Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2006

Ben Carson: "Mswahili" bingwa Marikani

Afrika imejaa watu ambao wakizitumia mbongo zao ipasavyo wanatikisa kabisa historia ya Dunia hii. Wanatetemesha! Mifano ya waafrika waliosumbua historia yetu ni ndefu. Tatizo letu kubwa ni kwamba hatuwaoni mabingwa wengi walio nje na ulingo wa siasa. Ben Carson , ni Mmarikani mweusi, daktari bingwa wa Nyurolojia (Neurosurgeon)katika hospitali ya Johns Hopkins aliyewahi kutenganisha mara kadhaa mapacha waliounganika vichwa vyao. Kishawahi kuja Afrika, kuwatenganisha watoto wenye matatizo hayo ambao wanaishi mpaka leo. Ben hutumia masaa mengi kwa siku akifanya upasuaji wa “Mbongo” za watoto hasa wenye matatizo ya uvimbe kwenye ubongo. Bonyeza hapa kupata simulizi zake kwa ufupi. Mtandao wa Topblacks umetambua mchango wake unaoleta heshima kwa weusi wa nchi hiyo. Huyu bwana, pamoja na kuwa Daktari wa Tiba za Afya, ameandika vitabu kadhaa akijaribu kutoa wosia kwa vijana hasa wanafunzi wa shule namna ya kufanikiwa katika masomo. Anao pia mfuko wa kusomesha vijana wanaofanya vizuri. Huu