Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya mahusiano

Ukifikiri Upendo ni Vitu Utamkinai Anayekupenda

Picha
Juzi naongea na kijana mmoja, umri nakadiria kavuka miaka thelathini, ananiambia ameanza kuhisi kama vile hakuumbiwa mapenzi. Ukisikia mtu anatoa kauli nzito hivi ujue kuna jambo. Kudodosa, kumbe, kayapambania mapenzi na yamekaribia kumtoa roho. Kila anayempenda kwa dhati anaishia kumwacha hewani.     Haelewi afanye nini.   “Hawa wanawake wanataka nini?” Kaniuliza. Tuliongea mengi. Naomba nikushirikishe, japo kwa muhtasari, maudhui ya mazungumzo yetu.    Picha: Tony Cordoza   |  Getty Images Tumeanza kuwa na kizazi cha vijana werevu, watafutaji, wenye uwezo mkubwa wa kutafuta pesa lakini wenye hisia kificho, wasiojali hisia na wasio na haja ya kina cha mahusiano.  Hiki ni kizazi, aghalabu, kilichozaliwa na kizazi cha wazazi wasomi, wenye maarifa zaidi na pesa zaidi kuliko kizazi kilichopita. Tunatumia muda mwingi kazini, kwenye biashara, na shughuli nyingine za kutafuta vitu. Ukiangalia kwa haraka unaona hiki ni kizazi chenye watu wenye kazi ...

Unampeleka mtoto mdogo bweni? Fikiria.

Picha
Miaka michache iliyopita, mtu ulikuwa ukisikia shule za msingi za bweni, tena kwa watoto wadogo, tafsiri unayopata kwa haraka haraka ni malezi mabovu. Unampelekaje mtoto wa miaka sita bweni? Kuna nini cha maana shule ya bweni kinachohalalisha mtoto kutengwa na wazazi wake? Kwa hiyo, tuliona bweni ni uamuzi wa mzazi asiyeelewa jukumu lake la malezi, mzazi asiyejali, anayeamua kumtelekeza mtoto kwa sababu zisizo na msingi. Lakini kwa hizi nyakati tulizonazo, tunapokabiliwa na mabadiliko mengi ya kijamii, saa nyingine tunahitaji kuwa na tahadhari tunapofanya mahitimisho ya haraka kwa namna hiyo. Sikiliza simulizi la Aisha, afisa wa benki, mama wa mtoto anayesoma shule ya msingi la bweni. “Sikuwahi kufikiri ningekuwa mama anayeona bora mtoto aende bweni. Ndugu yangu yamenikuta.” Aisha ana mgogoro mkubwa na mzazi mwenzake. Ugomvi wao, ananiambia, ulifikia ngazi ya uadui. Haikutosha wao kushindwa kuishi pamoja, lakini pia ikawa vigumu kukubaliana nani abaki na mtoto. “Tulivutana sana. Baad...