Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2009

Je, tunafikiri kwa kutumia lugha?

Kuna changamoto zimejitokeza kwenye ule mjadala wa tasnifu ya msomi wetu ambayo kwa maoni yaliyotolewa huenda ingekuwa bora kama ingekuwa katika kiswahili. Changamoto kubwa zaidi ni ile iliyoletwa na msomaji Godwin Habib Meghji akihoji ikiwa mwanadamu hufikiri kwa kutumia lugha. Hapa anasema: "Mimi sina uhakika kama binadamu anafikiria kwa kutumia lugha fulani. Viziwi na bubu pia hufikiri". Hii ni changamoto nyingine. Una maoni gani katika hili? Je, tunawezaje kufikiri? Fikra zinauhusiano wowote na lugha? Je, bubu ama kiziwi hana lugha kwa sababu tu hawezi kutamka ama kusikia?

Tembelea Website mpya

Pole na shuguli za kutupasha habari mbali mbali zinazotokea ndani na nje ya Tanzania. Naomba nafasi katika blog yako ili niwajulishe ndugu zangu watanzania kwamba nimetengeneza website www.rusumo.com ambapo wataweza kusikiliza nyimbo mbali mbali za Tanzania kama vile taarab,segere,dance,bongo flava,gospel na nyimbo za kigeni kama vile raggae,za kihindi,pop na nyengine nyingi tu. Pia kuna dictionary ya kisasa kabisa ambayo ina lugha zote za Ulaya na baadhi ya lugha za Asia,katika dictionary hii baada ya kupata tafsiri ya neno pia unaweza kuona picha za neno hilo kwa kubofya upande wa pili wa Ukurasa. Kadhalika wadau wataweza kuona hali ya hewa na wakati wa sehem mbali mbali za dunia. Karibuni sana wadau, ni mimi MSAFIRI ISMAIL RUSUMO. www.rusumo.com

Soma 'tasnifu' ya msomi wa Chuo Kikuu

Mjadala wa lugha gani itumike katika mfumo wetu wa elimu, ni suala la kutia aibu kuliko hata aibu yenyewe. Inadhalilisha sana unaposikia watu wazima hajui tutumie lugha gani kufundishia. Eti tunabishana kipi bora Kiswahili ama Kiingereza, kweli? Fedheha hii inatokana na ukweli kwamba lugha ya kiingereza inayolazimishiwa hivi sasa ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia kwa wanafunzi wengi. Leo nimekuja na ushahidi wa karibu kabisa unaonyesha sura halisi ya tatizo. Nimepata bahati ya kupata karabrasha la 'utafiti' uliofanywa na mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu aliyekuwa anajiandaa kuitetea Digrii yake kwa kuandika 'tasnifu'. Baada ya kusoma vipande vichache vya karabrasha hili naomba uamue mwenyewe kuwa Digrii iliyomwezesha kuandika andiko hili ni halali ama ni feki. Halafu fikiri nani wa kumlaumu: yeye mwenyewe asiyejua lugha ambayo ni ya wakoloni na haitumii kuwasiliana na jamii yake au ni serikali yake isiyoelewa makosa ya kugenisha hadi lugha? Inawezekana kabisa ku

Mkutano wa Copenhagen: Ugaidi wa kimaendeleo

Picha
Hivi sasa dunia yetu inapitia kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wowote. Joto limeongezeka sana. Barafu inayeyuka. Kina cha maji kinaongezeka kwa kasi na kwa kweli ndani ya kipindi kifupi, baadhi ya visiwa vitafurikwa na maji kikiwamo kile cha Zanzibar. Majanga haya yote yamesababishwa na akili ya mwanadamu mwenye fikra potofu ya kile kinachoitwa MAENDELEO. Mwanadamu wa sasa (wa kileo) ndiye hasa chanzo cha dhahama yote hii ambayo kwa sasa imefanyiwa Mkutano maalumu kule Copenhagen ambao ninaamini utaishia wale jamaa kupiga picha ya pamoja na kuja na matamko ya kisiasa then maisha yataendelea kama kawaida. Bonyeza hapa kujua kinachoendelea kwenye mkutano huo na tayari mashindano ya matamko yameanza. Ningependa tufanye tathmini ndogo ya namna ambavyo akili ya mwanadamu wa leo anayejiona kuwa kaendelea kuliko wengine wote waliopita. Moja. Mwanadamu wa leo ameshindwa kabisa kutatua tatizo la utumiaji (ukwapuaji) wa vyanzo vya asili. Akikwapua vikaisha, anahamia kwingine. Aki

Mwezi Desemba na suluba zake

HIVI unajua kuwa mwezi kama huu, mwakani, serikali iliyopo madarakani itakuwa imeenda zake? Hivi hivi tunashuhudia serikali hii ikimaliza muda wake. Namna gani tunalishuhudia hili inategemeana na asomaye mistari hii. Nilisahau hata nilichotaka kusema. Ni bukheri wa afya nasubiria mwisho wa mwaka. Kama kuna mwezi wenye sikukuu kibao ndio huu. Halafu naona kama siku kuu zote hazina mantiki kabisa. Kuanzia hii ya kesho kutwa (ya kusherehekea uhuru usiokuwepo) mpaka zile nyingine za kuadhimisha siku za kiroho kwa ubwabwa na mavazi. Uzuri wa mwezi huu tuna uhakika wa siku kadhaa ambazo tutabaki tumelala nyumbani. Kisa? Hakutakuwa na kazi kwa hivyo ofisi zitafungwa na kama kawaida tutaendeleza kwa kasi umasikini wetu ambao wapo wenzetu wanautumia kuendesha harakati za kuubakiza ili dili lisife. Unakumbuka wakati wa mzee Mwinyi, siku kuu ikiangukia siku za wikendi, basi siku hiyo inahamishiwa Jumatatu ili watu wale raha na kusahau kuhudumia wananchi. Ayaa... nimeenda nje ya pointi. Ni