Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2010

Wasemavyo wanablogu kuhusu Uchaguzi Mkuu

Ifikapo tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania zaidi ya milioni 19.6 watafanya uamuzi muhimu kuhusu hatma ya nchi yao. Watafanya hivyo kupitia uchaguzi mkuu wa nne chini ya mfumo wa vyama vingi. Wakati zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi huo, ulimwengu wa blogu wa Tanzania nao unafuatilia kwa karibu yale yanayotokea katika kampeni za vyama mbalimbali. Hapa Deogratias Simba wa Global Voices on line anatukusanyia habari kutoka kwa wanablogu. Bonyeza hapa kusoma makala nzima. Ukitaka kwa kiingereza bonyeza hapa . Unaweza pia kusoma makala nyingine kupitia ukurasa huu wa kiswahili wa Global Voices.

Mnalipwa kwa kushabikia upuuzi?

TULIWAHI kujadili wakati fulani tafsiri hasa ya msomi na usomi. Mimi bado ninaamini nchi yetu ina uhaba mkubwa wa watu wenye hadhi hiyo nyeti. Wengi wetu ni wasomaji kwa maana ya kuwa na uwezo kujua vitabu vimeandikwa nini na kwa kweli ninaamini ‘wasomi’ tulioanao hawatusaidii. Tunafahamu kabisa kwamba uchakachuaji/kughushi ni sehemu muhimu ya mfumo wa elimu yetu. Ndivyo tulivyojengwa. Ndio maana hata sikushangazwa na tafiti za hivi karibuni zilizokuwa na nia ya kubashiri nani na/au chama gani kinakubalika zaidi. Wewe fikiria kama, na si mara moja, mwanafunzi anaweza kabisa kuandaa ripoti ya kisayansi mezani (bila hata kutafuta data maabara) na ikatua mikononi mwa mwalimu wake naye aipitishe; ni nini cha ajabu kwenye tafiti hizi? Umekuwepo mjadala wa kuhoji uhalali wa kuwatumia sampuli ya watu 2000 ili kujua maoni ya watu milioni arobaini. Watu wanadai how comes? Pengine ni vyema kukumbushana kuwa ni kweli inawezekana kabisa maoni ya watu elfu mbili yakajirudia rudia ama kujenga p

Tunapenda ushirikina kuliko vitabu - Prof. Mbele

Picha
"...Umaafuru wa kitabu hiki (Rich Dad Poor Dad) nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita. Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma. Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili. Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wana

Pendekezo la kitabu: Rich Dad Poor Day

Picha
Kama hujawahi kukisoma hiki, kuna mengi unayakosa. Harakisha kukitafuta! Nakisoma kwa mara ya tatu sasa, sijakichoka!

Ujumbe wa Juma: Wapiga kura waumbueni REDET

"...Wapiga kura wasianze kukata tamaa kuwa CCM wataiba kura. Of course wataiba lakini ili 'kura zitoshe' watalazimika kufanya wizi wa 'mchana mweupe' (day light robbery) jambo ambalo sio rahisi sana,japo linawezekana.Wanaweza tu kuchakachua matokeo kama,kwa mfano Dokta Slaa akipata asilimia 51 na Kikwete asilimia 49.Hapo watarejea uchakachuaji kama ule wa Zanzibar.Lakini kama ni tofauti ya double digits,wanaweza kupatwa na kigugumizi katika kufanikisha ujambazi huo. Ni muhimu kutovunjwa moyo na hujuma hizi.Yatupasa kufahamu kuwa Kikwete na CCM yake ni kama mgonjwa mahututi ambaye yuko tayari hata kuning'inia kwenye uzi ili asalimike.Tutashuhudia vituko zaidi ya huo uchakachuaji wa REDET..." Kwa makala nzima bonyeza hapa . Asante sana Ndugu Evarist Chahali wa kulikoni Ughaibuni .

Ujumbe wa wiki hii

Picha
NAANDIKA makala hii kwa moyo wa upendo, mtu unayempenda ni lazima umwambie ukweli. Ukimficha ukweli unakuwa humpendi; ni kweli ukweli unauma na mara nyingi hatupendi kabisa kusikia ukweli; hata hivyo hakuna wa kutengua kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa vile Mungu hatukutani naye uso kwa uso, bali tunakutana naye kupitia kwa binadamu wenzetu; ni haki kusema kwamba msema kweli ni mpenzi wa watu? Naandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania. (Picha ya Kijiji cha Mjengwa) Hii ni aina ya barua ya wazi kwa wale wanaotamani kuendelea kutawala wakati miaka ya kustaafu inakaribia. Labda kuna haja ya kuongeza miaka hii ya kustaafu. Miaka sitini ya sasa watu wanakuwa bado wana nguvu na kutaka kuendelea kutumika au kula “utamu” wa uongozi. Kwa vile sasa hivi umri huu haujasogezwa mbele, kuna haja kuwakumbusha ndugu zetu ambao bado wana “Ambition” ya kutaka kuendelea na mbio hizi za hata kukalia viti muhimu kama urais na uspika, kwa