Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2018

Pay $900? I quit blogging

Picha
Global Voices Citizen Media Summit in Cebu, The Philippines in 2015. Photo Courtesy of Global Voices I started my blog in 2005. I was among very few Tanzanians who were inspired by Ndesanjo Macha to start blogging.  For those of you who do not know, the history of Tanzanian blogosphere recognizes the contribution of this great man. His influential  weekly column in a local newspaper invited many of us to his blog. In fact he was the first Tanzanian to blog in Kiswahili . That was in 2004. I had the privilege of meeting him in Nairobi, Kenya in 2012 and in Cebu, The Philippines in 2015. We were both attending Global Voices Citizen Media Summits. For me, blogging was fun. I never thought that blogs could actually threaten politicians. That was until 2010 when I had an opportunity to attend the Global Voices Citizen Media Summit   in Santiago de Chile. I was shocked to hear friends talking about restriction of freedom of speec

Uamuzi wa Kuachana na Blogu

Picha
Mkutano wa Global Voices, mtandao wa wanablogu, uliofanyika Cebu, Ufilipino, 2015 PICHA: Global Voices Nilianza kublogu katikati ya mwaka 2005. Wakati huo ilikuwa nadra kusikia mtu anaongelea blogu.  Ndesanjo Macha ndiye hasa aliyenifanya nikavutiwa kuanza kublogu. Wakati huo alikuwa mwandishi wa safu ya Gumzo la Wiki iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi kila Jumapili. Historia ya blogu hapa nchini haikamiliki bila kumtaja Ndesanjo Macha. Kimsingi, Ndesanjo ndiye mwanablogu wa kwanza kublogu kwa Kiswahili. Huo ulikuwa mwaka 2004. Nilipata bahati ya kukutana naye mara mbili kwenye mikutano ya waandishi wa kiraia kupitia mtandao wa wanablogu uitwao Global Voices. Mara ya kwanza ilikuwa jijini Nairobi, 2012 . Mara ya pili ikatokea jijini Cebu,Ufilipino, 2015 . Nakumbuka mwaka 2010 nikiwa nahudhuria mkutano wa wanablogu uliofanyika  Santiago de Chile , nilistushwa na masimulizi ya baadhi ya washiriki waliokuwa wakiongelea 'kuminywa kwa uhuru wa kujieleza kwenye nchi

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Picha
Katika utafiti uliofanywa na program ya Uwezo iliyochini ya Shirika la Twaweza, zaidi ya nusu ya watoto wa darasa la nne na tano katika nchi za Afrika Mashariki hawana uwezo wa kusoma na kuandika. Nilimwuuliza Bahiya Abdi, mhadhiri wa masuala ya mitalaa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, maana ya kutokujua kusoma na kuandika. Anasema: “Kuna mambo kadhaa ya kuangalia tunapozungumzia uwezo wa mtoto kusoma. Mbali na mtoto kutambua herufi, lazima awe na uwezo wa kusoma kwa haraka.” “Lakini pia, uwezo wa kusoma unapimwa kwa kiwango cha kuelewa kile anakisoma. Kama mtoto anaweza kusoma tu lakini hawezi kupata ujumbe vizuri, hapo tunaweza kusema uwezo wake uko chini ya kiwango.” Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mtoto wa darasa la kwanza na la pili anatarajiwa kutambua na kusoma kwa ufasaha maneno 50 yenye maana kwa dakika na maneno 40 yasiyo na maana kwa dakika. Kadhalika, anatarajiwa kuandika kwa ufasaha herufi kubwa na ndogo, na kufanya hesabu za kujumlisha na k

Unaweza Kumruhusu Mtoto Afuate Dini Apendayo?

Picha
PICHA: Pixabay Ipo nafasi muhimu ya imani/dini katika malezi ya watoto. Imani si tu inamsaidia mtoto kujitambua, lakini pia ina nafasi ya kumtengenezea mtoto sauti kutoka ndani yake inayomsaidia kupambanua lililo jema na baya. Sauti hii inaitwa dhamira. Utakuwa shahidi kuwa kuna mambo wakati mwingine unatamani kuyafanya lakini unajisikia hatia kuyafanya. Unaweza, kwa mfano, kuwa na uhuru wa kutaka kufanya chochote, lakini kuna sauti ndani yako ikakunyima ujasiri wa kukifanya. Hakuna anayekuona, hakuna anayekuhukumu, lakini kuna kengele ndani yako inakwambia kuwa unachotaka kukifanya sio sahihi. Mwanasaikolojia wa kale anayeitwa Sigmund Freud aliita kengele hiyo ‘Superego’ kumaanisha mkusanyiko wa maelekezo tunayoyapata kwa watu wanaotuzunguka. Kwa kawaida, sauti na maelekezo hayo inayoumbika ndani yetu ndiyo inayoamua namna gani tunadhibiti matamanio yetu ya asili kama hasira na tamaa za mwili. Imani, tafiti zinasema, ina kazi kubwa ya kujenga dhamira. Mtu mwenye

Kwa Nini Unatamani Kubadili Tabia Lakini Huwezi?

