Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya mijadala

Una nguvu ya kupambana na hali iliyokuchosha

Umewahi kujiuliza kwa nini mtu anapigwa, anaumizwa, anadhalilishwa na mpenzi wake na bado haoni kama kuna kitu anaweza kufanya? Mwingine anasitisha uhusiano lakini anapoanzisha mahusiano anakutana na mwingine mwenye tabia zile zile alizozikimbia kwa aliyemwacha. Ili kulitafakari hili, nikusimulie alichokifanya Martin Seligman na Steven Maier mwaka 1965. Washunuzi hawa waliwatia mbwa kifungoni kwa kuwafungia kwenye kizimba kisichowaruhusu kutoka. Mle ndani kizimbani mbwa walipigwa shoti ya umeme mfululizo iliwapa maumivu makali. Hata pale ambapo mbwa angefanya majaribio ya kutoroka asingeweza. Kizimba kilikuwa imara. Kilichowashangaza Seligman na Maier ni kwamba hata pale walipofungua mlango wa kizimba kuwaruhusu watoke, ingawa mbwa wale walilia kwa uchungu, wakilalamika na kutia huruma, hawakuthubu kujaribu kutoka pamoja na maumivu makali ndani ya kizimba. Hali ilikuwa tofauti kwa kundi jingine la mbwa lililokuwa limefungiwa kwenye kizimba kisicho na shoti ya umeme au kilichokuwa na uw...

Unampeleka mtoto mdogo bweni? Fikiria.

Picha
Miaka michache iliyopita, mtu ulikuwa ukisikia shule za msingi za bweni, tena kwa watoto wadogo, tafsiri unayopata kwa haraka haraka ni malezi mabovu. Unampelekaje mtoto wa miaka sita bweni? Kuna nini cha maana shule ya bweni kinachohalalisha mtoto kutengwa na wazazi wake? Kwa hiyo, tuliona bweni ni uamuzi wa mzazi asiyeelewa jukumu lake la malezi, mzazi asiyejali, anayeamua kumtelekeza mtoto kwa sababu zisizo na msingi. Lakini kwa hizi nyakati tulizonazo, tunapokabiliwa na mabadiliko mengi ya kijamii, saa nyingine tunahitaji kuwa na tahadhari tunapofanya mahitimisho ya haraka kwa namna hiyo. Sikiliza simulizi la Aisha, afisa wa benki, mama wa mtoto anayesoma shule ya msingi la bweni. “Sikuwahi kufikiri ningekuwa mama anayeona bora mtoto aende bweni. Ndugu yangu yamenikuta.” Aisha ana mgogoro mkubwa na mzazi mwenzake. Ugomvi wao, ananiambia, ulifikia ngazi ya uadui. Haikutosha wao kushindwa kuishi pamoja, lakini pia ikawa vigumu kukubaliana nani abaki na mtoto. “Tulivutana sana. Baad...