Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Imani na Mitazamo

Mwanaume anapokimbia 'kelele' nyumbani

Picha
  Mwanadamu ana uwezo mkubwa wa kuficha tabia. Samahani. Namaaminisha mwanaume. Unajua, katika jamii zetu, ni aibu mwanaume kukiri mahusiano yamekushinda. Kuliko kuitwa kila aina ya majina saa nyingine tunalazimika kujenga taswira ya ukamilifu hata kama kiuhalisia tunaugulia maumivu makali. Jumlisha hapo dini, kwa maana ya hizi itikadi za ufuasi wa halaiki, kiwango cha kuonesha ukamilifu lazima kiwe juu zaidi.   Tumeaminishwa ndoa ni kielelezo cha ukamilifu. Hakuna kukosea. Ukishasema una changamoto na mwenzako, watu wanakupiga jicho la dhihaka, “Hukumwomba Mungu akupe mke? Humtegemei Mungu vya kutosha?” Nani yuko tayari kuonekana hana uhusiano mzuri na Mungu?   Kwa upande mmoja, ninamuelewa sana Godi. Hofu ya kuchafua jina lake inamfanya aigize amani ya ndoa isiyokuwepo.   Swali nililojiuliza, kwa nini sasa Godi amefikia mahali hajali watu wa nyumbani kwake? Kama ana tatizo na mkewe, inakuwaje anashindwa kujali hata watoto?    Kila tabia, kwa ...

Unaweza Kumruhusu Mtoto Afuate Dini Apendayo?

Picha
PICHA: Pixabay Ipo nafasi muhimu ya imani/dini katika malezi ya watoto. Imani si tu inamsaidia mtoto kujitambua, lakini pia ina nafasi ya kumtengenezea mtoto sauti kutoka ndani yake inayomsaidia kupambanua lililo jema na baya. Sauti hii inaitwa dhamira. Utakuwa shahidi kuwa kuna mambo wakati mwingine unatamani kuyafanya lakini unajisikia hatia kuyafanya. Unaweza, kwa mfano, kuwa na uhuru wa kutaka kufanya chochote, lakini kuna sauti ndani yako ikakunyima ujasiri wa kukifanya. Hakuna anayekuona, hakuna anayekuhukumu, lakini kuna kengele ndani yako inakwambia kuwa unachotaka kukifanya sio sahihi. Mwanasaikolojia wa kale anayeitwa Sigmund Freud aliita kengele hiyo ‘Superego’ kumaanisha mkusanyiko wa maelekezo tunayoyapata kwa watu wanaotuzunguka. Kwa kawaida, sauti na maelekezo hayo inayoumbika ndani yetu ndiyo inayoamua namna gani tunadhibiti matamanio yetu ya asili kama hasira na tamaa za mwili. Imani, tafiti zinasema, ina kazi kubwa ya kujenga dhamira. Mtu mwenye ...

Wanavyokufahamu Watu Ndivyo Ulivyo?

Picha
PICHA: NCC PE ‘Jamaa ana madharau sana!’ alilalamika Lazaro. ‘Nani?’ alihoji Msafiri. ‘Si Peter?’ Uso wa Msafiri ulionesha mshangao. Hakufikiri Peter anaweza kuwa na dharau kama Lazaro anavyodai. Msafiri anamfahamu Peter mwenye tabia nyingine kabisa. Kwake, Peter ni rafiki,  mtu wa watu asiye na neno na mtu. ‘Peter huyu huyu ninayemfahamu mimi?’ Msafiri aliwaza kimya kimya akikumbuka namna Peter alivyomsaidia hivi majuzi alipokuwa na shida ya fedha. Hakuna rafiki aliyemsaidia isipokuwa Peter. Hakupata kufikiri hata mara moja kwamba Peter angeweza kuwa dharau akaona aulize imekuwaje, ‘Kwa nini umefikiri hivyo Lazaro?’ ‘Jamaa ana kiburi sana aisee. Nimepishana nae mjini kati jamaa kama hanifahamu vile. Na kile ki Vitz chake yaani kama hanioni vile!’ ‘Labda hakukuona mkuu. Peter hayuko hivyo.’ ‘Hapana alikuwa ananiangalia kabisa. Kaudhi sana jamaa. Tangu awe na hicho kigari kabadilika mbaya. Kijiweni haji tena. Anajifanya yuko busy.’ Msafiri haamini a...

