Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Safari

CCM ni maarufu Kigoma kwa 40.2%, ikifuatiwa na CHADEMA kwa 27.2%

Picha
Utafiti huru uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umeonesha kwamba mgombea yeyote wa nafasi ya Urais wa Chama cha Mapinduzi angeweza kuchaguliwa na wapiga kura wa Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa asilimia 40.2% ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu jioni ya leo.

Unaionaje Dublin kupitia jicho langu?

Picha
Leo nimepata bahati ya kutembea kidogo katika jiji la Dublin. Gari linalotumika kumwezesha mgeni kusafisha macho. Picha: @bwaya         Majengo ya zamani yanayovutia. Picha: @bwaya Mitaa yenye majengo yanayoitwa ya 'King George' wa Uingereza. Ireland ilikuwa koloni kwa miaka mingi. Picha: @bwaya Mto katikati ya Dublin. Picha: @bwaya Mavazi ya wa-Irish Picha: @bwaya Magogoni ya Ireland. Picha: @bwaya

Kupanda na kushuka kwa dini nchini Ireland

Picha
Nimebahatika kutembelea Chuo Kikuu cha Taifa Maynooth, Dublin Ireland. Ni chuo cha zamani sana tangu enzi hizo kikiwaandaa makasisi, kikiitwa St Patrick College. Maynooth University, Ireland. Picha: Jielewe Jambo la ajabu, nimeona picha zinazoeleza idadi ya wanafunzi waliokuwa wanajiunga kuchukua masomo hayo ya Upadre kila mwaka. Idadi inaonekana kupungua kila mwaka, mpaka walipoamua kukigeuza kuwa Chuo Kikuu kifundishe mambo mengine. Madhari ya Maynooth, Dublin. Picha: Jielewe Kwa ujumla, msisimko wa dini haupo nchini humu. Makanisa mengi ya Kikatoliki yamefungwa au kugeuzwa matumizi kusaidia shughuli nyingine. Kanisa maarufu nikiwa jengo la makumbusho. Picha: Jielewe 'Nikiwa hapa, ndiyo kwanza kashfa za makasisi kudhalilisha watoto zinapamba moto. Mambo yamebadilika. Sanamu ya Papa John Paul II alipotembelea hapa. Picha: Jielewe Dublin, mji mkuu wa Ireland ndiko yaliko makazi ya makampuni makubwa ya teknolojia. Ndiko waliko Yahoo! Na makampuni meng...

Guiness: Alama ya Taifa la Ireland

Picha
Kiwanda kinacholinda heshima ya walevi, Dublin, Ireland. Picha: Jielewe Katika bidhaa wanayojivunia wa-Irish, ni pombe maarufu ya Guiness. Ukikatiza mitaa saa za usiku baada ya kazi, wanywaji (najua ni kosa kubwa kuwaita walevi) hawanywi pombe nyinine zaidi ya Guiness. Kila baa ni Guiness. Nawambia mwenyeji wangu sinywi pombe, wananishangaa. 'Utarudije kwenu hujanywa Guiness?' Alama ya Guiness ni nembo ya Taifa. Pombe ni urithi wa taifa. Picha: Jielewe Kitu kingine ambacho nimekigundua, kumbe ile nembo ya Guiness unayoiona, ndiyo nembo ya Taifa. Kwa maana nyingine, wakati sisi urithi wetu ni Ngorongoro na mbuga za wanyama, hawa jamaa, urithi wao ni pombe. Pombe ni urithi wa taifa. Natania. Mtaani kweli imepangwa. Hongereni. Nimekumbuka kwetu. Sisi ni wazalishaji wakubwa wa bangi na mirungi tena kwa wingi sana ingawa kwa siri. Wa-Irish ni wazalishaji wakubwa wa Pombe. Sote letu moja. Unalijua?

