Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2017

Unajengaje Uhusiano Mzuri na Viongozi Kazini?

Picha
Moja ya mambo yanayoweza kukusaidia kufanikiwa kazini ni namna unavyohusiana na mkubwa wako wa kazi. Huyu ni mtu anayekuongoza, anayetoa maelekezo ya nini kifanyike na wakati mwingine ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye taasisi, idara au ofisi unayofanya kazi. Kwa nafasi yake, kiongozi wa kazi ni mtu mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi yanayohusu kazi yako hata kama anaweza asiwe mwajiri wako moja kwa moja. Huyu ni mkuu wa ofisi, idara, kitengo, kampuni au taasisi unayofanyia kazi. Ndiye mtu anayekusimamia na kupokea taarifa za utendaji wako na labda kuzipeleka kwenye mamlaka za juu.

Utamaduni wa Demokrasia Uanzie Ngazi ya Familia

Picha
PICHA: Dennis Louis Tumesikia madai kuwa baadhi ya watawala wetu wa ki-Afrika ni madikteta. Watawala hawa wanashutumiwa kupuuza haki ya raia kueleza mawazo yao wazi wazi bila hofu ya ‘kushughulikiwa.’ Inavyoonekana wananchi wana matamanio ya kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kudhibiti serikali wanazokuwa wameziweka madarakani. Bahati mbaya watawala wanapopata madaraka huziba masikio yao sambamba na kuhakikisha vivywa vya wananchi haviwezi kusema kinyume na maoni waliyonayo watawala.

Yatambue Madhara ya Adhabu ya Bakora

Picha
INGAWA wazazi wengi huwachapa watoto wakiamini wanafanya hivyo kwa lengo la kuwaadabisha, tulibainisha sababu zilizojificha. Kwa ujumla, tunaweza kusema mzazi aliyelelewa kwa fimbo hujikuta na yeye akiamini fimbo ndio suluhu ya matatizo ya kinidhamu anayoyaona kwa mwanae.

Mzazi Ufanyeje Unapompeleka Mwanao Shule ya Bweni?

Picha
PICHA: Paul Jeffrey PAMOJA na changamoto za malezi ya shule za bweni tulizoziona, bado mzazi anaweza kulazimika kumpeleka mwanae kwenye shule hizi. Kwanza, kuna suala la kazi. Wazazi wanaofanya kazi mbali na familia zao wanaweza kuamua kuwapeleka watoto kwenye shule ya bweni ili wasiwe na wasiwasi na uangalizi wao.

Umuhimu wa Kiongozi Kuwa Mnyenyekevu -2

Picha
PICHA: entrepreneur.com JUMA lililopita tuliona kuwa mtu huhitaji sifa fulani kumwezesha kupanda ngazi za uongozi. Mtu anapokuwa na uwezo wa kufanya kazi na watu; kuwasiliana vizuri na wakubwa wake wa kazi na hata walio chini yake na kufuatilia mambo ya msingi kwa makini anakuwa katika nafasi nzuri ya kupewa madaraka.

Namna ya Kujenga Uhusiano Mzuri na Wafanyakazi Wenzako -2

Picha
PICHA: gainrecruitment.com Katika makala yaliyopita , tuliona tabia mbili unazozihitaji ili kujenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzako. Tabia ya kwanza ni kuwafanya wenzako wajione wana hadhi ya juu kuliko wewe. Unapowafanya watu waamini wanakuzidi, kwa kawaida unawaondolea sababu ya kupambana na wewe. Tabia ya pili ni kuwasaidia wenzako kufikia malengo yao. Tulisema, kila mtu anajipenda. Sisi binadamu ni wabinafsi kwa asili. Ni nadra kumpenda mtu asiyetupenda. Tumia hulka hiyo kunyoosha mambo yako. Wasaidie wenzako kufanikisha malengo yao. Ukifanya hivyo, unatengeneza mtandao wa watu watakaojisikia kuwajibika kukusaidia na wewe. Katika makala ya leo, tunaangazia tabia nyingine nne zinazoweza kukusaidia kujenga mahusiano mazuri ya kikazi na wenzako.

Kwa Nini Wazazi Tunawachapa Watoto?

