Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Udadisi

Changamoto za kuwanyima watoto kufurahia utoto wao

Picha
  Tunaishi kwenye dunia inayopitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya ya kijamii na kiuchumi, kwa kiasi kikubwa, yamezidisha matarajio tuliyonayo kwa maisha. Ukiacha matarajio mengi tuliyonayo kwetu binafsi, kuna matarajio mengi hata kwa wenzi wetu. Mke, kwa mfano, anatarajia mume awe kila kitu anachokifahamu kuhusu mwanamume. Mume ana kazi ya kuwa mcha Mungu, mtu wa sala, mtafutaji na mchapa kazi hodari, mcheshi, rafiki msikivu, kiongozi bora,     baba mzuri na mume mzuri asiyechelewa kurudi nyumbani. Matarajio haya makubwa yana faida zake lakini pia yana upande wa pili unaochanga migogoro mingi katika familia.   PICHA:  Wikimedia Commons   Hatuishii kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Tunazidisha pia matarajio kwa watoto wetu kiasi cha kuwanyima fursa ya kufurahia utoto wao. Hebu fikiria mtoto asiyeruhusiwa kufanya makosa. Kila analojaribu kufanya, anapodadisi mazingira yake,  anakuwa anatafsirika kama mtoto asiye na nidhamu na adabu kwa wa...

Thamani Yako Inategemea Namna Unavyowasaidia Wengine

Picha
PICHA: Lifehack KUNA ukweli kwamba katika harakati za kutafuta mafanikio, unahitaji kuwa na uhusiano mzuri na aina fulani ya watu. Hawa ni watu wanaokuzidi kile unachotaka kukifanya na kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa msaada kwako kwa kukupa mtaji wa kutekeleza wazo lako, kukunganisha na nafasi za ajira zisizotangazwa hadharani au kukusaidia mawazo yatakayokupeleka mbele kimaisha.

Mwalimu Anavyoweza Kukuza Udadisi kwa Wanafunzi

Picha
PICHA: OBrown & Associates Education Consulting Mara nyingi tumesikia watu wakilaumu mtalaa wetu kwamba unafunga fahamu za wanafunzi wetu. Wenye madai haya wanafikiri bila mtalaa kufanyiwa marekebisho makubwa, haiwezekani elimu yetu ikamnufaisha mwanafunzi. Hata hivyo, tulisema wiki iliyopita, kazi ya mtalaa ni kutoa diraya jumla ya aina ya raia wanaotarajiwa kufundwa kupitia mtalaa husika.