Waholanzi na utamaduni wa baiskeli, sisi tunakimbilia magari binafsi

Picha
 Wakati sisi tunashindana kwenda kazini na magari ya bei mbaya, wenzetu wanakuja kazini na baiskeli. Hapa ni Ede, Uholanzi. Baiskeli ndio usafiri maarufu. Jambo hili si la kawaida. Fikiria, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu achilia Profesa wake, apande baiskeli kwenda chuoni. Kwa hakika ni jambo unaloweza kuliewa pale Dar es salaam. Waholanzi wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri. Picha:Jielewe Katika mazingira haya ambapo kila mtu anatafsiri maendeleo kwa kuangalia vitu, na katika mazingira ambayo kila mtu yuko tayari kuonekana naye yupo hata ikibidi kwa mkopo, almuradi aendeshe gari, ni vigumu kupata ufumbuzi wa 'kero' ya kudumu ya foleni jijini Dar es Salaam.  Kila mmoja anafikiri kutatua kero hii kwa kuongeza gari barabarani. Foleni itoke wapi kwa mazingira haya? Picha: Jielewe Kituo cha elimu MDF, Ede, Uholanzi. Picha: Jielewe Hebu fikiri kama watu wangeamua kutumia usafiri wa umma, huu huu uliopo, magari mangapi yangeondoka barabarani? Saa ...

Mitaa ya Nairobi kwa jicho langu

Picha
Foleni ya matatu, abiria wanaingia kwa utaratibu Alama ya jiji la Nairobi, land mark Iliko benki kuu ya kenya Mtaa wa Kimathi, Ofisi za Magazeti ya Nation Pilikapika za mtaa wa Tom Mboya Sanam ya shujaa Tom Mboya Alama za mitaa, zinaonekana uzuri

Mitaa ya Nairobi, 'Usomini UoN'

Picha
Chuo Kikuu cha Nairobi, kinachosemekana kuwa moja wapo ya vyuo bora Afrika Mitaa ya Chuo Kikuu cha Nairobi Ndani ya Chuo, karibu na duka la vitabu Bustani za wazi katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Nairobu Kama ni kweli, sehemu hii haihusiki basi sawa sawa Sijui nielekee wapi, huku au kule? Alama ya utambulisho wa Chuo Kikuu cha Nairobi

Vitabu Uarabuni

Picha
Saa nyingine si vibaya kupitia maeneo haya. Ingawa kuna gharama zake. /> Kwa tusiopenda kazi, ikawa rahisi sana kuona kitabu cha aina hii: Lakini pia si vibaya saa nyingine kujua imani za watu zinavyosemwa na wasio ndani: Hata hivyo, hiyo ikatosha kuwa ni zawadi ya Uarabuni.

Ni usalama wa Taifa au ni ubaguzi wa rangi?

Picha
Tuko ndani ya uwanja wa ndege wa Sao Paulo, Brazil. Ni usiku, tunangoja usafiri wa kwenda Dubai, kama lisaa limoja lijalo. Nimekamata kitabu changu nasoma. Ni kitabu cha rafiki yangu kanigawia nionje yaliyomo. Yeye naye kakaa zake kimya anasoma kitabu changu pia. Saa nyingine tunafunika vitabu, tunazungumza mawili matatu, tunaendelea kupekua pekua. Ni katika kuongoja tu usafiri. Faizul, Deo, Bijoy, na mimi jijini Sao Paulo. Picha: Dr Awab Mara wanatufuata watu wawili waliovaa kiraia. Mmoja kajazia, kajichora tatuu mkononi, kavaa viatu vinavyompyaya. Mtu wa mazoezi. Mwingine mdogo dogo tu, ila shida yake hasemi kiingereza. Kwa hiyo ni "mpole fulani hivi". Baunsa anatuonesha kitambulisho chake. Ni askari wa Kibrazil. "Ninaomba kuona hati yako ya kusafiria tafadhali?"askari bonge ananiambia, mwenzie akimsaidia kwa macho. Nilisita kidogo, nikijiuliza inakuwaje aje kwangu wakati nilikuwa na wasafiri wengine. Ndicho nilichomwuliza. Baada ya kudai kuwa anafanya ...

Mkutano wa wanablogu Santiago

Picha
Nimepata fursa ya kukuhudhuria mkutano wa wanablogu wa jumuiya ya Global Voices unaofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Taifa, Santiago Chile. Moja ya vivutio vya mkutano huo ni kukutana na mwanablogu wa kitanzania aishiye Australia Bw. Joe Nambiza Tungaraza na Njeri Wangari mwanablogu wa mashairi wa Kenya .

Arusha warembo ni majasiri wa kibiashara

Picha
Nimewapenda akina dada hawa wanaojishughulisha na biashara halali kama hizi. Ni majasiri wasiosita kufanya shughuli kama hizi kujipatia kipato licha ya urembo wao. Hapa niliwafuma wakimsubiri mwenzao. Then wakaendelea na shughuli zao. Pongezi kwao.

