Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2014

Rais mteule atumia mitandao ya kijamii kuwaomba raia kumchagulia Baraza la Mawaziri

KATIKA kuthibitisha kwamba kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni kubwa, hivi majuzi, Rais mpya wa Indonesia Mhe Joko Widodo (maarufu kama Jokowi) amewaomba watumiaji wa mtandao wa Facebook kumsaidia kuteua baraza lake la mawaziri kwa kupendekeza majina ya watu wanaoweza kushika wadhifa wa kuwa Mawaziri. Hatua hiyo, ni mwendelezo wa kile anachokiita mwenyewe 'kuongeza  kwa ari ya kujitolea' miongoni mwa raia wa nchi hiyo, baada ya watu wengi kujitolea kumsaidia katika harakati zake za kuingia ikulu. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jokowo ametoa orodha ya nafasi 34 za Uwaziri , zenye majina matatu yanayopendekezwa kwa kila nafasi, huku kukiwa na nafasi ya nne wazi kwa wananchi kupendekeza wanayemtaka. Widodo anataapishwa ifikapo Oktoba 20, 2014 kuwa Rais. Joko Widodo (53) Gavana wa zamani wa Jakarta, amechaguliwa kuwa Rais wa Indonesia baada ya kumbwaga mpinzani wake Prabowo Subianto kwa asilimia 53 ya kura milioni 130 zilizopigwa tarahe 9 Julai, 2014. Kama ilivyo

Watoto waliolelewa kidini, wamegundulika kushindwa kutofautisha uhalisia na mambo ya kufikirika

Picha
MIAKA miwili iliyopita, 2012, Justin L. Barret alionyesha kwamba binadamu wote huzaliwa na hitaji la asili la imani na kutambua nguvu zisizoonekana na kwamba imani haitokani na jamii kama wanavyodai watu wasio amini uwepo wa Mungu. Kwa Barret, imani za kidini ni sehemu ya 'maumbile' ya asili anayozaliwa nayo mtu. Hoja zake kuu katika kitabu chake ni mbili 1) kwamba watoto wana uwezo wa asili wa kuamini nguvu za kimungu zisizoonekana kwa sababu ya, pamoja na mambo mengine, huamini uwepo wa miungu iwezayo yasiyowezekana kibindamu kabla hata ya kufikia hatua ya kujua kuwa watu wazima wanajua zaidi ya watoto 2) kwamba watoto sio madodoki ya kunyonya utamaduni unaowafanya kuwa waumini wa dini kwa sababu imani, hata hivyo, hutofautiana kati ya mtu na mtu, mahali na mahali na kadhalika. Soma pitio la kitabu Barret kiitwacho Born Believers: the science of children's religious belief. Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni unapingana na hayo aliyoyasema Barret miaka ipatayo miwil

Shukrani za pekee kwa Prof. Mbele kwa zawadi ya thamani!

Picha
'Africans and Americans Embracing Cultural Difference', ni kitabu kizuri nilichokisoma kwa mara ya kwanza Aprili, 2009 nilipokiona katika duka la vitabu KIMAHAMA, Arusha. Ilikuwa ni baada ya kukisikia kikisemwa na rafiki yangu mmoja. Ni miaka mitano imepita, lakini kitabu hiki hakikuwahi kuizoea maktaba yangu tangu wakati huo. Kusoma kitabu chenye saini ya mwandishi, si jambo linalowatokea wengi. Ni muujiza ulionitokea. Picha: Jielewe Kwanza, kwa rafiki zangu wasomaji waliofika kwangu kwa mazungumzo ya vitabu na waandishi, kitabu hiki hakikukosekana kwenye mazungumzo hayo. Na kila aliyesikia sifa zake, alipenda kuthibitisha ikiwa nilisema  kweli kwa kukiazima. Kiliazimwa na wasomi, wasafiri, waongozaji wa watalii (tour guide), wapenda maarifa, kutaja kwa uchache. Ni bahati mbaya sana kwamba hakikuwa kinapatikana katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kiliazimwa, na kuazimwa, tena na tena kwa muda wa miaka miwili. Mwaka 2011, kiliondoka rasmi kwenye maktaba yangu. Nilikuja k

