Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2008

Watu wanapata taswira gani wanapokutazama?

Binadamu anao uwezo wa kujenga taswira yake - namna anavyoonekana - kwa wengine kwa kadiri apendavyo awe. Binadamu anaweza kuamua kuonekana mtu wa heshima zake, ama hata kuonekana mtu asiye na heshima zake. Uamuzi wa kujenga taswira hiyo, self-image kwa msisitizo, uko mikononi mwake yeye mwenyewe. Kwamba tunafikiri wengine wanatuchukuliaje ni suala la kujenga taswira zetu. Kwamba zaidi ya kule kujitathimini wenyewe, kujiangalia kwa macho yetu wenyewe, tunajaribu kujitazama kwa macho ya watu wengine. Tunajaribu kujifikiria kwa miwani ya wanaotuzunguka. Tukijiuliza swali kubwa: hivi huyu jamaa ananionaje hapo alipo? Self-image. Si tu kujiaminisha kuwa tu watu wa aina fulani kwa kutumia vigezo vyetu, bali kujaribu kurudusu, wengine wanatuonaje. Hatuwezi kujifahamu sisi ni akina nani kwa kujiangalia kwa macho yetu wenyewe. Macho yetu hutudanganya na mara zote hutafuta kutupendelea. Macho yetu hutafuta kutufanya tujisikie vizuri kuhusu nafsi zetu. Hivyo, tunapotaka kujifahamu kwa usahi

Fujo huanzishwa na 'wenyenguvu' si wanyonge

Hakuna mahali katika historia (labda niambiwe vingine) panapoonesha kuwa matumizi ya nguvu - mapigano na vita, huanzishwa na wanyonge. Ni hivyo kwa sababu wao wenyewe (wanyonge) ni matokeo ya ' maguvu' ya wenye nguvu. Ni hivyo kwa sababu pasingelikuwapo watu wanaoitwa wanyonge, bila hao wanaojiona wana nguvu kuzidi binadamu wenzao, wenye haki kama wao. Hivyo, mapigano huanzishwa na mabwana wakubwa wao wenyewe, kwa kiburi chao cha kugoma kuwatambua na kuwasikiliza wenzao kama binadamu pia. Mapigano huwa hayaanzishwi na wale wanaoonewa, wanaonyonywa na wasiotambuliwa na kuheshimiwa. Wasiopendwa huwa hawasababishi chuki, bali wale wasiopenda wenzao ambao hujipenda wao wenyewe. Si wasiojiweza - waathirika wakuu wa ugaidi - huweza hata kufikiri kuanzisha ugaidi, bali wenye maguvu ambao hutumia maguvu hayo kupunja haki za wenzao kwa kuwahesababu kama watu wawezao kuondoshewa uhai wao wakati wowote ule. Si waliodharauliwa huweza kuanzisha visasi, bali wale wenye dharau wenyewe.

Mtumwa asiyeona haja ya uhuru?

Haishangazi kuwa mtumwa. Kinachoshangaza ni kule kuwa mtumwa asiyejielewa kwamba yu utumwani. Kule kuwa mtumwa mzoefu kiasi cha kuuhesabu utumwa kuwa sehemu ya maisha yako kamili. Kiasi cha kushindwa kutofautisha kati ya utumwa na uhuru. Unajikuta ukiogopa kuwa huru. Mtumwa mzoefu. Mtumwa mwaminifu. Mtumwa anayefurahia kuwa utumwani, utatumia lugha gani kumwelewesha kuwa hayuko huru? Maana kwake yeye uhuru ni utumwa, na utumwa ni uhuru. Unawezaje kumsaidia akasaidika? Nimeamka na sentensi hizo asubuhi ya leo. Heri ya mwaka mpya.