Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2011

Pedagogy of the oppressed

Picha
Paulo Freire katika sura ya pili ya kitabu chake "Pedagogy of the Oppressed" anazungumzia dhana inayosisimua anayoiita "the banking concept of education" kama chombo kinachotumika kuwakandamiza wanyonge. Kwamba katika hayo yanayoitwa madarasa, wapo waungwana wanaojichukulia kuwa wanajua, hulipwa kwa kuwajaza wenzao "elimu" ambayo kimsingi ni chombo cha kuwakandamiza raia wanaoonewa. Freire anadhani hii si sawa kwa binadamu mwenzako kujiweka juu sana kiasi cha kuamua usome nini, na uache kipi (bila kujali mahitaji yako halisi). Anatoa mfano pale mwalimu anapoweza hata kupendekeza kwamba kitabu fulani kisomwe kuanzia ukurasa wa 10 hadi wa 15! Na eti anadhani anamsaidia mwanafunzi! Kwa mujibu wa Freire, elimu hii haiwezi kumkomboa mnyonge. Je, elimu yetu ina tofauti? Wanafunzi zaidi ya asilimia 50 "walishindwa" mtihani hivi majuzi, ni kweli walishindwa ama ni namna nyingine ya kuwakandamiza vijana wasio na hatia?

Shule zisizo na elimu zifungwe!?

Picha
Ivan D. Illich ni mwanafalsafa aliyezaliwa mjini Vienna mwaka 1926. Katika kitabu chake cha Deschooling Society, Illich anazishambulia taasisi ziinazohodhi wajibu wa kuelimisha jamii. Anasema; “…kwenda shule (tofauti na kuelimika) imekuwa ndio utaratibu wa maisha…shule zimeshindwa kukutana na mahitaji ya mtu mmoja moja, na mbaya zaidi zinaendeleza uongo ule ule kwamba yale yanayoitwa maendeleo yanayotokana na uzalishaji, utumiaji na faida ndicho kipimo cha ubora wa maisha ya mwanadamu. “…Vyuo Vikuu (shule) vimegeuka viwanda vya kutengeneza vibarua kwa ajili ya matajiri, vikiwapa raia vyeti kwa ajili ya kutoa huduma, wakati huo huo vikionekana kuwanyang’anya leseni wale vinavyowadhania kuwa hawafai (waliofeli).” Tafsiri ni yangu. Illich anatoa mapendekezo ya kukomesha mfumo huu wa baadhi ya watu kujipa wajibu wa kuwaelimisha wengine wakati wao wenyewe hawajielimishi. Haoni haja ya kuwa na majengo yanayoitwa shule ambayo kazi yake inaonekana kuishia kutengeneza watumwa wa soko huria

Matokeo Kidato cha IV 2010: Asilimia 89 wamefeli!

Inasikitisha kuwa katika matokeo ya Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani leo hii, zaidi ya asilimia 50 ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha IV mwaka 2010 wameishia kupata daraja sifuri. Asilimia 39 ya watahiniwa hao (waliozidi 440,000) wameambulia cheti kisicho na tija (yaani Daraja la IV)wakati ni asimilia 11 tu wameweza kupata Madaraja ya I, II na III. Hali hii si ya kufurahia hata kidogo. Je, tuchukue hatua gani kujinusuru na janga hili?

Ajuaye kusoma na hasomi ana nafuu?

Je, kuna tofauti kati ya mtu asiyejua kusoma (illiterate) na yule anayejua kusoma (literate) lakini hasomi?

Pesa bila kufisidi mali ya umma...

Picha
Pesa bila unyonyaji inawezekana? Ninakisoma hiki hivi sasa kwa mara ya pili, cha Napoleon Hill.

Wangapi huzitazama tabia zetu kwa jicho la mabadiliko?

Mwanzo wa mwaka huwa na matumaini tofauti na wakati mwingine wowote wa mwaka. Ni wakati ambapo watu hujisaili, na kutazama wanakoelekea kwa mwaka unaoanza. Ni wakati ambapo watu hujipanga namna ya kupiga hatua katika maeneo muhimu ya kimaisha. Hata hivyo, ni wangapi wetu huweka maazimio ya kubadili tabia zetu? Ni wangapi wetu tunao uwezo wa kuzitazama tabia zetu kwa jicho dhati la mabadiliko? Kwa mfano. kuamua kwamba mwaka huu ninapambana na tatizo la kutokusoma? Kuamua kwamba siwezi kuendelea kuwa mtu nijuaye kusoma lakini sisomi? Ni wangapi wetu hisia hizo za matumaini mapya tunazokuwazo mwanzo wa mwaka, huishia kwa matumaini yayo hayo mwisho wa mwaka? Kwa nini malengo mengi huishia kuwa malengo ya mwaka unaofuata? Kwa nini watu wengi humaliza mwaka kwa masikitiko –wakati wanapojikuta na hali ile ile ama mbaya zaidi ifikapo mwisho wa mwaka? Kumbuka uamuzi wa kufanya badiliko dogo, ambao unauhakika wa kuendelea nao kwa miezi kumi na miwili, ni wa muhimu kuliko kufanya maamuzi

Heri ya mwaka mpya!

Nikutakieni nyote heri ya mwaka mpya 2011. Mwaka wa matumaini mapya. Mwaka wa maendeleo zaidi. Mwaka wenye changamoto chanya zaidi. Na mwaka wa kujielimisha zaidi ya tunavyoelimisha.