Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2014

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Katika makala yaliyopita , tuliangalia matukio muhimu ya kimakuzi katika maeneo mawili makubwa ya ukuaji wa mtoto nayo ni 1) kimwili na 2) kiakili. Katika sehemu hii ya pili, tunasaili ukuaji wa kimahusiano na kihisia ili kutazama yabia zinazojitokeza pasipo kuathiriwa na malezi na haiba ya wazazi. Kwa lugha nyingine, haya ni matarajio ya mtoto yanayoendana na umri wake bila kuingiliwa na matarajio na yanayofanywa na mzazi kwake.

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Picha
Katika makala haya, tunatazama kwa ufupi makuzi ya mtoto mwenye umri wa siku moja mpaka miezi 36. Tutaangalia mambo ya msingi yanayonesha ukuaji wa mtoto unavyoendelea katika maeneo makubwa manne; 1) ukuaji wa kimwili 2)  kiakili 3)  kimahusino na watu wengine na mwisho 4) kihisia. Kwa kawaida maeneo haya manne yanategemeana ili kumwezesha mtoto kukua kwa ujumla. Kwa mfano ili mtoto akue kimwili, anahitaji ukuaji wa akili ipasavyo ambayo nayo itaathiri namna anavyomudu hisia zake na hivyo kuhusiana na watu wengine. Kwa hiyo ni sawa tukisema hakuna ukuaji wa eneo moja usiotegemea eneo jingine.

Uhusiano wa haiba ya mzazi na malezi ya watoto – 2

Picha
Wakati tunajiandaa kuangalia kwa kina malezi ya watoto wenye umri wa miaka 0 – 3 kama tulivyoahidi , na kuona namna watoto hawa wanavyoweza kuathiriwa na malezi wanayoyapata, ni vizuri tutazame japo kwa ufupi haiba kuu nne za wazazi zinazoweza kuathiri sana malezi ya watoto.

Miaka miwili ya Kuwa 'Mama' Ina Mafunzo Makubwa Kwangu...

Picha
Nilipoamua kuchukua uamuzi wa kubadilishana majukumu na mke wangu sikujua ni kwa jinsi gani uamuzi huo ungenibadilisha mimi na kunipa mtazamo mpya kabisa katika maisha. Baada ya kuzaliwa Baraka siku kama ya leo mwaka 2012 tuliamua kubadilishana majukumu ya familia; mimi nibaki na kuangalia watoto na kutunza nyumba na mahitaji yake yote na mke wangu aendelee kufanya kazi na kusaidia wakati wowote anaoweza.

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???

Picha
Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Ningependa tuanze kwa kujiuliza, 'Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu?' ...kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Uhusiano wa haiba ya mzazi na malezi ya watoto – 1

Picha
Katika mfululizo huu tunatarajia kujadili mahitaji ya kimahusiano ya mtoto mwenye umri usiozidi miaka 20 kwa vipengele kadhaa. Katika kufanya hivyo, tunajikita kwenye uhusiano wa moja kwa moja ulipo kati ya haiba ya wazazi na namna haiba hiyo inavyoweza kuathiri vile tunavyolea watoto wetu. Tutaona namna malezi hayo yanavyoathiri tabia na mwenendo wa watoto tangu wanavyozaliwa mpaka wanapofikia umri wa kujitegemea. Tutaonesha kwamba kwa kiasi kikubwa tabia tunazoziona kwetu si za kuzaliwa na wala hazitokei kwa bahati mbaya. Ni matokeo ya haiba na mahusiano yenu na wazazi waliotulea.