Mwanaume Anayejitambua Hatishwi na Mafanikio ya Mwanamke

Picha
PICHA: Ayo Martins Upo ukweli usiosemwa wazi kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Wanawake waliosoma, wenye mali na fedha, wenye madaraka makubwa katika jamii, wanakuwa na mtihani mkubwa kuanzisha na kudumisha uhusiano na wanaume.

Namna ya Kupunguza Changamoto za Wasichana wa Kazi

Picha
TUMETAJA mambo mawili yanayobadili mfumo wa malezi. Mosi, ni kubadilika kwa majukumu ya kijinsia yaliyozoeleka katika jamii. Mama anapoingia kwenye soko la ajira na kwenda kazini kama ilivyozoeleka kwa baba, changamoto inayojitokeza ni namna wanavyoweza kumlea mtoto wao katika muda wa kazi. Pili ni kufifia kwa utamaduni wa familia tandao unaozorotesha msaada wa kimalezi uliozoeleka kutoka kwa ndugu wa karibu. Mawili haya yanalazimisha familia za sasa kutafuta namna nyingine ya malezi kuwapa fursa wazazi kuendelea na kazi.

Unaweza Kumfundisha Mtoto Adabu Bila Kumchapa

Picha
Mjadala wa fimbo na malezi una historia ya mjadala mkali. Fimbo, kwa hakika, zimekuwa kama sehemu ya maisha yetu . Takwimu zinathibitisha hali hii. Kwa mfano, asilimia zaidi ya 80 ya wazazi wa nchi zinazoendelea wanatumia fimbo angalau mara moja kwa mwezi. Ndio kusema, vipigo kwa watoto vimekuwa sehemu ya malezi katika nchi zetu hizi. Matumizi haya makubwa ya fimbo kwa kiasi fulani yanatokana na imani waliyonayo wazazi kuwa bila mtoto kusikia maumivu hawezi kurekebisha tabia wala kuwa msikivu. Ingawa hakuna ushahidi wowote kuwa viboko vinasaidia kujenga nidhamu kwa watoto, bado wazazi wengi wanaamini adhabu ya fimbo ndiyo jibu la kumnyoosha mtoto.

Tunavyoweza Kuacha Tabia ya Kuhukumu Wengine

Picha
Majuzi nikiwa kwenye mgahawa mmoja mjini, waliingia watu wawili wanaume waliokuwa wamevalia mavazi yanayoashiria imani yao ya kidini. Wote wawili walipamba vichwa vyao kwa vilemba nadhifu, mmoja wao akibeba mfuko mdogo mweusi. Nyuso zao, kwa hakika zilipambwa na tabasamu pana la kirafiki lililofanya ndevu zao ndefu ziwe na mwonekano wa kupendeza. Miguu yao ilivaa viatu vya wazi na juu yake zilining’inia suruali fupi mithili ya kaptula ndefu zilizojitokeza ndani ya kanzu fupi nadhifu.

Tuyafanyayo ni Matokeo ya Tujionavyo

Picha
Ungeulizwa swali, ‘wewe ni nani’ ungejibuje? Wengi tungetaja majina yetu kwa kuamini ‘sisi’ ni majina yetu. Wengine tungetaja kazi zetu kwa sababu kwetu majukumu ndio utambulisho wetu. Sisi ni nani basi? Kwa hakika swali hili si jepesi lakini linatuwezesha kuelewa tabia zetu. Karibu kila tunachofanya ni matokeo ya vile tujionavyo. Katika makala haya, tutaangazia  mitazamo michache inayoweza kutusaidia kutafakari swali hilo. 

