Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mahojiano

ChatGPT Inapoaminika Kuliko Mzazi

Picha
Jioni moja wiki iliyopita nilikuwa Instabul. Huu ni mgahawa mmoja maarufu jijini Dar es salaam. Hapa nafanya nazungumza na Damari, mwanafunzi wa shahada katika taasisi moja ya elimu ya juu jijini Dar es salaam. Sikumwuuliza umri lakini nakadiria ana miaka 21. Kikao chetu kimezaliwa na kipindi nilichokuwa nimekifanya asubuhi hiyo kwenye kituo kimoja cha televisheni.   Tulizungumza kwa kirefu suala alilokuwa nalo na tufikia muafaka. Kisha nilimwuuliza swali ambalo huwa nawauliza ‘wadogo’ zake ninapokuwa naendesha mafunzo ya malezi shuleni.  "Nani ni rafiki yako wa karibu?" Nalenga kujua anamwamini nani.  Hakufikiri mara mbili akanijibu, "ChatGPT!” Sikuzuia mshangao. Jambo hili, kwa hakika, lilinisumbua. Sikuwahi kufikiri ChatGPT ingewahi kuwa rafiki wa mtu. Kama huifahamu, ChatGPT ni programu tumizi inayotumia teknolojia ya akili mnemba. Imentegenezwa kuwezesha mazungumzo yanayolingana na unachoulizia.    “Umesema ChatGPT ndio rafiki yako?” “Ndio. Rafiki ninayemwa...

Madikteta wa Familia Tunaweza Kudai Demokrasia?

Picha
Madai kuwa baadhi ya watawala wetu wa ki-Afrika ni madikteta hayashangazi. Inasemekana watawala hawa  hawasikilizi maoni ya watu wanaowaongoza, hawashauriki wakati mwingine na watu walioteuliwa kuwashauri, wanaminya uhuru wa maoni/kujieleza na kadhalika. Madai haya yanaonekana kuwa ni matamanio ya wananchi kuwa na serikali zinazoheshimu demokrasia -nguvu ya wananchi kushiriki katika uongozi/utawala wa taifa lao kwa kuamua utaratibu gani utatumika kujitawala na nani anaweza kupewa jukumu la kuwaongoza. Haya yote yanadai ushirikishwaji wa wananchi kwa kukuza uhuru wa kila raia kusema/kutoa maoni na kadhalika.

Wanafunzi waonyesha namna teknolojia rahisi inavyoweza kurahisisha upigaji kura bila kufika kituoni

Picha
NIMEFIKA hapa Diamond Jubilee kama mwananchi anayetamani kujionea hamasa waliyonayo wanasayansi chipukizi kuonyesha kazi zao nzuri. Ni maonyesho ya tatu ya Sayansi katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambayo hatimaye hapo kesho yatawaibua wanafunzi wawili kama washindi wa tatu wa shindano la wanasayansi chipukizi hapa nchini linaloandaliwa na Young Scientists Tanzania. Baadhi ya washiriki kwenye ufunguzi wa maonyesho leo. Picha: @bwaya Kwa hakika hamasa ni kubwa. Wanafunzi wamejawa na msisimko wa aina yake kuonyesha matokeo ya tafiti zao walizozifanya tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Wamejawa na matumaini, hasa kwa sababu ya maneno ya ufunguzi yaliyosemwa na Mkurugenzi wa YST, Dk Kamugisha wakati akiwakaribisha asubuhi ya leo. "Tulipata maombi ya kushiriki kutoka shule zaidi ya 200...lakini ni maombi 100 pekee yalifanikiwa kupenya katika mchujo. Mpaka hapo ninyi ni washindi. Kilicho muhimu zaidi, ni kwamba pamoja na kwamba kazi zenu zitapitiwa na watu wanaoelewa vyema zaidi maene...

‘Vijana waache kutumiwa’

Picha
JINA LA KAMALA si geni kwa wanablogu wengi. Yeye ni mwendeshaji wa blogu maarufu inayojadili (pamoja na mambo mengine) masuala ya kiutambuzi. Bonyeza hapa kuitembelea . Ndugu Kamala anajulikana pia kwa namna yake ya utoaji maoni huru katika blogu anazozitembelea ambayo hufikirisha na mara nyingine kuibua mijadala zaidi. Blogu hii ilipata fursa ya kuzungumza naye siku chache zilizopita kuhusu falsafa zake, blogu, dini, siasa na mambo yake binafsi. Karibu kujua zaidi kuhusu mwanablogu huyu anayeblogu kutokea kanda ya ziwa. ________________________________________ Ndugu Kamala, nashukuru kwa kukubali kutumia muda wako ili tuweze kujadiliana masuala mawili matatu. Labda tuanze na falsafa yako binafsi. Unaamini nini katika maisha ambacho ndicho kinachobeba utambulisho wako kama Kamala? Naamini katika utu, ubinadamu, upendo na umoja. Napenda kuelewa vitu na kudadisi na ndio maana natumia majina ya kihaya tu ninayoelewa maana yake na kwa nini yawepo… napenda kuacha maisha yaende na kuf...

Mazungumzo na Kamala Luta

Siku chache zilizopita nilipata bahati ya kufanya mazungumzo mafupi na Bw. Kamala Luta, mwanablogu machachari ambaye si mara moja amewahi kuibua mijadala mizito kupitia maoni yake huru ama makala kwenye blogu yake. Kaa mkao wa kula. Nitayachapisha mazungumzo yake mapema sana namalizia kuweka koma, nukta na funga semi.

