Unaona nini kwenye picha hii?Ukitazama picha hii kwa makini, unaweza kubaini utata fulani wa kimaamuzi. Ukiitazama kwa haraka haraka, huwezi kuuona utata huo na hivyo huwezi kukubaliana na mtazamaji mwingine atakayedai kuuona utata usiouona wewe. Sasa itazame kwa makini kadiri unavyoweza halafu ujiridhishe kwamba unachokiona ndicho kinachopaswa kuonwa.

Heri ya mwezi mpya.

Maoni

 1. Da! Hii kali, very interesting!

  Picha hii inawakilisha sura mbili, kuna moja ya mwanadada aliyevaa kilemba fulani hivi kama kofia halafu nikiiangalia vizuri tena naona sura ya mwanaume mwenye mzuzu.

  Bwayaeee, hiyo ndio namna nilivyoiparceive hiyo picha.Tuangalie wengine wameiona kivipi.

  JibuFuta
 2. Kwani huyu Dada aeangalia upande gani? Ni kama vile kiwiliwili kimeangalia huku na yeye kaangalia kula kwake. Lakini pia ni kama vile kiwiliwili kimeangalia upande wa mbele na yeye ameangalia kushoto kwake. Sijui

  JibuFuta
 3. inawezekana umejiangalia kwenye kioo na pia si rahisi kujua kama ni dada au kaka kwani miaka ya zamani wote walikuwa na nywele ndefu,wote walikuwa wanavaa kofia pia hata mavazi mengine yalikuwa sawa. Hata mimi sijui

  JibuFuta
 4. Uso wa binti unaangalia upande nyuma, ukiangalia vizuri unamwona babu anaangalia chini. Shingo ya binti iwe kidevu, sikio liwe ndio jicho la mzee. Nywele za binti ziwe ndo makunyanzi ya mzee. Nimepatia?

  JibuFuta
 5. nimerudi tena sasa nadhani naona sura nzuri ya binti mdogo na pia sura ya bibi kizee.

  JibuFuta
 6. Yasinta umeniwahi, jibu lako na langu lilikuwa lilo hilo. Msichana anatizama huko na bi kizee anatizama chini.

  JibuFuta
 7. Kibaya zaidi ni kuwa hata kwa majibu ya "kugandamizia" ya kina Da Subi na Da Yasinta mie bado sioni.
  Dah!!!
  Kaazi kwelikweli

  JibuFuta
 8. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

  JibuFuta
 9. Picha hii inanikumbusha wakati fulani wakti tulipokuwa kwenye semina ya utambuzi.
  Mwezeshaji alitoa mada inayosema mwonekano wa kwanza (First Impression)
  kabla hajaanza kuzungumza alituwekea hii picha kisha akatuuliza kama tunaoana nini, basi wapo waloona picha ya bibi kizeee aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 90 ambaye alikuwa hana meno yaani kibogoyo na wengine wenye tuliona picha ya binti mrembo wa miaka kama 20 hivi. basi ulizuka ubishi mkubwa kati ya pande mbili hatimaye yule mwezeshaji aktugawa katika makundi mawili yaani wale waloona picha ya kigori na wale waloona picha ya bibi kizee. kisha akasema kila kundi litetee hoja yake.
  Kizungumkuti kilianzia hapo,
  pua ya bibi kizee ilionekana ni kidevu cha binti mrembo.
  Jicho la bibi kizee lilionekana ni sikio la binti mrembo, hatimaye tuliklubaliana kwamba ile picha ilibeba taswira ya watu wawili (Ubunifu) yaani ya bibi kizee na ya binti kigori.

  MMtoa mada alikuwa akitaka kutujuza kuwa mara nyingi sisis tunatoa maamuzi kwa kuangalia muonekano wa kwanza.
  He nisije nikafungua darasa la utambuzi humu, ngoja niishie hapa.
  Ahsante kaka Bwaya kwa somo hili zuri.

  JibuFuta
 10. Picha hii inanikumbusha wakati fulani wakti tulipokuwa kwenye semina ya utambuzi.
  Mwezeshaji alitoa mada inayosema mwonekano wa kwanza (First Impression)
  kabla hajaanza kuzungumza alituwekea hii picha kisha akatuuliza kama tunaoana nini, basi wapo waloona picha ya bibi kizeee aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 90 ambaye alikuwa hana meno yaani kibogoyo na wengine wenye tuliona picha ya binti mrembo wa miaka kama 20 hivi. basi ulizuka ubishi mkubwa kati ya pande mbili hatimaye yule mwezeshaji aktugawa katika makundi mawili yaani wale waloona picha ya kigori na wale waloona picha ya bibi kizee. kisha akasema kila kundi litetee hoja yake.
  Kizungumkuti kilianzia hapo,
  pua ya bibi kizee ilionekana ni kidevu cha binti mrembo.
  Jicho la bibi kizee lilionekana ni sikio la binti mrembo, hatimaye tuliklubaliana kwamba ile picha ilibeba taswira ya watu wawili (Ubunifu) yaani ya bibi kizee na ya binti kigori.

