Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

Ayafanyayo Mzazi Huamua Atakavyokuwa Mtoto

Picha
PICHA: Pinterest 'Mwanangu ni mtundu haijapata kutokea’ alilalamika msomaji mmoja wa safu hii. Sikuelewa ana maana gani aliposema mwanae ni mtundu. Nikaomba ufafanuzi. ‘Hasikii. Jeuri asikwambie mtu. Usipomfanyia purukushani huwezi kumwambia kitu akasikia.’ Kwa mujibu wa maelezo yake, kuna nyakati hubidi amtishe, amwadhibu vikali na hata kumtukana ikibidi.

Fahamu Namna Ajira Inavyoweza Kukoma kwa Mujibu wa Sheria

Picha
Ufanisi wa ajira unategemea uhusiano mzuri uliopo kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mwajiri, kwa kawaida, huweka mazingira mazuri kumwezesha mwajiriwa kutekeleza kazi zake. Mwajiriwa naye, kwa upande wake, hutumia ujuzi na uzoefu alionao kufanya majukumu aliyokabidhiwa na mwajiri.

Wajibu wa Mzazi kwa Mtoto Kisheria -2

Picha
SHERIA ya Mtoto Na. 21 ya 2009 inamtambua mtoto kama mtu yeyote mwenye miaka pungufu ya 18. Sheria hii ilitungwa kukidhi matakwa ya makubaliano na mikataba ya kimataifa inayolenga kulinda haki, maslahi na ustawi wa mtoto.

Unavyoweza Kumfundisha Mtoto Kuwa Mkweli

Picha
PICHA: Heaths Haven Fikiria uko jikoni ukiandaa chakula cha jioni. Watoto wako wawili wadogo Fred na Joe wanacheza sebuleni. Salome yuko mezani akifanya kazi za shule. Mara unasikia mlio wa kitu kuvunjika sebuleni. Unapatwa na wasiwasi. Unakwenda haraka kujua kilichotokea. Maji yanatiririka sakafuni. Chupa ya chai imedondoka na kupasuka. Unakasirika.

Namna ya Kuutambua Wito wa Maisha Yako

Picha
PICHA: B aha'i Blog Umewahi kufanya kazi zenye heshima lakini hujisikii ridhiko ndani yako? Unapata kipato kizuri na watu wengine wanatamani kufanya unachokifanya lakini wewe mwenyewe hufurahii.  Unakuta umesoma vizuri lakini huoni thamani ya kile ulichokisoma. Zaidi ya kutaja chuo ulichosoma na ngazi ya elimu uliyofikia huoni namna gani elimu yako inakusaidia kutoa mchango kwa jamii.

Unahitaji Nidhamu ya Fedha Kujikwamua Kiuchumi

Picha
PICHA: usaa.com Juma lililopita tuliongelea uwezekano wa mfanyakazi kujikwamua kiuchumi . Kubwa ni nidhamu. Unapokuwa na nidhamu ya mshahara, unaongeza uwezekano wa kuwa na usalama wa kifedha. Swali linaweza kuwa, ‘Kinachomfanya mfanyakazi akose nidhamu ya fedha ni nini?’ ‘Inakuwaje mchuuzi mdogo wa bidhaa awe na nidhamu ya fedha kuliko Afisa wa Serikali?’

Wajibu wa Mzazi kwa Mtoto Kisheria

Picha
Tumeshuhudia matukio mengi katika jamii yetu ya watoto kunyanyaswa na kudhalilishwa na watu wazima wakiwemo walezi na hata baadhi ya wazazi wasio waadilifu. Imekuwa kawaida kusikia watoto yatima wakitendewa vitendo vya uonevu baada ya wazazi wao kufariki. Ndugu na jamaa, bila haya, wamekuwa wakifanya maamuzi yanayowahusu watoto bila kuzingatia maslahi na haki za watoto.

Jifunze Namna Bora ya Kumrudi Mtoto

Picha
PICHA: IT News Africa Tunapojadili mbadala wa adhabu ya bakora tunatambua changamoto kadhaa. Kwanza, ni wazi bakora zimekuwa sehemu ya malezi yetu. Kwa wazazi wengi, unapozungumzia nidhamu ya mtoto, maana yake unazungumzia bakora. Imejengeka imani kwa watu kuwa bakora ndiyo nyenzo kuu inayoweza kumrekebisha mtoto.

Wajibu wa Wamiliki wa Shule za Msingi za Bweni

Picha
PICHA: B ORGEN Magazine TUMESHAURIANA mambo kadhaa ya kuzingatia tunapolazimika kuwapeleka watoto wadogo kwenye shule za msingi za bweni. Kubwa zaidi ni mzazi kujiridhisha na namna shule inavyomwekea mtoto mazingira mazuri yanayofanana na yale ya nyumbani.

Unavyoweza Kutumia Mshahara Kujikwamua Kiuchumi

Picha
Wapo watu wanawakejeli wafanyakazi kwa kuajiriwa. Kwamba kama mtu asiye na elimu anaweza ‘kuosha magari mtaani’ na akakuzidi kipato kuna sababu gani kuishi maisha magumu ofisini? Upo ukweli wa namna fulani. Wafanyakazi wengi wanaishi maisha ya ukata. Kazi yao kubwa ni kupambana kuhakikisha kuwa mishahara inakutana. Katika mazingira ya namna hii, inakuwa vigumu kupiga hatua za maana kimaisha.

Nidhamu ya Mtoto Bila Viboko Inawezekana

Picha
PICHA: Pinterest Adhabu ya bakora ni utamaduni. Kwa wengi wetu bakora ni imani. Tunaziamini kiasi cha kuwa tayari kuzirithisha kwa wanetu kama ambavyo na sisi tumeziridhi kwa wazazi wetu. Kwa hiyo tunapopendekeza mbadala wa bakora kama adhabu iliyozoeleka tunaelewa hili haliwezi kuwa jambo jepesi. Kama tulivyoona, wazazi tunapowachapa watoto tunaamini lengo ni kuwasaidia wawe na nidhamu. Hata hivyo, kwa kutazama mazingira yanayoambatana na adhabu hii ni dhahiri bakora haiondoi tatizo linalokusudiwa.