Je, tunafikiri kwa kutumia lugha?

Kuna changamoto zimejitokeza kwenye ule mjadala wa tasnifu ya msomi wetu ambayo kwa maoni yaliyotolewa huenda ingekuwa bora kama ingekuwa katika kiswahili.

Changamoto kubwa zaidi ni ile iliyoletwa na msomaji Godwin Habib Meghji akihoji ikiwa mwanadamu hufikiri kwa kutumia lugha.

Hapa anasema: "Mimi sina uhakika kama binadamu anafikiria kwa kutumia lugha fulani. Viziwi na bubu pia hufikiri". Hii ni changamoto nyingine.

Una maoni gani katika hili?

Je, tunawezaje kufikiri? Fikra zinauhusiano wowote na lugha?

Je, bubu ama kiziwi hana lugha kwa sababu tu hawezi kutamka ama kusikia?

Maoni

 1. MWANAFALSAFA wewe ni rahisi kufikiria kwa kutumia lugha unayoielewa ingawaje kufikirian hakuna lugha.
  mmmhh nimeshindwa kaka hii nzito

  JibuFuta
 2. Kwa Markus Mpangala.
  NI RAHISI KUKIELEZA KITU ULICHOFIKIRIA KWA LUGHA UNAYOIELEWA VIZURI. Lugha hapa inatumika kama nyenzo tu ya kutoa na kukieleza ulichofikiria. ILA BADO INABAKI PALE PALE(kwa mtazamo wangu)BINADAMU HAFIKIRI KWA KUTUMIA LUGHA

  JibuFuta
 3. Nami naungana na ndugu Meghji kuwa binadamu hafikiri kwa kutumia lugha. Haiwezekani mtu kufikiri kwa kiswahili, kichaga, kingoni au Kiingereza., tusiandikie mate na wino upo, hebu fikiri, kisha jiulize ulikuwa unatumia lugha gani kufikiri.
  Viziwi na bubu nao hufikiri, ni vile tu hawawezi kutoa wayafikiriyo kwa namna ya kawaida ya kuongea. Lakini viziwi na bubu wana namna ya kuwasiliana( sign language) nayo ni lugha kama inavyojieleza kwenye mabano. Je, na wao wanafikiri kwa lugha hii?

  Lugha inaleta kufikiri. Bila lugha hujapata kufikiri.

  JibuFuta
 4. Kwanza:

  LUGHA NI NINI?

  Mtoto akilia mama yake kuna wakati huelewa Mtoto anafikiria nini.:-(

  JibuFuta
 5. Hivi mpaka umefikiri, nini huwa kimetokea kwenye akili?


  Tukijenga mazingira ya bubu kukua hali akiwa katengwa mbali na watu wengine wanaozungumza, je kwa kubashiri bubu huyo anaweza kuwa na hali aliyonayo bubu anayeishi na wasio mabubu?

  Kama ndio, nini kinaleta tofauti baina yao?

  Kama siyo, kwa nini?

  JibuFuta
 6. Ili ufikirie unahitaji michoro mahsusi ubongoni ambayo haiwezekaniki bila lugha husika.
  Unaposema mtu nhafikiri kwa lugha unakosea. Kisaikolojia imethibitika kwamba lugha ni muhimu ili kutengeneza michoro (sina lugha sahihi) hii ambayo ni muhimu kwa aijili ya kufikiri.

  Bubu aliyeishi mahali pasipo na lugha hawezi kufikiri kama yule aliyeishi penye lugha. Sababu ni hiyo hapo juu.

  Yangu yanatosha wakubwa

  Marijani

  JibuFuta
 7. Ndugu anony, mimi nadhani hapa ndugu Bwaya alikuwa anamaanisha kinachoendelea wakati wa kufikiri na si kinacholeta kufikiri. ndio maana hata mimi niliandika hapo juu kuwa lugha ni muhimu katika kuleta kufikiri kwani inaunganisha ubongo na mazingira ya nje. Kwenye ubongo kuna taswira mbalimbali na conceptual frameworks nyingi na ndio maana unaweza kumkumbuka mtu na hata kufananisha vitu mbalimbali. Binafsi bado sijashawishika kuwa tunafikiri kwa kutumia lugha bali lugha ina initiate kufikiri.

  JibuFuta
 8. Kaka Bwaya
  Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
  Baraka kwako

  JibuFuta
 9. Mzee wa Changamoto asante sana kwa salaam. Sijambo nashukuru naendelea vema wakati huu wa sikukuu. Salaam kwa familia yako pia, heri ya mwaka mpya 2010

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3