Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1
Kama tulivyoona katika makala yajuma lililopita, usaili ni hatua ya mwisho kuelekea kupata kazi. Sehemu kubwa
ya usaili ni maswali na majibu yanayolenga kupima uwezo wako wa kukabiliana na
changamoto halisi za kazi.
Ingawa yapo maswali yanayoweza
kukupa wasiwasi wa nia ya mwuulizaji, fahamu kuwa hakuna swali linaulizwa kwa
nia mbaya au kwa bahati mbaya. Kila swali linaloulizwa linalenga kutafuta
uthibitisho kuwa wewe ni mtu sahihi kwa kazi unayoomba.
Vijana wengi wenye ufaulu mzuri wanaoomba
kazi, hujikuta pasipokujua, wakifanya makosa madogo yanayowagharimu. Kwa kuwa
umetumia muda wako kuandika barua, kuandika wasifu wako wa kazi, wakati
mwingine kusafiri kwenda kuhudhuria usaili, ni muhimu kufanya maandalizi
yatakayokuongezea nafasi ya kufanikiwa.
Katika makala haya, tutaangazia
baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye usaili wa kazi na namna unavyoweza
kuyajibu.
Mapokezi
Unapokaribishwa kwenye usaili, jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa unatengeneza taswira ya mtu anayejitambua, mkomavu na mwenye nidhamu. Salimia jopo linalokupokea kwa tabasamu na salamu ya adabu yenye kuonesha kujiamini. Ikiwa ni lazima kushikana mikono na wanajopo, fanya hivyo kwa kujiamini.
Kisha, kuwa mtulivu uelekezwe mahali
pa kukaa. Hakuna sababu ya kuwa na papara kukaa mahali hata kama unahisi ndiyo
sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yako. Unapokaa, kaa mkao unaoashiria mtu
mnyenyekevu asiye na makuu. Mara nyingi kukaa wima ni vizuri na kuambatane na
hali inayoonesha kuwa unayo motisha ya kupata kazi unayoomba.
Kunja miguu yako kistaarabu, ukikutanisha
mikono yako juu ya mapaja kutuma ujumbe wa mtu mtulivu. Egemea mbele badala ya
nyuma, watazame wana jopo machoni. Kwa haraka, wazoee wana jopo kwa kuwaona ni
watu wa kawaida, lakini wanaostahili heshima.
Unapojibu maswali, epuka kutikisa
kichwa. Kukunja nne, kuegemea nyuma, au kuweka mikono kwa namna inayoonesha
mamlaka, ni kutuma ujumbe hasi usiokusudiwa.
Utambulisho
Kumbuka kuwa usaili wako ulianza
tangu jopo la usaili lilipopokea nyaraka zako. Kwa kiasi fulani, tayari wanayo
taswira fulani kukuhusu. Una kazi muhimu ya kuwathibitishia kuwa hayo
uliyoyaandika yana ukweli.
Mara nyingi unapokaribishwa kwenye
usaili, kiongozi wa jopo la usaili, atawatambulisha kwa wenzake. Anapofanya
hivyo, ana lengo la kukufanya uwazoee wanajopo, utulie na usiwe na wasiwasi.
Shukuru kwa utambulisho wao.
Kiongozi huyo anaweza kukutambulisha
wewe kwa jina lako na kukaribisha maswali. Mara nyingi swali linaloanza ni, ‘Tuambiwe
wewe ni nani?’ ‘Karibu ujitambulishe…’
Swali kama hili halihitaji utaje
majina yako bali kufahamu mhutasari wako kikazi. Ingawa utakayoyasema
yatatokana na uliyoyaandika kwenye wasifu wako wa kazi, mara nyingi hautarajiwi
kurudia maelezo hayo.
Jipambanue wajihi wako kikazi na
kiutendaji. Jopo linatarajia uwambie mambo ya msingi unayoyaamini yanayoweza
kuwasaidia kuelewa mtazamo wako kikazi. Ongelea majukumu ya kikazi uliyowahi
kuyafanya ukiyaonanisha na kazi unayoiomba. Anza na kazi ya nyuma zaidi
ukimalizia na kazi unayoifanya sasa hivi au ya hivi karibuni zaidi.