  MMtoa mada alikuwa akitaka kutujuza kuwa mara nyingi sisis tunatoa maamuzi kwa kuangalia muonekano wa kwanza.
  He nisije nikafungua darasa la utambuzi humu, ngoja niishie hapa.
  Ahsante kaka Bwaya kwa somo hili zuri.

  JibuFuta
 11. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

  JibuFuta
 12. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

  JibuFuta
 13. Kaazi kwelikweli.Ndiyo mambo ya kutazama hayo.

  JibuFuta
 14. Asanteni kwa majibu.

  Mkodo anasema ameona picha ha ha ahaaa!

  Hivi mna hakika kwamba hakuna sura nyingine zaidi ya hizo mbili zilizotajwa tayari?

  Kwa nini wasomaji wengine waliona tofauti na wengine? Funzo?

  JibuFuta
 15. Bwaya,
  Sura ya tatu ipo katika ile picha nyingine, itizame hapa http://www.freewebs.com/abu_princeton3/manwoman.gif
  Alafu picha nyingine za kuchangamsha akili na maelezo ya kutosha kuhusu dada na bibi ambao Mube alipata ziro katika kuwaona, zipo hapa: http://www.freewebs.com/abu_princeton3/someillusions.htm

  JibuFuta
 16. Asante dada Subi kwa kuunganishi. Nitapita hapo kuchangamka

  JibuFuta
 17. Kinachoniuma ni kwamba pamoja na hayo yoote wasemayo, mie naona binti na huyo bibi naona jicho tuu. Siwezi kuunga hiyo picha ya bibi. Hebu nitoeni tongotongo jamani. Sikio ni jicho, na vingine viko wapi? Yaani mmesema kidevu cha binti ni pua ya Bibi? Kageukia wapi na vingine vya kumuonesha vema ni vipi?
  Usicheke, si unajua twatofautiana? Wengine akili kama ulimbo na sie ndio kama dawa za kikohozi (shake well before use).
  Lol

  JibuFuta
 18. Wewe si umeanza na sura ya binti? Ok sasa angalia pale shingo inakounganika na mabega, kuna kijimstari hivi cha nguo, umekiona? Sasa hicho kijimstari kifanye ndio mdomo wa bibi kizee, mabega ya bibi yawe ndio kidevu, halafu sura ya binti iwe ndio pua ya binti, sikio la msichana liwe ndio jicho la bibi, halafu hizo nywele za binti zilizoangukia nyuma ziwe ndiyo makunyanzi ya bibi.

  Hebu cheki vizuri, ikiwezekana shika kabisa picha ukifuatilizia. Te he te he ehe

  JibuFuta
 19. Anon wa 4/3/09 9:30 PM amejitahidi sana kumwonesha Mube picha kwa njia ya maandishi, sasa Mube tumechoka kukuelekeza, tumesha-shake well before use kilichobakia ni wewe kuingizwa kwenye zamu ya ratiba ya fimbo tu. Basi!

  JibuFuta
 20. Subi, unafikiri kwa nini Mubelwa amechelewa kumwona 'bibi'?

  JibuFuta
 21. Bwaya, mi nadhani Mube amechelewa kumwona Bibi kwa kuwa aidha anafanya kusudi kwa kuwa ana lake jambo, hivi anatuzingua tu hapa na kuturusha roho pasina sababu atuone subira zetu zinachukua muda gani kabla ya kwisha, na tukamgeukia tukamcharaza viboko baku baku na picha akaiona bila miwani. Ama Mube ni mwepesi wa kuwaona mabinti na watu wa rika yake tu.

  Wewe Mube wewe, kwa nini unapenda kutizama wasichana tu na wazee usiwaone? Hii picha itaachwa hapa kwa Bwaya, utakapozeeka tutakukokota hadi hapa tukuulize swali hili hili halafu tusikize majibu yako, na wakati huo ukianza kwa kumwona binti, si neno, ila na bibi lazima umwone. Kwa kweli utamwona tu. Yaani usijaribu kuthubutu kutokumwona bibi!

