Ukitaka Kujifunza Waruhusu Watu Waone Usichokiona
UKIFUATILIA mazungumzo ya wa-Tanzania wengi kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kuona namna watu wanavyojinasibu kujua. Mijadala mingi imejaa ‘ujuaji’ unaofanya watu wajigambe, wadhihaki wengine, watukane na wakati mwingine, kadri ya mamlaka yao, watake kulazimisha kile wanachokiona wao ndio kiwe ukweli usiopingika. Katika makala haya, ninajaribu kuonesha kuwa ili tujenge jamii ya watu wastaabu wanaoheshimiana lazima tuwe tayari kujifunza hata katika mazingira ambayo tunaamini tunajua.