Unayatumiaje masaa ishirini na mane?

Binadamu wote ni sawa kwa maana nyingi. Usawa mmoja wapo ni kiasi cha muda ambacho kila mmoja wetu anacho. Kila binadamu anayo masaa ishirini na mane kwa siku. Masaa yaliyotimia yenye dakika sitini. Kinacholeta tofauti, ni namna tunavyoyatumia masaa haya kwa faida. Kile tunachofanya katika kila 'lisaa' linalopita mikononi mwetu. Wakati wapo wanaoweza kupangilia mgawanyo wa muda kwa siku inayofuata, na kutathimini adabu waliyo nayo kwa kile walichopanga, wengi tunajikuta tunafanya yale tusiyoyapanga na hivyo hatuna namna ya kutathmini matendo yetu ya siku. Watumiaji wazuri wa muda wanao uwezo mzuri wa kusema 'hapana sikupanga hili' wakati watumiwaji wa muda hawana uwezo huo. Ninaposhindwa kusema hapana mahala ambapo nilipaswa kufanya hivyo, ni namna bora zaidi ya kuteketeza muda. Ikiwa tutaweza kudhibiti matumizi ya muda, tutakuwa tumeweza kuyadhibiti maisha yetu.

Gwamaka: Kile tusichofundishwa madarasani

Leo nilipata fursa ya kupata chakula cha mchana na rafiki yangu Gwamaka. Gwamaka ni kijana mwenye changamoto nyingi. Ukiongea naye hukosi jipya. Ni mwanaharakati, mwanafalsafa mwenye kichwa kinachofikiri. Ni msomaji mzuri wa vitabu. Na unaweza kubashiri inakuwaje ukikutana na msomaji wa vitabu kama Gwamaka. Ni lazima nikiri kuwa vitabu vingi nilivyosoma, yeye ndiye alinishawishi. Hivi sasa kaniambia anasoma kitabu kiitwacho: Why we need you rich . Ameniahidi kuwa kina mambo mazuri katika eneo la fedha. Japo sijawa msomaji mzuri wa vitabu vya "fedha" nimeshawishika kukitafuta. Kwa hiyo unaweza kuona kwa nini tukio la kukutana naye huwa na umuhimu wa aina yake kwangu. Basi. Gwamaka alipomaliza 'shule' aliamua kujikita katika shughuli binafsi. Hataki kuajiriwa. Aliwahi kuajiriwa miezi michache akaona sio. Hivi sasa yuko kwenye mchakato wa kutengeneza ofisi yake mwenyewe pale Mwenge, barabara ya Sam Nujoma. Mambo ya ujasiria mali. Kupata, kadiri ya unavyowekeza. Anayo...

Kura nipige mimi, kula wale wenyewe?

Niko saluni jioni Jumamosi. Kuna vijana wanne. Umri wao wote ni kati ya miaka 20-30. Kinyozi: (Huku akininyoa baada ya kimya kifupi)…Ee bwana watu wengine noma. Mie: Imekuwaje? Kinyozi: Hapa watu karibu wapigane kisa Simba (timu ya mpira wa miguu) kafungwa mbili na Azam kitimu kidogo... Mie: Kwani tatizo ni nini? Kinyozi: Tatizo ni kwamba wanaopigana hata kadi za uanachama hawana. Mie: Labda ushabiki si unajua tena…au wewe hushabikii mpira? Kinyozi: Mi hata sifuatilii sana mambo ya kijinga haya. Mi nafuatilia mambo yangu bwana. Mie: Kwa hiyo mpira hufuatilii kabisa? Kinyozi: Hata mara moja bosi wangu. Upuuzi mtupu. (Akalalamikia uongozi mbaya wa timu zetu kwa zaidi ya dakika tano kisha…) Mi labda timu za Ulaya. Napenda Aseno. (Akatumia dakika kadhaa kuifagilia) Mie: Una kadi ya Aseno? Kinyozi: (Akicheka) Sina ila sipigani wakifungwa Mie: Sasa hapa home unafuatilia nini? Kinyozi: Bongo nifuatilie nini hapa pamechoka hivi… kwanza ningekuwa na uwezo ningezamia...

Maisha hayawezekani bila wanasiasa?

Kama kuna 'kazi' ambazo zinanitatanisha ni zile zenye uhusiano wa moja kwa moja na kile kinachoitwa siasa. Kazi hizi zimepata umaarufu sana katika nchi za dunia ya tano ikiwamo Tanzania. Kuna wanaoamini kuwa siasa ni porojo. Siasa ni usanii. Siasa ni uchezewaji wa wazi wa akili za watawaliwa. Udanganyifu. Utapeli wa wazi. Siasa. Sina hakika kama ninakubaliana na mawazo haya. Bado natafakari. Kwamba siasa ina uhusiano na maendeleo yetu (hasa sisi wa dunia ya tano) hilo ni jambo la kufikirisha. Siku hizi siasa imekuwa kama muziki wa Bongo Flava. Kila mtu anataka kujihusisha nayo. Wataalamu wa fani mbambali wenye ujuzi adhimu, wanazitosa ofisi zao na kukimbilia siasa. Tunawafahamu walimu wa Vyuo Vikuu ambao hata hawana haiba ya siasa, bado walidiriki kuzitosa ofisi zao. Kisa? Ulaji. Samahani siasa. Na idaidi yao haihesabiki. Mtu unajiuliza mwananchi aliyesomeshwa kwa fedha ya walipa kodi fukara, na akawa mathalani daktari bingwa, ama mtaalam wa uchumi kwa mfano, anaachana ...