Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2011

Take the Risk cha Ben Carson

Picha
Ndio kwanza nimeanza kukisoma. Take the Risk: learning to identify, Choose and Live with accepatable Risk. Kimeandikwa na Mganga Ben Carson kwa msaada wa Gregg Lewis na kuchapishwa na Zondervan Publishing House mwaka 2008. Kitabu kinaanza na masimulizi ya upasuaji mgumu uliofanyika Julai 2003 kuwatenganisha Ladan na Laleh, mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana sehemu ya vichwa vyao. Mapacha hao hata hivyo walifariki dunia wakiwa na umri wa miaka 29 wakati upasuaji huo ukiendelea huko Singapore. Katika kitabu hiki, mwandishi anajaribu kutupatia somo lilitokana na Upasuaji huo. Ladan na Laleh raia wa Iran muda mfupi kabla ya upasuaji huo uliofanyika Julai 2003.

Elimu pasipo maandishi inawezekana?

Picha
Pamoja na ukweli kuwa wengi wetu tunayakwepa maandishi, lakini hiyo haimaanishi kuwa hatuna kiu ya kujifunza. Pichani, wananchi wa mjini Moshi wakionekana kuvutiwa na matumizi ya video katika kuelimika. Picha: Sayuni Philip