Kanuni muhimu za kuwa baba anayejua wajibu wake

Da'Subi wa blogu maarufu ya habari wavuti.com ameweka makala yenye kanuni muhimu kwa wale wanaotaka kuwa akina baba bora. Makala hiyo iliandikwa awali kwa Kiingereza na Leo Babauta ambaye amekuwa baba kwa miaka 21 na ana watoto sita. Leo anayataja mambo matano muhimu ikiwa unataka kuwa baba anayejua wajibu wake kwa watoto wake. Hapa tumeyaeleza kwa ufupi kwa lugha ya Kiswahili: Upendo. Huu ndio wajibu mkuu kuliko wajibu wowote unaoweza kuwa nao kama baba. Anasema kuwapa chakula, malazi, mavazi ili wakue, si kazi ngumu. Kazi ni kumfanya mtoto ajisikie kupendwa, hali ambayo ndiyo itakayofinyanga tabia yake ukubwani. Kipimo cha mafanikio ni ikiwa unaweza kumfanya mwanao ajisikie kupendwa, Kuwa mfano. Maisha unayoishi yana maana kubwa kwa wanao kuliko maneno unayowaambia. Unachofanya ndicho kinachochukuliwa serious. Ukizoea kuwaadhibu, ndicho wanachojifunza. Ukiwabana sana, hawajifunzi kutushirikisha walivyonavyo. Kama unataka wanao wale chakula bora, anza wewe. Ukitaka wasome

Ni kweli Israel haikosei kwa Mkristo kama ilivyo Hamas kwa Mwislam?

Picha
JUZI nikiwa katika pita pita zangu katika mitaa ya mjini, nimebahatika kukutana na bango kubwa sana barabarani. Bango lenyewe lilikuwa na ujumbe wa kuhamasisha maandamano ya siku ya Quds kupinga 'Masaibu ya Wapalestina' yatakayofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 25 Julai, 2014. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa umma, maandamano hayo yataanza saa 3 asubuhi, kuanzia kituo cha Boma, Barabara ya Kawawa, jijini Dar es Salaam. Bango hilo lina picha ya msikiti. Tutakumbuka kwamba Israel imekuwa ikiwashambulia vikali Wapalestina kwa siku za hivi karibuni, hali ambayo kwa kweli inasikitisha. Mamia ya Wapalestina wamepoteza maisha yao wakiwemo watoto. Ni hali ambayo inatia simanzi. Maandamano kadhaa tayari yameshafanyika kuishutumu Israel kwa mashambulio hayo. Israel kwa upande wao, wanadai wanachokifanya ni kulipiza kisasi kwa uchokozi wa Hamas. Siandiki kutafuta kujua nani anafanya vizuri na yupi anakosea katika mgogoro huo wa enzi na enzi. Hayo si ya leo. Bango lililoko maeneo ya

Namna ya kuifanya huduma ya 'day care' imfae mwanao

Picha
TULIJADILI kwa kifupi sana hitaji la huduma ya malezi yasiyo ya mama (non-maternal child care). Anzia hapa kama hukuisoma . Tulisema, sababu kubwa ni kwamba akina mama wa kileo wanatafuta kipato nje ya nyumba, hali inayosababisha changamoto ya kimalezi. Tuliona pia kwamba katika jamii yetu, huduma isiyorasmi ya malezi ndiyo inayotumika zaidi. Changamoto yake kubwa kuliko zote ni ukweli kuwa akina dada hawa wengi hawana uelewa wa kutosha wa malezi. Ni kweli kuwa hata akina mama wengi hawana uelewa huo unaoitwa wa kutosha. Lakini angalau, tunafahamu kuwa mama anaweza kujibiisha kuhangaika na mahitaji ya mtoto kuliko house girl, ambaye wakati mwingine hata hatumjui vizuri, yeye mwenyewe, wala familia yake, wala undani wa tabia yake. Shauri ya changamoto hizo, pamoja na nyinginezo, familia zenye uwezo kidogo zinachagua kutumia huduma za malezi rasmi ya watoto. Day care. Mtoto mara nyingine wa miezi kadhaa hadi wa umri wa kuanza shule, hupelekwa kwenye vituo vinavyotambulika ili alelewe k

