Rais mteule atumia mitandao ya kijamii kuwaomba raia kumchagulia Baraza la Mawaziri

KATIKA kuthibitisha kwamba kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni kubwa, hivi majuzi, Rais mpya wa Indonesia Mhe Joko Widodo (maarufu kama Jokowi) amewaomba watumiaji wa mtandao wa Facebook kumsaidia kuteua baraza lake la mawaziri kwa kupendekeza majina ya watu wanaoweza kushika wadhifa wa kuwa Mawaziri.

Hatua hiyo, ni mwendelezo wa kile anachokiita mwenyewe 'kuongeza  kwa ari ya kujitolea' miongoni mwa raia wa nchi hiyo, baada ya watu wengi kujitolea kumsaidia katika harakati zake za kuingia ikulu.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jokowo ametoa orodha ya nafasi 34 za Uwaziri, zenye majina matatu yanayopendekezwa kwa kila nafasi, huku kukiwa na nafasi ya nne wazi kwa wananchi kupendekeza wanayemtaka. Widodo anataapishwa ifikapo Oktoba 20, 2014 kuwa Rais.

Joko Widodo (53) Gavana wa zamani wa Jakarta, amechaguliwa kuwa Rais wa Indonesia baada ya kumbwaga mpinzani wake Prabowo Subianto kwa asilimia 53 ya kura milioni 130 zilizopigwa tarahe 9 Julai, 2014. Kama ilivyo kawaida ya chaguzi nyingi, Subianto amegoma kukubali matokeo hayo.

Kwa habari zaidi za uchaguzi huo, bofya hapa.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu