Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2017

Unavyoweza Kukuza Tabia Njema kwa Mwanao -4

Picha
Katika makala yaliyopita tumejifunza aina mbili za misukumo ya utovu wa nidhamu. Kwanza, tumeona mtoto huweza hufanya ukorofi kutafuta kusikilizwa. Anaposumbua na hata kudeka bila sababu, mara nyingi, anajaribu kutuambia kuwa hatujampa muda wa kuwa karibu naye. Anafanya hivyo kutafuta usikivu wetu. Pia, tumeona wakati mwingine mtoto husukumwa na hisia za kutaka kulipiza kisasi. Kama ilivyo kwa mtu mzima, mtoto naye anazo hisia. Anaweza kuumizwa na kauli na matendo anayoyatafsiri vibaya. Jitihada za kupunguza maumivu yake huishia kuwaumiza na wengine. Namna gani tunawasaidia watoto kuondoa tafsiri hizi potofu, huamua aina ya tabia watakazojifunza. Katika makala haya tunaangazia malengo mengine mawili yanayotengeneza msukumo wa kukosa nidhamu.

Unavyoweza Kukuza Tabia Njema kwa Mwanao -3

Picha
TUMEKWISHA kuona kuwa mtoto hakosi adabu kwa bahati mbaya. Kila anachokifanya kina malengo yaliyojificha. Malengo haya, kama tulivyoona, mara nyingi hayako sahihi. Ni mbinu tu za kutafuta ukaribu na mzazi ambazo kimsingi zimejengwa kwenye tafsiri isiyosahihi. Makala haya yanaangazia malengo mawili kati ya manne yanayowafanya watoto waonyeshe utovu wa nidhamu. Kadhalika, tunaangalia namna tunavyoweza kuuelewa ujumbe uliofichwa kwenye malengo hayo.

Unavyoweza Kukuza Tabia Njema kwa Mwanao -2

Picha
Mama Neema anarudi nyumbani jioni. Neema anaposikia mlio wa gari ya mama yake, anatoka nje kwa furaha. Mara moja anamrukia mama  kumpokea kwa bashasha. Mama amechoka. Amekuwa na siku ndefu kazini. Haonekani kuwa mchangamfu. Neema anauliza maswali mengi kwa mama yake. Hajibiwi. Hata pale anapojibiwa, mama haonekani kuwa na uzingativu. Ili apate nafasi ya kumpumzika, mama anamwelekeza Neema kwenda kufanya kazi za shule alizokuja nazo nyumbani. Neema anavunjika moyo lakini analazimika kuondoka.

Namna Shule za Msingi za Bweni Zinavyoathiri Tabia za Watoto -3

Picha
KATIKA makala yaliyopita, tumeona kuwa shule za msingi za bweni zinachangia kuwanyima watoto fursa ya kujifunza ujuzi wa kujitegemea. Uwezo hafifu wa kujifunza stadi za maisha, kwa kiasi kikubwa, unachangiwa na matarajio makubwa ya kitaaluma waliyonayo wazazi kwa watoto wao. Wamiliki na waendeshaji wa shule za bweni, kimsingi, wanaitikia wito wa wazazi wanaotarajia watoto wao kujifunza maarifa ya shule zaidi hata ikibidi kwa gharama ya kudumaza maeneo mengine muhimu ya kimakuzi.

Unavyoweza Kukuza Tabia Njema kwa Mwanao -1

Picha
Fikiria mwanao ana umri wa miaka kumi na minane na anaondoka nyumbani kwenda kujitegemea. Je, ungependa awe mtu mwenye tabia zipi? Ungependa mwanao anapoondoka nyumbani kwako kwenda kuanza maisha mapya awe mtu wa namna gani? Sifa zipi, ujuzi upi, haiba ipi ungependa imtambulishe akiwa mtu mzima?

Tunayopaswa Kuyafahamu Kuhusu Shule za Msingi za Bweni -2

Picha
Tulianza kujadili namna gani mazingira ya shule za bweni yanavyochangia kuwasaidia watoto wadogo kuimarika kiakili. Bonyeza hapa kama hukusoma makala hiyo. Tuliona shule za bweni zinaweka mazingira sisimushi yanayowajenga watoto kiufahamu zaidi kuliko wenzao wanaoishi nyumbani. Mambo kadhaa yanaonekana kuchangia kukuza uwezo huu. Kwanza, tulitaja uwepo wa ratiba inayoongoza mtiririko wa shughuli za watoto wanapokuwa katika mazingira ya shule.

Tunayopaswa Kuyafahamu Kuhusu Shule za Msingi za Bweni

Picha
Katika miaka ya hivi karibuni, shule za msingi za bweni zimekuwa maarufu. Kimsingi, si tu shule za msingi, lakini hata shule za awali za bweni. Hivi sasa, miji karibu yote katika nchi hii inazo shule kadhaa zinazopokea watoto wadogo na kuwasomesha kwa mfumo wa bweni. Takwimu rasmi za hivi karibuni hazipatikani. Lakini kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, mwaka 2012 nchi yetu ilikuwa na shule za msingi zipatazo 684 zenye huduma ya bweni. Shule hizi zinafahamika pia kama shule zinazotumia Kiingereza kama lugha rasmi ya kufundishia, yaani English Medium, zikimilikiwa na watu binafsi au taasisi zisizo za umma.

Kusamehe Wazazi Wako Kunavyoweza Kubadilisha Maisha Yako

Picha
Kuna tabia fulani tunaweza kuwa nazo ambazo, kwa hakika, tunajua zinatufananisha na wazazi wetu. Tunafanya vitu fulani, wakati mwingine bila hata kujua, lakini vinafanana na yale tuliyowahi kuwaona wazazi wetu wakiyafanya. Ipo mifano mingi kuelezea jambo hili. Baba, kwa mfano, unaweza kuwa na tabia ya hasira kali. Mwanao akifanya kosa dogo unakuwa mwepesi wa kukemea. Wakati mwingine, unatoa adhabu kubwa mno zisizolingana na makosa halisi ya mtoto. Ukichunguza vizuri unakuta kumbe ndivyo alivyo na baba yako.