Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2009

Inaanza na wewe...

TUMEKUWA maarufu kwa kuwalaumu watu wa mabara mengine kwa umasikini wetu. Tunatumia muda mwingi kuorodhesha visingizio. Kwamba ni ukoloni ndio umeyatenda yote haya, huo ndio umekuwa wimbo wa kurithisha vizazi na vizazi. Sitetei wakoloni. Lakini hebu na tufikiri. Kama matatizo yetu yanauhusiano na ukoloni huo, mbona, miaka hamsini baada ya kile kinachoitwa uhuru, hali imebaki pale pale? Kama kweli umasikini wetu una harufu ya ukoloni, mbona leo hii, tunausomba ukwasi tulionao kuupeleka ughaibuni? Halafu baadae tunaufuata huko huko kwa jina la misaada ya hisani? Linaelezekaje hili? Miaka hamsini ya kujitawala, bado waafrika weusi hawataki lugha zao. Wanafundishana mambo ya hao wanaowalaani kwa lugha za hao hao! Wanaongea wao kwa wao kwa lugha za kuazima! Ndugu zangu, sababu ya umasikini wetu ni akili zetu.

Kupima UKIMWI kunasaidia?

Suala la kupima UKIMWI linasemwa sana. Tunaambiwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, kwa kupima. Inakuwa kama kujua afya yako ni jambo la maana sana. Ukiangalia athari za kujua afya yako kulinganisha na faida, utaona jinsi ambavyo tendo hilo la kupima halina msaada mkubwa kama inavyosikika. Kuishi maisha ya kutokuwa na hakika na uwapo wa wadudu hao mwilini, hakuwezi kukuathiri kama pale unapokuwa unajua ubomoaji wa seli unaendelea mwilini. Ni rahisi kuanza kuugua kabla ya wakati, kitu ambacho kisingekuwapo kama ungesingejua. Faida iko wapi? Kujua kwamba tayari unaumwa, kunakushawishi kujinyanyapaa mwenyewe, na kuanza kuhisi kufakufa, jambo ambalo haliwezi kuelezeka kama faida. Ni kama unapokunywa maji yasiyochemshwa bila taarifa. Huumwi tumbo. Suala la kupima kimsingi halina maana zaidi ya kukusanya takwimu za wagonjwa nchini. Maoni ya Daktari mwanafunzi, Muhimbili. Asante sana!

Tuzo za elimu zaja....

Picha
Si muda mrefu, tulijadili umuhimu wa kuwa na tuzo kwa maeneo mengine ambayo hayaonekani kupewa kipaumbele. Bofya hapa kujikumbusha. Binafsi simfahamu huyu bwana na wala sikumbuki jina lake japo alitambulishwa kwenye kipindi. Shirika nalo sikufanikiwa kulikumbuka. Kilichonishawishi kumbandika humu, ni mazungumzo yake niliyoyasikia leo asubuhi. Kwamba kuna mpango wa kuwa na tuzo za elimu kwa wanafunzi na walimu bora kwa kila mtihani wa taifa. Nadhani huu utakuwa mwanzo mzuri. Alikuwa akihojiwa asubuhi ya leo na mtangazaji Godwin Gondwe wa Kumekucha ITV.

Iko siku yote yatawezekana...

Ule mjadala wa kuifufua Jumuiya yetu ulisishia hewani. Bonyeza hapa kuusoma . Na si kwamba nimekata tamaa. Hata kidogo. Ila naamini kuna siku inakuja tutaweza. Kabisa. Kwa sasa itoshe nikidhani kuwa kipo kisichokuwepo.

Nenda hapa upate mwangaza...

Kissima ni mwanablogu mgeni. Ameanza kublogu mwaka huu. Nafurahi kwamba amekuwa mchangiaji mzuri katika blogu mbalimbali. Na inafurfahisha kwamba baadhi ya wanablogu wamekuwa mstari wa mbele kuchangia mijadala motomoto anayoianzisha bloguni kwake. Tafadhali bonyeza hapa kumtembelea, ukikumbuka kuchangia maoni katika mijadala yenye mwangaza.

Yuko wapi Ndesanjo Macha?

NIMEKUWA msomaji mzuri wa maandiko ya Ndesanjo . Kuna wakati nakumbuka nilikuwa nakesha kwenye mtandao kusoma makala zake motomoto. Nilikuwa 'naumwa' kumsoma. Huyu bwana ni msomi wa kweli kweli. Na lazima nikiri kwamba amekuwa changamoto kubwa katika ufahamu wangu, hasa katika masuala ya utamaduni wetu. Naandika kusikitika kwamba siku hizi amekuwa kimya. Haandiki tena Gumzo la Wiki kwenye Mwananchi, na zile makala zale za ripway zimepotea. Nauliza, wapi Ndesanjo Macha?