Picha
PICHA:  Coherentnews.com HEMEDI anavuta zaidi ya ‘pakiti’ moja ya sigara kwa siku. Ingawa, mara kadhaa, amejaribu kuacha tabia hii asiyoipenda, bado hajafanikiwa. Nia ya kuacha sigara anayo lakini kuacha ameshindwa. Unaweza kufikiri Hemedi yuko tofauti na sisi wengine. Lakini ukweli ni kwamba nasi, kwa namna tofauti, tunakabiliwa na mitihani mikubwa ya kitabia, pengine kuliko huo alionao Hemedi.   Kuna mambo fulani kwenye maisha yetu tunatamani kuyaacha lakini hatuwezi. Inawezekana ni matumizi mabaya ya fedha; kuongea kupita kiasi; hasira ya kulipuka; kusengenya na tabia nyingine tusizosipenda. Kwa upande mwingine, tunaweza kutamani kujenga tabia mpya lakini tunashindwa. Nawafahamu watu wengi ambao kila mwaka mpya unapoanza wanajipanga kufikia malengo makubwa. Wanautazama mwaka mpya kwa mtazamo tofauti na wanatamani kuwa watu tofauti na walivyokuwa kwa mwaka uliomalizika. Wengine wanajiapiza kuanza kusoma vitabu; wengine kufanya mazoezi ya mwili; wengine kuanza ku

Je, Kazi yako Inakuza au Inadumaza Wito Wako?

Picha
Inawezekana unafanya kazi ambayo hukuwahi kufikiri kama siku moja ungeifanya. Labda unadhani hukuchagua vizuri kipi cha kufanya, au pengine mazingira yalikulazimisha kushika kilichokuwa kinapatikana. Kwa upande mwingine, inawezekana pamoja na kuipenda kazi yako, unahisi kuna namna fulani ya udumavu. Hupati fursa za kupanda ngazi kiutendaji na umeanza kujihisi unapoteza wito wako. Vyovyote iwavyo, bado kuna tumaini. Unaweza kabisa kufanya kazi unayojua fika haiendani na wewe, lakini hatua kwa hatua, ikakutengenezea jukwaa zuri la kuumba vizuri wito wako. Hapa ninakuletea uzoefu utakaokusaidia kujitathmini na pengine kuchukua hatua muhimu katika kuchochea ule uwezo wa pekee ambao Mungu ameuhifadhi ndani yako. Unafanya kazi yenye staha? Mratibu wa Ukuuzaji wa Ujuzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Dar es Salaam, Bw. Albert William Okal anaeleza namna gani mazingira yako ya kazi yanavyoweza kukuza wito wako: “Hakuna kitu kama uchaguzi mbaya wa kazi. Kila kaz

Mbinu Nne za Kugundua na Kukuza Kazi ya Wito Wako

Picha
Umewahi kujisikia unafanya kazi isiyokupa utoshelevu? Unaweza kuwa na kiwango kikubwa cha elimu, kazi nzuri yenye heshima na mshahara mkubwa lakini unajikuta hufurahii kile unachokifanya. Ingawa moja ya sababu inaweza kuwa uongozi na mazingira mabaya ya kazi, hata hivyo, mara nyingi, tatizo huanzia ndani yetu  –k ufanya kazi isiyoakisi wito wetu. Mifumo ya elimu hulenga kutuandaa kukidhi mahitaji ya nje matarajio ya jamii, soko la ajira na mengine yanayofanana na hayo –matokeo yake mifumo hiyo inatuchonga kuwa watu tusiokidhi miito tuliyozaliwa nazo. Robert Green, mwandishi wa vitabu maarufu vya “Mastery” na “The 48  Laws of Power” anasema elimu ina nafasi kubwa ya kutupoteza. Kadri tunavyoelimishwa na watu waliotuzunguka ndivyo tunavyojikuta “tumekuwa wageni wa nafsi zetu wenyewe.” Maoni ya wazazi, walimu, marafiki, matarajio ya jamii, mara nyingi, yanatupeleka mbali na wito.  Kwa hiyo, badala ya kuheshimu kile ninachokiita wito, tumefungwa kwenye matara