Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2017

Namna ya Kutambua na Kukuza Kipaji cha Mtoto -2

Picha
Katika makala yaliyopita tuliona mambo yanayoweza kujenga kipaji cha mtu na uhusiano wa kipaji na mafanikio katika maisha. Kufurahia kile unachokifanya kazini au katika shughuli nyinginezo kunategemeana na namna unavyotumia vipawa ulivyozaliwa navyo. Kadhalika, tulibainisha umuhimu wa wazazi kufanya kazi ya kuwasaidia watoto kubaini vipaji vyao mapema. Kufanya hivyo ni kujaza pengo la mitaala yetu ambayo kimsingi haifanyi mengi katika kuibua na kukuza vipaji vya watoto.

Namna ya Kutambua na Kukuza Kipaji cha Mwanao -1

Picha
Kila mtoto ana kipaji. Ingawa ni kweli kuwa watu wengi hawatambui vipaji vyao, hiyo hata hivyo, haimaanishi hawana vipaji. Zipo sababu nyingi zinazofanya watu wasitambue vipaji vyao. Kwanza, ni mfumo rasmi wa elimu unaotumia tafsiri finyu ya uwezo wa kiakili.

Mambo ya Kuzingatia Unapompeleka Mwanao Kwenye Kituo Cha Malezi

Picha
Watafiti wa malezi ya watoto wamejaribu kuangalia namna gani huduma za malezi ya kituoni –day care yanavyoweza kuboreshwa. Moja wapo ya watafiti maarufu katika eneo hili ni   Taasisi ya Marekani ya Mtandao wa Afya ya Mtoto na Maendeleo ya Utafiti wa Malezi ya Watoto (NICHD) . Maswali ya msingi yanayojaribu kujibiwa na tafiti hizi ni ikiwa kuna uhusiano wa ubora wa huduma zinazotolewa na vituo hivi na makuzi ya mtoto katika nyanja za kiakili, kihisia, kimwili na kistadi; aina ya mazingira yanayoweza kuhusianishwa na ukuaji mzuri wa kihisia na kiakili kwa mtoto na kiasi cha masaa kinachopendekezwa kwa mtoto kulelewa katika kituo kwa siku/juma.

Hatua za Kuchukua Unapoamua Kuacha Kazi -1

Picha
Kuacha kazi si jambo dogo. Lakini zipo sababu kadhaa zinazoweza kukufanya uamue kuacha kazi. Mosi, kupata kazi mpya. Unapoitwa kuanza rasmi kazi uliyoomba, ni vigumu kuendelea na kazi uliyonayo. Kwa kuwa ni vigumu kuwa na ajira mbili kwa wakati moja, mara nyingi utalazimika kuacha kazi uliyonayo. Pia inawezekana umeshindwa kuendelea na kazi uliyonayo hivi sasa. Ingawa haishauriwi kuacha kazi bila kuwa na uhakiki wa kazi nyingine, hutokea mtu akafikiri kwa kina, akapata ushauri wa kitaalam na kujiridhisha kuwa ugumu wa mazingira ya kazi haumruhusu kuendelea na kazi aliyonayo.

Mbinu Nne za Kukuza Ubunifu wa Mtoto

Picha
Ubunifu ni uwezo wa kufikiri, kutafuta majibu au kutatua changamoto kwa namna isiyotarajiwa. Mtu mbunifu hufanya mambo kwa namna isiyo ya kawaida. Hafanyi vitu fulani kwa sababu ameona watu wakifanya. Hafuati mazoea wala uzoefu. Huwa tayari kufanya mambo mapya. Ingawa kuna uhusiano mdogo kati ya ubunifu na uwezo wa jumla wa akili, kwa kawaida, mtu mwenye akili si lazima awe mbunifu. Unaweza kuwa na akili ya kuchambua, kuelewa, kukumbuka na kueleza mambo unayojifunza lakini usiweze kufanya mambo kinyume na mazoea.

Faida, Hasara za Vituo vya Kulea Watoto

Picha
TUMEKUWA tukijadili changamoto zinazowakabili wazazi wanaofanya kazi mbali na nyumbani. Njia kadhaa zinatumika kukabiliana na changamoto hizi. Moja wapo, ni kuwaajiri wasichana wa kazi kwa lengo la kusaidia kuwalea watoto. Tulipendekeza kuwa msingi mkuu wa kupunguza changamoto za huduma hizi zinazotolewa na wasichana wa kazi ni kujenga nao mahusiano mazuri ya kifamilia na kikazi. Mahusiano haya yanawajengea motisha ya kufanya kazi kwa uadilifu na moyo wa kujituma.

Jinsi ya Kumsaidia Mtoto Kuchagua Masomo

Picha
Mfumo wa elimu yetu humtaka mtoto kusoma masomo yote kuanzia darasa la awali mpaka angalao kidato cha pili. Matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yanakuwa kipimo cha aina ya masomo ambayo mtoto anaweza kuyawekea mkazo zaidi. Mkazo anaouweka katika baadhi ya masomo unaitwa mchepuo. Mchepuo ni njia anayoichagua mtoto kufanya maandalizi ya kuelekea kule anakolenga kwenda baada ya kuhitimu masomo yake.

Tabia Saba Zitakazokuwezesha Kutekeleza Malengo Unayojiwekea

Picha
KUANZA kwa mwaka mpya kunaambatana na matarajio mengi. Tunapoingia mwaka mpya tunamani kubadili maeneo mengi katika maisha yetu. Tunatamani kuwa na maisha bora yenye tija kiuchumi, kijamii, kiimani na kwenye maeneo mengine. Hata hivyo, katika kutekeleza malengo yako, ni dhahiri kuwa zipo baadhi ya tabia ulizonazo zinazoweza kuwa kikwazo katika kutekeleza malengo ya mwaka huu. Unahitaji kubadili tabia ili uweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza malengo yako.