Mwisho wa mwaka Singida

Picha
Hapa ni sehemu ya mji wa Singida kama ilivyokuwa Krismas ya mwaka huu. Wengine ni Bw. Albert William, mhadhiri msaidizi DUCE (huyu aliwahi kublogu hapa miaka kadhaa iliyopita, bila shaka atarejea tena. Mwingine ni mkewe Krissie, mtafiti wa bayoteknolojia, Mlimani aliyewahi kublogu hapa na kuitelekeza blogu hiyo kwa muda. Na huyo mwingine (mwenye kaki) ni kilaza, mimi.

Viziwi wanaosikia tusivyovisikia...

Singida kwema. Nimekuwa na wakati mzuri na marafiki tulioachana kwa kipindi kirefu. Nimekuwa kiguu na njia utadhani kuku mfungwa aliyeachiwa kwa makosa. Jana nilipata fursa ya kutembelea shule ya viziwi na wasioona, Huruma. Nilikutana na walimu waliojitoa kuwasaidia watu hawa kwa moyo. Ilisisimua kuona viziwi wakipiga soga kwa lugha ya ishara. Walikuwa wenye furaha, kiasi kwamba hakuna kilichoonekana kuwapungukia. Nikajifunza. Kumbe furaha ni vile unavyoamua uwe. Huna haja ya kuwa na vyote ili kuipata. Nilimwona kijana asiyeona wala kusikia, lakini mwenye kusema! Ili kuwasiliana nae, unaandika mkononi mwake, anaelewa, halafu anajibu kwa mdomo! Naye huwezi amini kwa jinsi alivyojaa furaha! Nikaonana na wasioona wenye matumaini. Wasioona, wenye kuona tusivyoviona. Wenye furaha bila kutegemea vionekanavyo. Nikaondoka nikiwa na mawazo tele. Upofu na uziwi ni zaidi ya huu wa mwilini!

Operesheni ya kilimo cha barabara

Nimerejea tena baada ya kumalizana na Kaizari. Nimepita Moshi kwa ufupi Jumamosi, kisha nikaja Singida, kupitia Arusha. Njiani nilishuhudia 'maendeleo' ya kilimo cha barabara. Barabara ya Minjingu-Babati inaparurwa kwa kasi. Ile ya Babati - Katesh - Singida nayo haiko nyuma, mkandarasi yuko 'saiti.' Nakumbuka tukiwa Magugu, abiria mmoja niliyebahatika kukaa naye, mtu wa makamo akaniambia; 'Kijana hivi unajua kwa nini barabara hii inajengwa kwa kasi hivi?' Nikamjibu; '...mzee sina hakika kama najua' Akafunga gazeti alilokuwa analisoma, akanitazama akisema: '...hii ni operesheni pumbaza kuelekea uchaguzi.' akaendelea; '...Nchi hii haitawaliwi kwa mipango ya muda mrefu. Kila kinachofanywa kina nia ya miaka isiyozidi mitano..' Barabara hii italimwa wee mpaka kampeni zifike, waitumie kama mradi wa kuvunia kura, na usishangae mambo yakiishia hapo hapo...' Niko Singida mpaka mwezi wa tisa.

Shule za "yeboyebo" na Mimba za utotoni

Ni ajabu na kweli. Baada ya kubaini kuwa karibu vijana wengi wanaotumia internet hapa Singida, lengo lao ni kujiridhisha na picha za ngono, kumbe lipo tatizo jingine. Mimba za utotoni. Sijafikia kuhalalisha uhusiano uliopo kati ya uangaliaji wa picha za ngono na hili la mimba. Lakini kwa mbali naanza kuhisi. Kwa sababu nimegundua pia kuwa mitaa mingi imesheheni sehemu za kuonyeshea filamu za "kikubwa" ambapo ndiko zilipo prepo za wanafunzi wengi wa shule za yeboyebo (kata). Ukweli ni kwamba siku hizi kila mwanafunzi "anafaulu" kuingia sekondari. Maana tumetoka nyakati zile za kufaulu na bado ukakosa nafasi, mpaka nyakati hizi ambapo unafeli na bado unaambiwa umefaulu. Pamoja na neema ya kufaulu, karibu kila familia ninayoitembelea hapa Singida inauguza maumivu ya binti kuzaa kabla ya wakati. Mabinti wa shule za msingi na sekondari wanapachikwa mimba (Mara nyingine na waalimu wao ambao wengi ni wale wa voda fasta). Wale walioshindwa kuendelea na masomo wanazalia ...