Picha
PICHA: M ountain TV I Gilgit-Baltistan ‘Nakubaliana na njia unazopendekeza (kumfundisha mtoto tabia njema kwa kushirikiana nae). Lakini hii ya kutokumchapa sikubaliani nayo,’ ananiandikia msomaji mmoja na kuendelea, ‘Nina watoto wakubwa nimewachapa tangu wakiwa wadogo na wanakwenda vizuri tu […] Naelewa hatari ya kutokumwadhibu mtoto. Viboko vinasaidia sana sana kumnyoosha mtoto. Usipompa mapigo mtoto unakaribisha maradhi. Biblia iko wazi katika hili.’

Kuyamudu Mafanikio Yako...

Picha
Fikiria umehitimu masomo kwenye chuo maarufu; umepata alama nyingi kwenye mtihani mgumu; umepata kazi yenye heshima; umejenga nyumba nzuri; umenunua gari la ndoto zako; umesafiri kwenda mahali wanakotamani kwenda watu na hawawezi au basi tu umekutana na mtu fulani maarufu. Unajisikiaje kama watu hawatafahamu? Kwa nini watu wakifahamu unajisikia vizuri zaidi?

Namna ya Kujenga Uhusiano Mzuri na Wafanyakazi Wenzako -1

Picha
PICHA: tovoy.se Moja ya sababu zinazowafanya wafanyakazi wengi wakose ari ya kazi ni mahusiano mabaya na watu kazini. Kimsingi, tafiti nyingi zinabainisha kuwa, mbali na kutokuridhishwa na maslahi ya kazi zao, wafanyakazi wengi hufikia huacha kazi kwa sababu ya kutokuelewana na watu kazini. Unapokuwa na watu wengi ofisini kwako wasiofurahia kukuona; watu wanaokerwa na kazi nzuri unazozifanya; watu wanaokuonea wivu; watu wanaojenga uadui na wewe, ni rahisi kukosa amani na mazingira ya kazi unayoifanya. Kukosa amani kazini kunakuondolea ujasiri na uchangamfu wa kuchangamana na wenzako. Hali hii, kwa kiasi kikubwa, inaweza kupunguza ufanisi wako kazini.

Fanana na Unayetaka Asikilize Nasaha Zako

Picha
Fikiria mtoto amekuwa na tabia ya kufanya vibaya darasani. Wewe kama mzazi hupendi hali hiyo. Ungetamani mtoto afanye vizuri. Kwa shauku hiyo, unaona uongee na mwanao kumhamasisha afanye juhudi kwenye masomo. Unamwambia, 'Hebu jitahidi mwanangu. Alama hizi unazopata hazifai. Mimi sijawahi kupata alama hizi. Nilipokuwa na umri kama wako, nilikuwa na bidii sana kwenye masomo. Kwa sababu ya kufanya bidii, siku zote nilishika nafasi kati ya nambari moja na tatu darasani!' Lengo ni jema kabisa. Unachofikiri hapo ni kuwa mwanao akisikia simulizi la mafanikio yako, atahamasika na kuanza kujitahidi. Unafikiri uwezo wako unaweza kumtia hamasa kijana. Inawezekana ikawa hivyo. Lakini mara nyingi mambo huwa kinyume.

Shirikiana na Mtoto, Usishindane Nae

Picha
Tunaendelea kujibu swali linaloulizwa na wazazi wengi, ‘kwa nini watoto hukosa adabu?’ ‘Kwa nini wakati mwingine watoto hawasikii hata pale wanapoadhibiwa?’ ‘Inakuwaje mtoto anakuwa na nidhamu mbele ya mzazi lakini akiwa mbali na mzazi anakuwa na tabia nyingine?’ Jibu la maswali haya ni mjadala mrefu. Hata hivyo, tumejaribu kuonyesha kwamba mtoto kukosa adabu haitokei kwa bahati mbaya. Kwanza, hazaliwi na msukumo wa kushindana wala kumkosea adabu mzazi. Badala yake, huzaliwa na fahari ya kumpendeza na kushirikiana na mzazi. Kwa mfano, mtoto hufurahia mzazi anapocheza nae, anapomkumbatia, anapomrusha rusha kwa furaha na hata anapomtania.

Kanuni Nne za Kufurahia Kazi Yako

Picha
Kwa nini unaamka asubuhi kwenda kazini? Kitu gani kinakupa sababu ya msingi ya kwenda kazini?  Ni dhahiri vigezo tunavyovitumia kufurahia kazi haviwezi kufanana.  Wapo wanaofurahia kiwango kikubwa cha mshahara. Thamani ya kazi inategemea na ukubwa wa kipato. Wengine wanaridhika na kazi inayowajengea hadhi katika jamii. Kazi inayowaongezea hadhi inawapa kuridhika.