Changamoto ya kumpa 'mtumwa wa ndani' jukumu la malezi ya watoto

Picha
SIKU ZA NYUMA, familia zilikuwa tofauti na ilivyo leo. Akina mama walikaa nyumbani kulea watoto. Waliitwa mama wa nyumbani. Kazi yao kuu ilikuwa ni kuitunza nyumba kwa maana ya familia. Ni baba ndiye aliyekuwa na wajibu wa kutafuta mkate wa familia iwe kwa ajira, kujiajiri au namna nyingine.  Ilikuwa hivyo kwa sababu watoto wa kike walionekana si sawa na wenzao wa kiume. Hawakuwa na haki ya kusoma, na hivyo kujikuta katika mazingira ambayo hawakuwa na uchagazi mwingine zaidi ya 'ajira' ya kutumika nyumbani. Ndivyo ilivyokuwa katika jamii nyingi hasa barani Afrika. Leo hii mambo yamebadilika. Wanawake wanahitaji, na kwa kweli wanastahili haki na fursa ya kama ilivyo kwa wanaume. Hii leo, watoto wa kike wanasoma sana. Sawa na, hata zaidi ya, watoto wa kiume. Na matunda ya fursa sawa kwa wote kielimu, yamekuwa ni fursa sawa kiajira pia. Haki zimekuwa sawa. Sasa hivi hata waajiri wametambua kuwa akina mama wanaweza. Akina mama ni waaminifu. Wanashika madaraka makubwa makazini, na

Kujikataa, kuikataa hali yako kwaweza kuwa kichocheo cha muhimu kujielewa

Picha
HUENDA umekutana na watu wanaoshauri ujikubali. Na huenda na wewe ni mmoja wao. Unajikubali. Kwamba ili kufanikiwa, ni busara ujipokee vile ulivyo na vyote ulivyonavyo kwa shukrani. Msingi mkuu, inasemwa, bila kujikubali na kujipokea huwezi kuwa na amani. Na amani na furaha, huenda, kama sio ndivyo ilivyo, likawa ndilo kusudi kuu la maisha ya mwanadamu. Purukushani zote tunazoziona, kukusanya mali, elimu, kuwa na familia bora, madaraka makubwa, umaarufu na kadhalika mwisho wa siku ni kutafuta furaha. Utoshelevu. Ridhiko la moyo. Watu wasiojikubali, tunaambiwa hawana amani na maisha yao. Wanavyojiona sivyo vile wanavyotaka wao. Matokeo yake, ndio hao wanajichubua wafanane na sura wanavyoitaka wao. Sote tumesikia maisha ya yule mwanamuziki maarufu mweusi aliyejigeuza afanane na wazungu. Matokeo mabaya ya kutokujikubali. Wengine tunasikia wakidanganya wasifu na elimu zao. Ulaghai. Lakini ukweli ni kwamba wanaona wasifu walio nao haufanani na vile wanavyotaka wao kuwa. Inabidi kudangan

