Gharama ya kusema ukweli inazidi gharama ya kuongopa? -3
TUMEJARIBU kuonyesha sababu za watu kutokuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo. Sababu zote zinafungwa kwenye fungu moja: Hofu ya kukataliwa . Hofu ya kushusha hadhi. Faida ya ukweli huonekana pale ambapo ukweli wenyewe utatusaidia sisi kukubaliwa na watakaousikia. Mume awapo mkutanoni, mahali panapomsaidia kuonekana anawajibika kwa familia yake na mwajiri wake, hawezi kudanganya. Kusema yuko mkutanoni kunamsaidia isipokuwa kama ukweli huo unaweza kuhatarisha heshima yake. Katika mazingira ambayo ukweli hauwezi kusaidia kulinda heshima yetu, hatuwezi kuwa tayari kuusema. Hapa ndipo tunapojikuta tukiusema ukweli nusu nusu au kwa lugha nyingine uongo. Katika kujua gharama ya ukweli, waweza kutazama hata namna ambavyo viongozi wa dini wanaohubiri umuhimu wa ukweli wanapojikuta nao wakishindwa kuusema ukweli halisi pale ambapo ukweli huo unahatarisha usalama wao binafsi au wa taasisi wanazoziongoza. Ni nadra kwa mfano kumsikia kiongozi wa dini aliyetoa kauli yenye ukakasi kuhusu sual...