Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mafanikio

Hulka ya Mwanadamu Kujikweza na Kukwepa Wajibu

Picha
Umewahi kujiuliza kwa nini mtu akifanikiwa jambo (biashara, kazi, elimu, siasa nk) anataka aonekane ana bidii, ana uwezo na kitu cha tofauti kinachomtofautisha na wengine? Kwa nini, kwa mfano, ikitokea kinyume, mtu akashindwa, akafanya vibaya, hutaka ionekane kuna watu wanamkwamisha, kuna upinzani, kuna wabaya wake na inakuwa nadra kukubali huenda tabia zake mwenyewe zinamgharimu? Mwaka 1978, washunuzi Berglas na Jones waliwatumia wanafunzi wa chuo kuichunguza dhana hii. Makundi mawili ya wanafunzi yalipewa 'puzzle'— fumbo linalohitaji akili kulifumbua. Kundi A walipewa fumbo rahisi. Halikuhitaji kufikiri sana. Kundi B wakapewa fumbo gumu (lisilowezekana hata ukeshe nalo). Makundi yote yalipewa maelekezo kuwa wakihitaji kuboresha uelewa ili wafumbue fumbo wanaweza kuomba kidonge kinachoitwa Actavil lakini wakiona wanahitaji kidonge cha Pandocrin kinachopunguza uelewa pia wangeweza kuomba. Wakati zoezi kiliendelea, 80% ya washiriki wa kundi A (wenye fumbo rahisi) waliomba kido...

Zijue Ishara Tano Kuwa Mwajiri Amekuchoka

Picha
UMEWAHI kuhisi huhitajiki kazini? Umewahi kuona dalili kwamba pengine ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kabla mambo hayajaharibika? Mwandishi Speancer Johnson aliyeandika kitabu maarufu cha ‘ Who Moved My Cheese ” anasema ni muhimu kusoma alama za nyakati katika maeneo ya kazi. Unapofanya kazi bila kuelewa ishara za awali mambo yanapoanza kwenda mrama, unajiweka kwenye hatari ya kujikuta kwenye mazingira ya kufanya maamuzi kwa kuchelewa. Wafanyakazi wengi huamini mwajiri akiwachoka atawaandikia barua ya kuwafuta kazi. Hawajisumbui kujua kusoma ishara mbaya kwa kuamini mwajiri hawezi kuwachoka na akabaki kimya. Unaweza kujiuliza, kama kampuni haikuhitaji kwa nini hawakuambii? Ukweli ni kwamba, wakati mwingine mwajiri huona ni afadhali akuwekee mazingira ya wewe kuondoka mwenyewe kuliko kukuondoa. Mwajiri anapokuondoa anajiweka kwenye mazingira yanayoweza kumletea usumbufu wa kisheria na wakati mwingine wafanyakazi wanaobaki hupatwa na tahayaruki. Ili kuepuka k...

Kwa Nini Wanawake Wenye Mafanikio Wanaogopwa?

Picha
UPO ukweli kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Hawa ni wanawake wenye kiwango kikubwa cha elimu, fedha, umaarufu au hata madaraka katika jamii. Hoja ya wanaume wenye mawazo haya ni ugumu wa kuwaongoza wanawake wanaowazidi kama alivyonieleza Godfrey, mwalimu wa sekondari jijini Arusha: