi wa Manispaa ya Moshi na vitongoji vyake leo wameonja adha ya kukosa usafiri kufuatia mgomo wa mabasi  yanayotoa huduma ya usafiri mjini hapa, maarufu kama daladala.  Kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi kama inavyoonekana dakika chache zilizopita  Mgomo huo umetokea kama hatua za waendeshaji wa huduma hiyo kupinga kupanda kwa kiwango cha ushuru kilichotangazwa na Halmashauri ya Manispaa hiyo. Vibao vipo, magari hayaonekani  Kwa  mujibu wa tangazo la Halmashauri hiyo inayoongozwa na CHADEMA, ushuru huo umepanda kwa asilimia 50 kutoka Tsh. 1000 zilizokuwa zikilipwa awali mpaka Tsh 1500 zinazotakiwa kuanza kulipwa mara moja. Kituo kikiwa tupu, huku Polisi wa 'kutuliza' ghasia wakiwa kazini Tayari Katibu wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro, Bw. Lema, kupitia Radio za FM mjini hapa ametoa tamko la kupinga vikali ongezeko hilo, akiliita kuwa 'hujuma' inayofanywa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na chama chake kuonyesha kuw