Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Elimu na Jamii

Jifunze Uhusiano wa Malezi na Vilema vya Haiba (Personality Disorders)

Picha
Kizazi chetu kinakabiliwa na magonjwa mengi yasiyoonekana. Tunaumwa, na wakati mwingine taabani, lakini hatujui kuwa tunaumwa. Tunatembea, tunakutana na watu, tunapiga picha zenye nyuso zilizochangamka, tunaonekana kufurahia maisha lakini tunateseka na mahangaiko mengi tusiyoweza kuyasema.   Tazama kiwango chetu cha ukatili. Haiwezi kuwa kawaida, kwa mfano, kuona mwenzako anaumizwa na wala hujali. Unamuumiza mtu na bado unashangaa kwa nini analalamika. Unamtesa mwenzako kihisia na bado unamdhihaki anapougulia maumivu. Unajiuliza, tumefikaje mahali mwanadamu unaweza kumtesa mwenzako, ukamsababishia maumivu na hujisikii kujutia.    Mbaya, wakati mwingine, kiwango hiki cha ukatili kinakuwa kama nyenzo ya kupata tunachokitaka. Tunataka madaraka, tunataka umaarufu, mali na kila kinachotufanya kujione tunnawazidi wengine. Tunakuwa waraibu wa ukatili dhidi ya binadamu wenzetu na hatujisikii kujutia. Tazama kiwango chetu cha ubinafsi. Kwa nini tumepoteza uwezo wa kuafikiria hisia...

Usidanganyike. Wema huanzia nyumbani.

Picha
Umewahi kukutana na mtu mwema kiasi kwamba unawaonea ‘wivu’ familia yake? Unajiuliza, “kama huyu jamaa anaweza kuwa mkarimu hivi kwa sisi wapita njia tusiomhusu kivile, nyumbani kwake si watakuwa wanamfaidi sana?” Sasa usinielewe vibaya. Silengi kukukatisha tamaa. Ni vile tu nimeshangazwa hivi majuzi.   Godi ni rafiki yangu wa siku nyingi. Kwa hulka, ni mtu mchangamfu mwenye wingi wa bashasha. Kaa na Godi mzungumze utapenda namna yake ya kuzungumzia masuala. Godi anajua aseme nini wapi na kwa nani.   Halafu kuna wema. Godi hasubiri umtafute. Haipiti wiki hajakupigia na wala hatakuuliza kwa nini humpigii. Hivyo. Ukiwa na shida, Godi huyu hapa. Hana uwezo sana kifedha. Maisha yake ni haya haya kama ya wengi wetu. Sema ni ule utajiri tu wa roho ya mtu. Usha’nfahamu? Godi. Ukiniuliza mtu mwema nimewahi kukutana naye, nitakwambia Godi bila hata kupepesa macho.   Jamaa yetu mmoja aliwahi kumsifia kiutani lakini alikuwa sahihi. Kwa jinsi alivyo mwema, jamaa alisema, ...

Usiyempenda anaweza kuwa baba wa mwanao?

Picha
  Watoto wanahitaji uwepo wa mzazi. Simulizi la Slaquara lilitukumbusha hakuna muujiza kwenye malezi. Mzazi unavuna ulichopanda. Renee anakazia funzo hilo. “Umeongelea athari za umbali kati ya mzazi na mwanae. Nayajua maumivu yake,” anasita na kufafanua, “Sikumbuki lini niliongea na mama yangu. Siwezi kusema ni adui yangu lakini sio mtu naweza kumtegemea kwa lolote.”   “Mara ya mwisho kuonana naye ni miaka miwili iliyopita alipokuja kusuluhisha mgogoro wangu na mzazi mwenzangu,” leso anayoitumia kujifutia inalowa machozi. Renee anaikunjua na kuigeuza kutafuta penye ukavu. “Nilimpa nafasi ya pili akaitumia vibaya. Badala ya kusikiliza upande wangu anielewe, aling’ang’ania kuwa upande wa yule mwanaume akinilazimisha kuishi naye. Hakutaka kabisa kuelewa kwa nini nilichagua abaki kuwa mzazi mwenzangu na si zaidi ya hapo.”   Mgororo huu mkubwa wa mzazi na mwanae umeanzia wapi? Renee anasimulia, “Nimekuzwa kama mtoto yatima. Nasimuliwa baba alipofariki nikiwa mdogo sana...

Mbinu za Kumshirikisha Mwanafunzi Katika Ujifunzaji

Picha
PICHA:  United Nations Majuzi niliwatembelea walimu wanafunzi waliokuwa wakiendelea na mazoezi ya ufundishaji. Mafunzo kwa vitendo yana umuhimu wa kipekee katika maandalizi ya walimu. Katika kipindi hiki, mwanafunzi anapewa fursa ya kutumia maarifa aliyojifunza darasani katika mazingira halisi ya kazi. Kwa mwalimu, kama mimi, hiki ni kipindi cha kutathmini uwezo wa mwanafunzi wa ualimu kumudu majukumu yake. Moja wapo ya vipindi vingi nilivyopata bahati ya kuhudhuria ni Baiolojia kidato cha III kilichokuwa kikifundishwa na mwanafunzi wangu wa mwaka wa II. Baada ya kufanya utangulizi wa somo lake, mwalimu huyu mwanafunzi aliwaelekeza wanafunzi wake kukaa katika makundi ya watu watano watano kusudi wafanye majadiliano. Majadiliano ni mbinu muhimu ya ufundishaji inayowawezesha wanafunzi kujifunza. Kama tulivyosema kwenye makala yaliyopita, kupitia majadiliano, mwanafunzi hupata fursa ya kusikiliza mtazamo tofauti kutoka kwa wenzake. Aidha, majadiliano ni mb...