Unaweza kuwa mzazi bora zaidi kwa kujifunza kwa wazazi wako

NI UKWELI kwamba katika suala la malezi, hakuna kitu unachoweza kukiita 'the obvious'. Hakuna uzoefu. Na tunahitaji kujifunza kwa wengine. Ndivyo anavyofanya mzazi mmoja nchini Panama, Joel Silva Díaz , anayeandika uzoefu wake wa kimalezi katika blogu yake . Lengo lake ni kushirikisha wasomaje wake kile anachodhani kinaweza kuwasaida watu wenye kiu ya kujifunza. Anasema,  Sikumbuki kuwa na mazungumzo ya zaidi ya mistari mitano na baba yangu. Ni miaka kumi na zaidi imepita. Kwa matukio ya hapa na pale kati yangu na baba yangu, naweza kusema tu ni kwamba angalau nilikuwa na baba. [...] Na hicho ndicho ninachotaka kukifanya vizuri zaidi, nataka kuwa baba anayefanya bila hata kutambua, nataka kuwakumbatia, kuwabusu, kuwapa fursa bora za kufanya maamuzi bora na kuwasaidia wanapokuwa hawajafanya chema, sichelewi kuwonyesha upendo na kuwajali, hata kama kuna nyakati naweza kweli kuwafinya. [...] Kama mzazi, nisingependa  niwe mtu wa kuwachungulia wanangu kila baada ya maj

Je, ni kweli lugha huathiri namna tunavyofikiri?

Picha
MJADALA wa nafasi ya lugha katika namna tunavyofikiri na kuyaelewa mazingira yetu una historia ndefu. Kwa ujumla kumekuwepo na pande mbili kuu. Upande wa kwanza unashikilia kuwa lugha, ama mawasiliano ayafanyayo mtu na wengine, iwe kwa maneno, ishara, alama au vitendo haina uhusiano wowote na namna mtu anavyofikiri. Ushahidi wa madai haya ni namna watoto wadogo wanavyoweza kufikiri uzuri bila hata kujua lugha. Na ni kweli pia kwamba kwa mtoto fikra au uelewa hutangulia uwezo wa lugha. Kwamba hawezi kusema wala kuonyesha kusikia kinachosemwa, hiyo haimaanishi kuwa mtoto hafikiri. Na ndio maana wakati anajifunza lugha, mtoto huweza kutumia neno moja kumaanisha mambo mengi. Anaelewa kuliko anavyotumia lugha. Vile vile, inasemekana, watu wenye ulemavu wa kutumia maneno kuwasiliana na wenzao, bubu kama tunavyowaita, wana uwezo mzuri wa kufikiri kama watu wengine. Kwamba watu hawa hawana tatizo la kuyatambua na kuyaelewa mazingira yao kwa ufanisi ule ule tunaouona kwa watu wasio na ulemavu

Mahojiano na washiriki wa maonyesho ya Utamaduni wa Kenya Washington DC

Picha
Kati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali. Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia. Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha. KARIBU UUNGANE NASI Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya Na mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya Mtaalamu wa

Jinsi matarajio yetu yanavyoathiri mitazamo na tabia za wengine

Picha
ILIKUWA ni mwaka 1968 Rosenthal na Jacobson walipogundua namna matarajio ya walimu yanavyoweza kusabisha matokeo yasiyotarajiwa kwa wanafunzi wao. Watafiti hawa walikwenda kwenye shule moja na kupima uelewa wa wanafunzi kwa kutumia mtihani maalum maarufu kama IQ test . Walimu wa shule hiyo walishuhudia zoezi hilo. Basi, baada ya kuwapima wanafunzi, bila kujali matokeo ya kipimo cha uelewa, waliwagawa wanafunzi katika makundi mawili. Kundi la kwanza lilikuwa la wanafunzi waliopachikwa jina la 'wanafunzi wakali' hata kama haikuwa kweli. Walimu wao walipewa habari hiyo, kwamba wanafunzi hawa wamepimwa na wameonekana ni wazuri sana kiakili na wangeweza kufanya vizuri sana baada ya muda mfupi hata kama hawakuwa wakifanya vizuri kwa sasa. Lengo lilikuwa ni kutengeneza na kupandisha matarajio ya walimu kwa wanafunzi hawa. Kwenye kundi la pili la wanafunzi lililokuwa na wanafunzi wenye uwezo kama wenzao wa kundi la kwanza,  walimu hawakuambiwa lolote kuhusu uelewa wa wanafunzi hao. K