Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2007

Shinto: Dini iliyoanzia Japani na kuishia Japani.

Nchi zilipokea dini zilizokuwa zimeanzishwa katika nchi nyingine. Inaaminika kuwa dini hizi zilipokelewa bila tafakuri ama kwa sababu ya kupumbazwa na ubunifu ulikuwa ukitumiwa na waenezaji wa dini hizo. Katika Japani, hali ni tofauti kidogo. Wajapani walianzisha na kuamua kuienzi dini yao maarufu ya Shinto ambayo yaweza kuchukuliwa - hasa na watu waliathirika na umagharibi- kuwa ni kishenzi. Maana kwa watu hawa dini ya kweli ni ile yenyeuhusiano wa jinsi yoyote na wale jamaa wanaopambana na ugaidi. Shinto ni dini iliyoanzishwa Japani na inaonekana kushindwa kuvuka mipaka ya Japani. Lakini inayo umaarufu wake nchini humo. Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu dini hii yenye waumini wasiozidi milioni 4 duniani. Nitapandisha maelezo mafupi kuhusu Urastafariani hivi karibuni.