Kuanza Kupotea kwa Desturi ya Ukaribu wa Kifamilia Kunavyoathiri Malezi

Picha
Malezi katika mazingira yetu ya ki-Afrika ni suala nyeti. Kwa kutambua umuhimu wa malezi katika kujenga jamii yenye ustawi, wa-Afrika tumekuwa na desturi ya kuelekeza nguvu zetu nyingi katika malezi ya wanetu. Kwa mfano, tangu mtoto anazaliwa, ilikuwa ni lazima alale kitanda kimoja na wazazi wake kwa muda unaozidi miaka miwili. Mtoto mchanga hakuachwa alale kwenye kitanda chake mapema kwa sababu za msingi zilizokubalika katika jamii zetu.

Watoto Wagomvi, Wasumbufu na Wenye Utukutu katika Umri wa Miezi 0 – 36

Picha
Tangu tumeanza mfululizo huu, tumejaribu kuonesha namna tabia za mtoto zinavyohusishwa na malezi ya mzazi kuliko vinasaba. Kwa ujumla tumeona kile anachokifanya mtoto ni matokeo ya kufikiwa au kutokufikiwa kwa matarajio yake . Katika makala haya tunaangalia kundi la watoto wenye tabia za ugomvi, utukutu, ukaidi na usumbufu na kuona namna mazingira ya kimalezi yanavyochangia hali hii.

Kwa nini ni rahisi kumsifia mtu akifa kuliko akiwa hai?

Picha
Hatupendi kuwasifu wengine wala kusikia wakisifiwa na wengine, lakini ni wepesi sana kumsifia marehemu. Na ni nadra kusikia tabia ya marehemu ikikosolewa. Hata waliokuwa hawamsifii akiwa hai, huomba fursa ya kuusemea vizuri wasifu wa mpendwa aliyetutoka. Mtu fulani maarufu akifa, kwa mfano, watu ambao hata siku moja hawakuwahi kumsema marehemu enzi za uhai wake, ndio huanza kushindana kutundika picha zake zikiambatana na maneno ya ‘apumzike kwa amani’. Sasa swali, kwa nini ni vyepesi kumsifia marehemu asiyesikia kuliko kumsifia binadamu anayesikia?

Unaanzisha mahusiano ya ndoa/mapenzi?

Picha
MAZUNGUMZO mengi yanayohusu maandalizi ya ndoa hujikita katika kufanikisha tukio la siku ya harusi. Na wakati mwingine wanaojiandaa kwa ndoa huandaliwa siku chache sana kabla ya tukio hilo. Kwa ujumla, suala la ndoa limerahisishwa kiasi cha kuonekana kuwa yeyote anaweza kukabiliana nalo kwa uzoefu pasipo maandalizi ya kutosha. Hata hivyo, pamoja na wepesi wa maandalizi halisi, na msisitizo uliowekwa na jamii katika 'siku ya harusi', ndoa nyingi huishia kwenye migogoro mingi muda mfupi baada ya tukio la harusi.

Muhtasari na Hitimisho, 'Kanuni zinazoongoza mahusiano na migogoro ya wanandoa'

Picha
TANGU tulipoanza mfululizo wa makala za mahusiano , jambo kubwa nililojaribu kulionesha ni nafasi ya mahitaji ya hisia katika kuimarisha au kuvuruga mahusiano. Na msingi wa haya yote ni kusema kwamba mahusiano hayana miujiza. Mahusiano yanaongozwa na kanuni za kawaida sana ambazo ukifanikiwa kuzitambua na kuzitumia utapunguza kama sio kuondoa matatizo mengi. Kwa mhutasari, ningependa tuyapitie mambo makuu yaliyojitokeza katika mjadala wetu kwa kuyaweka katika makala moja inayojitegemea.

Kama mwanaume, uko tayari kulipa gharama za mahusiano bora?