  Bwaya (tuache utani), kitaalamu we unafikiri ni kwa nini Mube hakuwaona kabisa watu hawa wawili na sasa anachelewa kumwona Bibi?

  JibuFuta
 22. Lol. Subi umenikandamiza lakini nasema ukweli. Unajua nampenda bibi yangu kuliko mke wangu? Lol.
  Anyway, nadhani namna nionavyo hili tatizo / tega n'tegue ndio tatizo / mtego

  JibuFuta
 23. Kuna nadharia nzuri. Ngoja tusubiri amwone kwanza...

  Mube umemwona bibi?

  JibuFuta
 24. Kuna nadharia nzuri. Ngoja tusubiri amwone kwanza...

  Mube umemwona bibi?

  JibuFuta
 25. Bado naangalia. Sasa sikia yaliyonikuta leo hapa kazini. Nimefungua picha, akaja best yangu nikamuonesha akasema anamuona binti. Nikamtafsiria alivyoandika anon (nashukuru kwa maelezo hapo juu) jamaa akamuona bibi akafurahi akaenda kuwaita na wenzake watano, tukakaa hapa naeleza na kueleza lakini ni yeye pekee aliyemuona. Hajaamini kama hatumuoni na hakuwa akijua kuwa mimi simuoni, sasa jamaa mwingine aliposema hebu nipe details kidogo, nikasema mie mwenyewe namuona bibi nusu, sioniyake kamili. Best yangu kachoka na sidhani kama anaamini kuwa nimempa hints za kuona alichokuwa hakioni na bado mimi sioni.
  Ila nimefarijika kuwa siko peke yangu mwenye "jicho bovu" ( i hope sio kwamba kampuni imejaa kina sie)
  Naendelea kuangalia wakuu. Mpaka nimuone bibi yangu vema

  JibuFuta
 26. I got itttttttttttttt!!!!!!!!!!
  Najiona mwerevu sasa. Najiandaa kuwakusanya wenzangu niwaelimishe.
  Thx all

  JibuFuta
 27. Jamani! Kwenye kidevu cha huyo mnayemwita bibi kuna mzuzu, na ndicho hasa kilichoniridhisha mimi nitafsiri mzee huyu kuwa ni babu. Kwani kile kilichozunguka kwenye kidevu chake mwakitafsiri vipi? Nisaidieni hapa, ila dada Subi usianze na viboko tafadhali!

  JibuFuta
 28. Hongera sana Mube.

  Sasa tuambie (kwa kumwangalia vizuri hivi sasa) kwa nini unafikiri umechelewa sana kumwona bibi?

  JibuFuta
 29. Ha ha haaaa, kwanza nianze na Kissima, fimbo anayo Mnali bado, kisha tupo mbali sana, itabidi atumie meli kuisafirisha hivyo usijali kabisa, hamna viboko.
  Nimalize na Mube, pole sana kwa kazi kubwa uliyoifanya na hongera kwa kutumia picha kuchangamsha akili za wengine. Hongera kwa kumwona bibi.
  Kwa wote,
  Ikiwa ni msikilizaji ama msomaji wa taarifa na tafiti mbalimbali, utakubali usemi kuwa michezo yoyote ya kuchangamsha akili ni mizuri katika kuimarisha kumbukumbu na kuongeza uwezo wa ubongo kutafsiri mambo mbalimbali katika jamii tofauti, aghalabu, michezo ya kuchangamsha akili ni mizuri kwa afya ya mwili na huongeza kujiamini katika kujumuika na watu mbalimbali kwani hata usipokuwa na la kuchangia kuhusu mkutano wowote bado unaweza kutumia michezo ya akili kujiweka sawa katika kundi - ndiyo siri ya kuanza urafiki!

  JibuFuta
 30. Duh naona picha ya msichana tu!

  JibuFuta
 31. Egidio ni lazima ungemwona msichana. Kwa umri wako huwezi kumwona bibi ha ha ha aaa!

  Karibu sana kaka. Nimefurahi umerudi tena.

  JibuFuta
 32. Jamani na mimi sioni kitu zaidi ya binti na jicho la bibi ambalo ndilo sikio la binti. Nadhani niko sawa na mzee wa changamoto.

  JibuFuta
 33. Tazama kwa makini Dada Mija. Kuna bibi katazama chini. Fuatilia maelekezo ya anon hapo juu amejaribu kuelekeza vyema.

  Karibu sana Mija.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3