Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2016

Vitabu 49 Nilivyovisoma Mwaka 2016

Picha
Namshukuru Mungu nimeweza kusoma vitabu 49 kwa mwaka 2016. Nimejifunza mengi. Kusoma ni kama kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na watu wa kila namna ya uelewa ambao kwa hali ya kawaida usingeweza kuwasikia vijiweni.  Msisitizo wangu umekuwa kwenye vitabu vinavyochambua tabia katika maeneo mbalimbali ya maisha. Hata hivyo, vipo vichache vya masuala ya imani, falsafa na dini. Sijawa msomaji wa riwaya/novel. Nikutie moyo wewe mwenye ratiba ngumu kwa siku. Unaweza kufanya maamuzi ya kusoma ikiwa utaamua kuweka ratiba yako vizuri. Nijitolee mfano mimi mwenyewe.

Siri za Watu Wanaotekeleza Maazimio ya Mwaka Mpya

Picha
TULIJADILI baadhi ya sababu zinazofanya watu washindwe kutekeleza maazimio wanayoyaweka kila mwaka mpya unapoanza. Tuliona sababu kubwa tatu; kuweka maazimio kwa msisimko tu wa kuingia mwaka mpya usioenda sambamba na tafakari ya kina; kuweka malengo mapana mno yasiyopimika; na pale malengo yanapohusisha mabadiliko ya tabia, kutokujua uliko mzizi wa mabadiliko hayo.

Namna ya Kupunguza Changamoto za Wasichana wa Kazi

Picha
TUMETAJA mambo mawili yanayobadili mfumo wa malezi. Mosi, ni kubadilika kwa majukumu ya kijinsia yaliyozoeleka katika jamii. Mama anapoingia kwenye soko la ajira na kwenda kazini kama ilivyozoeleka kwa baba, changamoto inayojitokeza ni namna wanavyoweza kumlea mtoto wao katika muda wa kazi. Pili ni kufifia kwa utamaduni wa familia tandao unaozorotesha msaada wa kimalezi uliozoeleka kutoka kwa ndugu wa karibu. Mawili haya yanalazimisha familia za sasa kutafuta namna nyingine ya malezi kuwapa fursa wazazi kuendelea na kazi.

Kwa Nini Maazimio Mengi ya Mwisho wa Mwaka Huwa Hayatekelezeki?

Picha
Kila mwaka mpya unapoanza, ni kawaida kwa watu wengi kuweka maazimio fulani ya kutekeleza. Wapo ambao huazimia kubadili tabia wasizozipenda. Wengine huazimia kuanzisha mwenendo mpya wa maisha wanayoyatamani. Wengine hufikiria kutekeleza malengo fulani ya kijamii na kiuchumi yatakayobadili maisha yao kwa mwaka unaoanza. Ingawa ukweli ni kuwa mwaka unapoanza kinachobadilika huwa ni tarehe tu, watu huwa na imani kuwa wanaingia kwenye zama za maisha mapya. Imani hiyo huambatana na jitihada za kujaribu kubadili maisha yao yaendane na zama hizo mpya. Wanasema, ‘mwaka mpya na mambo mapya!’

Jifunze Namna Bora ya Kumzawadia Mwanao

Picha
Watoto wanapenda zawadi. Namna watoto wanavyochukulia zawadi inabadilika kulingana na umri. Katika umri mdogo, mtoto huchukulia zawadi kama haki ya kupata kila akipendacho kwa wakati wowote. Mzazi anaporudi nyumbani jioni, kwa mfano, watoto hutarajia pipi bila kufanya chochote. Lakini kadri mtoto anapoendelea kukua, mtazamo wa zawadi kama haki hupungua. Mtoto huanza kufikiria zawadi kama matokeo ya kufanya kile kinachotarajiwa na mzazi. Mtoto anapofaulu mtihani, mathalani, anatarajia kitu. Unapompa kile anachokitarajia, anajenga hamasa na motisha ya kutia bidii zaidi masomoni.  

Mbinu za Kutengeneza Mtandao wa Ajira

Picha
Changamoto kubwa inayowakabili vijana wanaotafuta kazi ni namna ya kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kupata kazi. Ingawa vipo vyanzo vingi vya kupata taarifa hizo, watafuta kazi wengi hutegemea matangazo rasmi ya ajira pekee kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo, tafiti za kazi na ajira zinaonyesha kuwa nafasi nyingi za kazi hasa katika sekta binafsi hazitangazwi hadharani. Waajiri wana tabia ya kutafuta mtu  anayeaminika kupitia vyanzo vinavyoaminika. Tafsiri yake ni kuwa kijana anayetegemea kupata taarifa za kazi kupitia matangazo rasmi, anapitwa na taarifa nyingi muhimu.

Jinsi ya Kumsaidia Mtoto Anayefanya Vibaya Shuleni

Picha
Si jambo la kufurahisha kwa mzazi unapoona mtoto hajafanya vizuri masomoni. Unapofahamu kuwa maendeleo ya mwanao si kama vile ulivyotarajia, ni rahisi kupatwa na simanzi, wasiwasi na hasira. Ni dhahiri mzazi unatamani mtoto awe na mustakabali mzuri kimaisha. Matumaini hayo yanakufanya uchukulie kushindwa kwake masomo kama kiashiria cha kuharibika kwa maisha yake ya baadae. Hakuna mzazi angependa mtoto awe na maisha yasiyoeleweka.

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 2

Picha
Katika makala yaliyopita tuliona maeneo manne muhimu ya kuzingatia unapoingia kwenye usaili. Kwamba pamoja na maswali mengine, unaweza kuulizwa maswali kuhusu uzoefu wako wa kikazi huko ulikotoka. Tuliona kuwa unapoulizwa maswali kama hayo, lengo ni kupima namna unavyoweza kuwa mkweli.