Picha
UNAPOWASIKILIZA wanaume wengi wakizungumzia kile wanachodhani wao kinawagusa wanawake kwenye mahusiano, utashangaa orodha ya vitu hutawala mazungumzo. Kwa mwanaume wa kawaida, mwanamke anahitaji vitu ili akupende. Utasikia, "Ah, mwanamke pesa. Ukiwa na hela zako bwana, basi." Imani ni kwamba wanawake wanahitaji sana vitu na hivyo ndivyo vinavyowavuta na kuwabakiza kwenye mahusiano. Pamoja na ukweli fulani kwamba vitu navyo vina nafasi yake kwenye mahusiano, hasa kwenye kizazi hiki cha sasa kinachotanguliza thamani ya fedha kuliko kitu kingine chochote, bado huwezi kuthamanisha moyo wa mwanamke na fedha, ingawa ni kweli anazihitaji. Kudhani kwamba baada ya kuhakikisha mwanamke amepata kila anachokihitaji kwa maana ya vitu, basi unaweza kuendelea na shughuli nyingine kwa kuamini umemaliza kazi, ni kutokuelewa mahitaji halisi ya kihisia ya mwanamke. Najua wapo wanawake wasiohitaji kingine chochote kwa mwanaume zaidi ya fedha na vitu. Mahitaji ya kihisia tunayoyaz...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -2

Tuliona katika makala iliyopita  maana ya saikolojia na kuhitimisha kwamba kinachotazamwa zaidi katika saikolojia ni tabia. Kwa hakika matatizo mengi yanayoikabili jamii yetu chanzo chake ni tabia. Tabia ndio chanzo cha matendo tunayoyaona kama kukosekana kwa uaminifu, ubadhilifu wa mali za umma, ufisadi, migogoro ya ndoa, misuguano ya kijamii, chuki, upendo, ugaidi, unyanyapaa, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kidini, changamoto za kimalezi na kadhalika. Yote haya yanaweza kuchambuliwa na kupatiwa majibu yake kwa kutumia sayansi ya tabia (saikolojia). Katika makala haya nitatoa mifano mifano kadhaa kuonesha namna sayansi ya tabia, inavyoweza kutumika kutatua matatizo yanayoikabili jamii.

Mahusiano mazuri na watu hujengwa kwa kutambua na kuheshimu hadhi zao na sio kulinda hadhi yako

Picha
WATAFITI wa saikolojia ya jamii, wanakubaliana kuwa miongoni mwa sababu nyingi zinazosababisha hali ya mitafaruku katika mahusiano ya watu -iwe kazini, nyumbani, na kokote- ni kule kujisikia kushushiwa heshima. Kwa kawaida, binadamu hatupendi kushushiwa hadhi, ego, ambayo ndiyo hutufanya tupambane na yeyote anayetishia kuharibu namna tunavyojiona na pia tunavyoonwa na wengine. Tunaambiwa, watu wenye kuamini kuwa hadhi zao haziko salama , insecure, wenye kujihisi kama watu wenye hitilafu fulani, huwa ni wepesi zaidi kuhisi hadhi zao zinachezewa na hivyo kuhitilafiana na watu kirahisi. Hawa ndio watu ambao, unaweza kuwakosea kwa bahati mbaya huhisi kudharauliwa. "Acha dharau dada!" Ndio kusema hawaamini hadhi zao. Watu secure, wanaoamini kuwa hadhi zao hazitishiwi na wengine, si wepesi kukwaruzana na watu. Sababu ni kwamba hawaoni kirahisi threat ya heshima na hadhi zao, na vile vile wanao uwezo mzuri wa kulinda hadhi na heshima za watu wengine. Migongano ya kimahusiano...