Rariki yangu Rama muuza magazeti

Kazi ya kwanza niliyoifanya baada ya kufika Singida ni kulazimisha matangazo ya blogu zetu. nimekuwa nikibadili 'settings' kwenye kila kompyuta niliyoitumia kwa kubadili 'home page' iliyopo kuwa blogu moja wapo kati ya nyingi tulizonazo watanzania. Nimebadili badili baadhi ya kopyuta na mpaka sasa kuna kama blogu kumi hivi kama home page. Kwahiyo, kama inavyotarajiwa, kila mtumiaji wa kompyuta husika anapojaribu kuingia mtandaoni, atasalimiwa na blogu ya kiswahili. Hiyo nadhani inaongeza wigo wa blogu zetu. Nilifanya hivyo pia kwa baadhi ya miji niliyopita mwaka huu. Nadhani inasaidia kuzitangaza blogu. Ukweli ni kwamba bado matumizi ya mtandao yamekuwa zaidi katika kuandikiana barua pepe na mambo yetu yaleee niliyoyasimulia juzi. Hata ivyo naamini mabadiliko hata kama yanaonekana kwenda taratibu, bado yanakuja. Ni wajibu wetu kuyachochea. Leo nimekuja kwenye cafe nyingine. Hii kidogo iko wazi sio kama ile iliyokuwa imefunikwa gubi gubi. Kuna jamaa hapa tumekaa ka...

Singida: Here I come

Niko Singida. Baada ya kufika niliona ingefaa kupata huduma ya intaneti cafe. La haula! Nakutana na picha za ngono. Nahisi jamaa aliyekuwa akitumia kompyuta hii ndio kazi kubwa iliyomleta hapa. Uzuri, kama kweli ni uzuri, kompyuta za hapa zimewekewa uzio. Privacy. Unafanya kile unapenda bila hofu ya kuichunguliwa. Waswahili ukiwapa uhuru, ndo umeharibu kabisa. Jamaa aliyeondoka hapa ni mtu na heshima zake. Tai. Suti na vitu kama hivyo. Mtu na ofisi yake bila shaka. Sitaki kuamini kwamba ndicho alichokuwa anakifanya hapa. Ni lini net zitatumika kwa mambo ya maana, hilo ndilo twapaswa kujiuliza. Vijana wanajazana net siku hizi. Usifikiri (wengi wao) wanafanya vya maana. Ngono ndugu msomaji. Hivi hata nilitaka kuandika nini hata nimeshahau. Kwa nini ngono? Labda anajifunza lakini. Tuchukulie anajifunza. Sasa kujifunza kupi kwa picha za mnato wajameni? Mjadala hapa. Au tuwashauri wenye net waondoe uhuru? No. Hilo sio jibu. Siku hizi kuna simu. Watu "wanafaidi" mambo haya waki...

Safari zinavyotukutanisha na mengi

Nimekuwa na pilika pilika za hapa na pale. Sehemu kubwa ya muda wangu nikiutumia katika vijiji vyetu. Nilianzia Morogoro. Tukuyu. Kyela. Baridi ile mbaya. Watu wanalima kahawa wa kununua haonekani. Akiwepo basi bei ni ya kutupa. Mtu unajiuliza hivi ni lini wakulima watapata thamani sawa na watu wengine? Mwananchi anahangaika na mashamba ambayo hayamsaidii kujikwamua. Watu wamekata tamaa. Ndugu zangu tuache kufarijiana. Wananchi wamekata tamaa. Majuma kadhaa ya mwezi Julai nimeyatumia Tunduma na Vwawa. Watu wanaishi maisha magumu sana. Wanajua kuwa nchi yao inazo hela, lakini zinaliwa na walafi wachache. Ukitaka kuijua Tanzania, usiishie dasalama. Vwawa na Mbozi panaweza kukupa picha ya nchi yetu. Nikiwa Mbeya mjini nikajaribu kupandisha picha kwenye blogu, ikawa ngumu. Hata sijui palikuwa na nini hapo. Nikiwa Ipogolo Iringa nako sikuweza kukaa na kuandika. Juma moja likaishia Dodoma nikiwa na heka heka nyingi kidogo. Nikadhani nikiwa Singida ningeandika. Wapi bwana. Singida ndio ...