Kupima UKIMWI kunasaidia?

Suala la kupima UKIMWI linasemwa sana.

Tunaambiwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, kwa kupima.

Inakuwa kama kujua afya yako ni jambo la maana sana.


Ukiangalia athari za kujua afya yako kulinganisha na faida, utaona jinsi ambavyo tendo hilo la kupima halina msaada mkubwa kama inavyosikika.


Kuishi maisha ya kutokuwa na hakika na uwapo wa wadudu hao mwilini, hakuwezi kukuathiri kama pale unapokuwa unajua ubomoaji wa seli unaendelea mwilini. Ni rahisi kuanza kuugua kabla ya wakati, kitu ambacho
kisingekuwapo kama ungesingejua.
Faida iko wapi?

Kujua kwamba tayari unaumwa, kunakushawishi kujinyanyapaa mwenyewe, na kuanza kuhisi kufakufa, jambo ambalo haliwezi kuelezeka kama faida.

Ni kama unapokunywa maji yasiyochemshwa bila taarifa.
Huumwi tumbo.

Suala la kupima kimsingi halina maana zaidi ya kukusanya takwimu za wagonjwa nchini.

Maoni ya Daktari mwanafunzi, Muhimbili. Asante sana!

Maoni

 1. Asante kwa ujumbe huu. Lakini hata hivyo ni muhimu kupima sio UKIMWI tu ni muhimu kupima afya yako.

  JibuFuta
 2. Faida au hasara za kupima ukimwi inategemea na mtizamo wa mhusika ktk swala zima la kupima.

  Kupima kunaweza kumfanya mtu akaishi kwa matumaini kwani ataweza kutumia madawa ya kutuliza makali pamoja na kuzingatia maswala ya msosi.Hili linawezekana kama tu mhusika atakuwa na mtizamo chanya kuhusu swala hili.


  Kupima ukimwi pia kunaweza kuchangia ktk kupunguza maambukizo ya ukimwi.Mtu muungwana akijua kuwa ameathirika, hatajihusisha ataweka ahadi ya kutokusambaza lakini yule ambaye si muungwana ataamua kukomoa na kusema "ni bora tufe wengi" na akadhamiria kuusambaza. Kwa hiyo hasara au faida za kupima inategemea hasa na namna mtu atakavyolipokea swala hili la kupima Ukimwi.


  Labda niache changamoto hapa.

  Unafikiri ni kwa nini mtu anapokufa kwa Ukimwi mara nyingi kwenye historia fupi ya marehemu, kama alikufa kwa ukimwi huwa hawaliweki wazi hili.?

  JibuFuta
 3. ups sorry delete plz [url=http://duhum.com].[/url]

  JibuFuta
 4. ups sorry delete plz [url=http://duhum.com].[/url]

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Fumbo mfumbie mwerevu

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3