Watoto waliolelewa kidini, wamegundulika kushindwa kutofautisha uhalisia na mambo ya kufikirika

Picha
MIAKA miwili iliyopita, 2012, Justin L. Barret alionyesha kwamba binadamu wote huzaliwa na hitaji la asili la imani na kutambua nguvu zisizoonekana na kwamba imani haitokani na jamii kama wanavyodai watu wasio amini uwepo wa Mungu. Kwa Barret, imani za kidini ni sehemu ya 'maumbile' ya asili anayozaliwa nayo mtu. Hoja zake kuu katika kitabu chake ni mbili 1) kwamba watoto wana uwezo wa asili wa kuamini nguvu za kimungu zisizoonekana kwa sababu ya, pamoja na mambo mengine, huamini uwepo wa miungu iwezayo yasiyowezekana kibindamu kabla hata ya kufikia hatua ya kujua kuwa watu wazima wanajua zaidi ya watoto 2) kwamba watoto sio madodoki ya kunyonya utamaduni unaowafanya kuwa waumini wa dini kwa sababu imani, hata hivyo, hutofautiana kati ya mtu na mtu, mahali na mahali na kadhalika. Soma pitio la kitabu Barret kiitwacho Born Believers: the science of children's religious belief. Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni unapingana na hayo aliyoyasema Barret miaka ipatayo miwil...

Ni kweli Israel haikosei kwa Mkristo kama ilivyo Hamas kwa Mwislam?

Picha
JUZI nikiwa katika pita pita zangu katika mitaa ya mjini, nimebahatika kukutana na bango kubwa sana barabarani. Bango lenyewe lilikuwa na ujumbe wa kuhamasisha maandamano ya siku ya Quds kupinga 'Masaibu ya Wapalestina' yatakayofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 25 Julai, 2014. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa umma, maandamano hayo yataanza saa 3 asubuhi, kuanzia kituo cha Boma, Barabara ya Kawawa, jijini Dar es Salaam. Bango hilo lina picha ya msikiti. Tutakumbuka kwamba Israel imekuwa ikiwashambulia vikali Wapalestina kwa siku za hivi karibuni, hali ambayo kwa kweli inasikitisha. Mamia ya Wapalestina wamepoteza maisha yao wakiwemo watoto. Ni hali ambayo inatia simanzi. Maandamano kadhaa tayari yameshafanyika kuishutumu Israel kwa mashambulio hayo. Israel kwa upande wao, wanadai wanachokifanya ni kulipiza kisasi kwa uchokozi wa Hamas. Siandiki kutafuta kujua nani anafanya vizuri na yupi anakosea katika mgogoro huo wa enzi na enzi. Hayo si ya leo. Bango lililoko maeneo ya ...

Kujikataa, kuikataa hali yako kwaweza kuwa kichocheo cha muhimu kujielewa

Picha
HUENDA umekutana na watu wanaoshauri ujikubali. Na huenda na wewe ni mmoja wao. Unajikubali. Kwamba ili kufanikiwa, ni busara ujipokee vile ulivyo na vyote ulivyonavyo kwa shukrani. Msingi mkuu, inasemwa, bila kujikubali na kujipokea huwezi kuwa na amani. Na amani na furaha, huenda, kama sio ndivyo ilivyo, likawa ndilo kusudi kuu la maisha ya mwanadamu. Purukushani zote tunazoziona, kukusanya mali, elimu, kuwa na familia bora, madaraka makubwa, umaarufu na kadhalika mwisho wa siku ni kutafuta furaha. Utoshelevu. Ridhiko la moyo. Watu wasiojikubali, tunaambiwa hawana amani na maisha yao. Wanavyojiona sivyo vile wanavyotaka wao. Matokeo yake, ndio hao wanajichubua wafanane na sura wanavyoitaka wao. Sote tumesikia maisha ya yule mwanamuziki maarufu mweusi aliyejigeuza afanane na wazungu. Matokeo mabaya ya kutokujikubali. Wengine tunasikia wakidanganya wasifu na elimu zao. Ulaghai. Lakini ukweli ni kwamba wanaona wasifu walio nao haufanani na vile wanavyotaka wao kuwa. Inabidi kudangan...