Usiyetaka kukosea...

KUNA watu huamini kabisa kukosea kwao hakupo. Kukosea ni kudhalilika.

Wanasahau kukosea ni sehemu ya kupatia.
Na kupatia hakuwezi kuwepo bila kukosea.

Wanasahau 'wasiokosea' ni wale wasiofanya lolote jipya. Waoga wa kujaribu. Waoga wa kukoselewa.


Ndio maana kwao, kuomba msamaha ni sehemu ya adhabu dhalili.

Je, ni haki kuwalaumu 'wakosefu'?

Maoni

 1. Inategemea,unaweza kumlaumu mtu kama kosa hilo hilo anamekuwa akilirudia mara kwa mara.Mtu wa namna hii kama anajielewa vizuri,yeye mwenyewe lazima nafsi yake imsute,lazima ajiulize kwa nini,kwa maana hii hata yeye mwenyewe atakuwa anajilaumu.Kimsingi hatakiwi kukata tamaa bali kuweka agenda ya kujirekebisha kwa kadiri awezavyo na hatakiwi kukatishwa tamaa na wanaomlaumu.
  Kuna mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema
  "experience is a hard teacher,he gives you test first and a lesson there after"

  JibuFuta
 2. sasa kwa nini unaulizia juu ya uwezekano wa kuwalaumu wakoseao wakati unaonyesha sivyo?

  mbona sasa wewe tayari umeshakosea? je nikulaumu kwa hilo?

  kwani kosa ninini na kukosea kunafananaje? mimi sijui!

  JibuFuta
 3. Kulaumu akoseaye nafikiri ni RUKSA!
  Naamini kulaumiwa inaweza kurutubisha uangaliaji wa kosa kwa alaumiwaye zaidi kidogo kuliko kusipokuwa na lawama.

  Katika maisha yenye mengi tunasahau mengi kwa kuhangaika na mengi na lawama ni kitu kimoja kisaidiacho kuturudisha katika swala ambalo tokea litokee labda tumeshaharibu kwingine.

  Cha muhimu ni kujifunza kutoka kwenye kosa ingawa jamii inatabia mbaya. Ukikosea na kujikojolea hadharani unaweza kuitwa milele kikojozi kwa kosa la kujikojolea kama ni kosa. Ukifaulu kwa kimoja kipendwacho sana kam Eistein au Gandhi, mengine makosa husahauliwa .Ukijulikana kwa upendo kama Yesu , stori zako za kupiga wafanyabiashara kwenye sinagogi hazionekani kosa la kutumia nguvu au ugomvi.

  Na kunauwezekano ukiamini kukosea ni sehemu ya kupatia ukajikuta unaridhika na kukosea.:-(

  JibuFuta
 4. @ Kisima umesema "...akilirudia mara kwa mara..." sasa unamhesabu mkosaji kwa vigezo gani? Hapa nina maana ya kuuliza unajuaje kwamba kakosea? Kama alichofanya hapiswi kulingalishwa na yaliyopita, unatuaje kwamba kakosea "mara kwa mara"?

  @ Kamala,
  Tendo haliwezi kuhesabiwa kuwa ni kosa kama tendo hilo litapimwa lenyewe kama lilivyo. Kosa ni pale tendo husika linapopimwa kwa kulilinganisha/kulipambanisha na matendo mengine.

  Kwa hivyo ninaweza kuwa nimekosea kama "nikilinganishwa na" matarajio fulani ambayo kimsingi sikuwa nayo.

  @ Mkodo, kama nikiamua kuwa kupatia kuwe ni kwa vigezo vya suala husika bila kufanya majaribio ya kulilinganisha suala hilo na "yaliyopita" kwa nini ionekane kama nakosea?

  Na hata hivyo nikiridhika na 'kukosea' (kwa maana ya kujilinganisha na matarajio fulani yasiyokuwa halisi) si ni faida kwamba nitaendelea kujaribu na kujaribu?

  JibuFuta
 5. Kwani Bwaya wazo la kukosea ulilipata kivipi? Au kukosea kuna maana gani? Kama sio kurudia jambo ambalo fika linajulikana si sahihi?
  Ukiweka chumvi kwenye chai ambayo sukari ndio ilitakiwa kuwekwa, utakuwa umekosea, lkn binafsi sitakulaumu, lkn ukirudia tena, lazima nikulaumu lkn kwa maana ya kukusisitizia ktk kutokurudia.

  JibuFuta
 6. Kama jumuiya imekubaliana kuwa swala fulani ni kosa, basi anayetenda kosa lile anafanya hivyo makusudi ni haki kumlaumu.

  JibuFuta
 7. Bado sina hakika hasa kosa ninini.Kwa mfano ukiwa mkristo ukioa mke zaidi ya mmoja wanasema ni kosa lkn muislamu anaruhusiwa na wote tunaishi kwenye jamii hiyo hiyo.Ukipigana na rafiki yako ikatokea ukamuua kwenye ugomvi wanasema ni kosa lkn kuna wenye mamlaka ya kuua walioua wenzao,hawa inasemekana hawana makosa ingawa nao wanaua watu wengi zaidi kuliko yule aliyeua kwenye ugomvi.
  Ukiua ukiwa huna jina kubwa linalotanguliwa na waziri,mkuu wa mkoa au rais unakamatwa mara moja na inasemekana ni kosa lisilokuwa na dhamana,lkn jina lako kama lina kitangulizi huwezi ukakamatwa mpaka iundwe tume au itatangazwa kuwa huna kosa ila uliua kwa bahati mbaya.
  Jamani nisaidieni mimi bado sijui kosa ninini na ni nani anayeamua kuwa suala au kitendo fulani kiitwe kosa?
  Je huyo mtu au hao watu wapo sahihi?

  JibuFuta
 8. Fred nimependa maswali yako mazuri. Bila shaka yatapanua zaidi mjadala. Kwamba kitu hichohicho chaweza kuhesabiwa kosa na wakati huo huo chaweza kuwa si kosa. Tunahitaji majibu katika hili.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Pay $900? I quit blogging