Ari na uwezo wako wa kazi
Unaweza kuulizwa, ‘Kwa nini unafikiri tukuchukue kwa nafasi hii?’, ‘Kwa
nini unataka kufanya kazi na sisi?’ Watu wengi wanapoulizwa swali hili hufikiri
wanachohitaji ni kujilinganisha na wengine kwa majina. Huna sababu ya kuwataja
wengine kama namna ya kuonesha unavyofaa zaidi.
Kwa swali kama hilo, kimsingi
wanataka kuona kama unaielewa taasisi yao. Thibitisha kuwa umeitafiti taasisi
kwa kina, na una uelewa wa huduma wanazotoa. Onesha unavyojisikia kuwa sehemu
ya malengo mapana ya taasisi yao.
Kadhalika, ni fursa kwako kuonesha
namna gani vipaji na ujuzi ulivyonavyo vinaweza kumsaidia mwajiri wako
mtarajiwa. Lijibu kwa ujasiri, bila kusita. Ukionesha wasiwasi katika majibu
yako, wanaokusaili nao watakuwa na wasiwasi na uwezo wao. Onesha namna gani
unafaa kuajiriwa kwa sababu ya uwezo wako.
Katika eneo la ari na uwezo wako wa
kazi, unaweza kuulizwa, ‘Unafikiri utaongeza tija gani katika taasisi yetu?’
Hapa ongelea ujuzi na uzoefu wa kazi
unaofikiri unaweza kumsaidia mwajiri wako kutatua changamoto alizonazo.
Jitahidi kuonesha namna ujuzi na vipaji ulivyonavyo vinavyoweza kutumika katika
maeneo mengine zaidi ya nafasi unayoomba. Kwa kawaida, mwajiri huvutiwa na mtu
anayeweza kutumika katika eneo zaidi ya moja.
‘Unaweza kuniambia mapungufu
uliyonayo?’ Usiwarahisishie kazi ya kuyaelewa mapungufu yako waziwazi. Waache
wao wenyewe wayajue. Badala yake zungumzia ‘mapungufu’ ambayo mtu akiyatafakari
anaona ni tija.
Mfano, ‘napenda kufanya kazi muda
mrefu’, ‘Nina tabia ya kufanya mambo kwa ukamilifu kiasi cha kujikuta sina muda
wa kutosha kukamilisha kazi kwa wakati ninaotaka’
Uzoefu wako huko ulikotoka
Unaweza kuulizwa maswali mengi kuhusu uzoefu wako kazini. Ikiwa kwenye wasifu wako wa kazi ulionesha kuwa uliwahi kufanya kazi mahali na ukaiacha, unaweza kuulizwa swali, ‘Kwa nini uliacha kazi yako?’ au ‘Kwa nini unataka kuacha kazi uliyonayo?’
Unaweza kuulizwa maswali mengi kuhusu uzoefu wako kazini. Ikiwa kwenye wasifu wako wa kazi ulionesha kuwa uliwahi kufanya kazi mahali na ukaiacha, unaweza kuulizwa swali, ‘Kwa nini uliacha kazi yako?’ au ‘Kwa nini unataka kuacha kazi uliyonayo?’
Hili ni swali gumu. Mwuulizaji
analenga kupima uaminifu wako na anataka kujua mambo gani hasa yanakuridhisha
kazini. Kimsingi lengo sio kujua yaliyofanyika huko uliko (kuwa) bali kujua
unavyoweza kumfaa. Hutakiwi kuzunguka kwa kutafuta sababu zisizo za kweli. Jibu
kwa urahisi na uwazi lakini ukiwa makini.
Inaendelea
Hutujenga Sana hizi dondoo kwa watafuta ajira
JibuFutaAsanteni manake mnatufanya tupunguze wasiwasi
JibuFutaAsanteeeni Sana tume elewa
JibuFutaVery nice post.
JibuFutaคาสิโนปอยเปต
คาสิโนปอยเปต
คาสิโนปอยเปต
Nice
JibuFutaJibu lini ulirizika katika kaz yk
JibuFutaMnatufanya tupunguze wasiwasi kwenye usahili
JibuFutaasante sana
JibuFuta