Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Masimulizi

Vitabu Nilivyosoma kwa Mwaka 2017!

Picha

Je, Shule za Bweni Zinafaa kwa Malezi ya Watoto Wadogo?

Picha
PICHA: SOS Schools Ongezeko kubwa la shule za bweni kwa watoto wadogo ni kiashiria kimoja wapo cha mabadiliko ya kijamii yanayoendelea kuathiri desturi za malezi. Pamoja na changamoto zake, mzazi anapofanya maamuzi ya kumpeleka mwanae shule ya bweni huamini anafanya hivyo kwa faida ya mtoto.

Chuki Unakuumiza Wewe Kuliko Unayemchukia

Picha
PICHA:  PM Notes MIAKA kadhaa iliyopita nilikosana na mtu ambaye awali tulikuwa karibu kikazi. Nilimwamini kama rafiki tuliyefanya kazi pamoja. Sikufikiri angeweza kujitafutia sifa binafsi kwa kunihujumu. Kilichoniumiza si tu kutendewa osa la makusudi, bali kuona mtu niliyemheshimu akijaribu kufikia malengo yake kwa kujaribu kuniharibia kazi yangu.

Kwa nini Wazazi Huwapeleka Watoto Wadogo Shule za Bweni?

Picha
PICHA: The Citizen Miaka kadhaa iliyopita, wakati huo nikiwa mwanafunzi, nilishangazwa kusikia mtoto wa ndugu yangu, wakati huo akiwa na miaka sita, alikuwa anasoma shule ya bweni. Sikufikiri jambo hilo lingewezekana.                                                                                     Nakumbuka mara yangu ya kwanza kwenda shule ya bweni nilikuwa na umri wa miaka 17 nikisoma kidato cha 5. Kwa kuwa haikuwa rahisi kwangu kuzoea maisha ya mbali na nyumbani, nilishindwa kuelewa inawezekanaje mzazi kumpeleka mtoto mdogo kiasi hicho kwenda shule ya bweni.

Upendeleo wa Wazazi Unavyoweza Kuchochea Uadui kwa Watoto

Picha
PICHA: Aim Lower Journal KUNA kisa kimoja kwenye biblia kinachoweza kutufundisha jambo muhimu kama wazazi. Kisa chenyewe ni kile cha Yusufu, mtoto wa mzee Yakobo, aliyejikuta kwenye mtafaruku mkubwa  na ndugu zake. Ugomvi wa Yusufu na kaka zake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kaka zake waliazimia kwa pamoja kumwuuza Misri kama adhabu. Jambo la kuzingatia ni kwamba ugomvi huu wa Yusufu na ndugu zake haukutokea kwa bahati mbaya. Chanzo cha yote hayo ni upendeleo.

Tabia Saba Zitakazokuwezesha Kutekeleza Malengo Unayojiwekea

Picha
KUANZA kwa mwaka mpya kunaambatana na matarajio mengi. Tunapoingia mwaka mpya tunamani kubadili maeneo mengi katika maisha yetu. Tunatamani kuwa na maisha bora yenye tija kiuchumi, kijamii, kiimani na kwenye maeneo mengine. Hata hivyo, katika kutekeleza malengo yako, ni dhahiri kuwa zipo baadhi ya tabia ulizonazo zinazoweza kuwa kikwazo katika kutekeleza malengo ya mwaka huu. Unahitaji kubadili tabia ili uweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza malengo yako.

Mwaka Mmoja Bila Mama, Mkono wa Mungu Haujatuacha…

Picha
Nakumbuka mwezi Juni 2002, nikiwa mwanafunzi wa sekondari, eneo ni stesheni ya gari moshi (treni) mjini Singida nikiwa ninarudi nyumbani nikitokea Dodoma. Ilikuwa ni safari ya kuunga unga iliyoanzia Dar es Salaam kupitia Dodoma na kisha Singida. Wakati huo tulikuwa tunaondoka Dodoma saa nne asubuhi, Singida tunafika saa za jioni kuanzia saa kumi na moja hivi tukiwa taabani kwa uchovu wa kukaa kwenye mabehewa yaliyoonekana kuhangaika mno kupita kwenye mataruma katikati ya vichaka ya Dodoma na Singida. Jioni hiyo ninayoikumbuka vyema tulichelewa kidogo na hatimaye tulifika Singida stesheni saa kumi na mbili unusu hivi za jioni.

Nilichojifunza Katika Miaka 10 ya Kublogu

Picha
Kwa mara ya kwanza nililisikia neno blogu mwaka 2004. Wakati huo nilikuwa msomaji wa dhati wa safu ya ‘Gumzo la Wiki’ iliyokuwa ikiandikwa na Ndesanjo Macha katika gazeti la Mwananchi. Kwa kufuatilia anuani iliyokuwa ikihitimisha safu hiyo, niligundua kuwa sikuhitaji kusubiri   Jumapili kuweza kulisoma ‘Gumzo’. Anuani hiyo ilikuwa ni ya blogu ya kwanza ya Kiswahili ikiitwa Jikomboe .

Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Wakati wa Majanga ya Kitaifa?

Picha
  "TWITI TENA kama unadhani PNoy alipaswa kuhudhuria mapokezi ya heshima badala ya tukio la Kiwanda cha Magari. #NasaanAngPangulo" alitwiti @BobOngWords. Alama habari #NasaanAngPangulo, yenye maana 'Rais yuko wapi' katika lugha ya Kitagalog, ilikuwa mada maarufu zaidi kwenye mtandao wa Twita duniani wakati Wafilipino walipokuwa wakionesha hasira zao kwa Rais Noynoy Aquino kufuatia  kukosekana kwake  kwenye mapokezi ya heshima ya miili ya polisi waliouawa wakiwa kwenye operesheni maalum.

Kwa nini ni rahisi kumsifia mtu akifa kuliko akiwa hai?

Picha
Hatupendi kuwasifu wengine wala kusikia wakisifiwa na wengine, lakini ni wepesi sana kumsifia marehemu. Na ni nadra kusikia tabia ya marehemu ikikosolewa. Hata waliokuwa hawamsifii akiwa hai, huomba fursa ya kuusemea vizuri wasifu wa mpendwa aliyetutoka. Mtu fulani maarufu akifa, kwa mfano, watu ambao hata siku moja hawakuwahi kumsema marehemu enzi za uhai wake, ndio huanza kushindana kutundika picha zake zikiambatana na maneno ya ‘apumzike kwa amani’. Sasa swali, kwa nini ni vyepesi kumsifia marehemu asiyesikia kuliko kumsifia binadamu anayesikia?

"Ningerudia ujana tena, kipaumbele changu kingekuwa familia!"

Picha
Re-living my life ? " anauliza halafu anajijibu mwenyewe, "Ningebadili mtazamo wa tafsiri ya mafanikio. Mafanikio yangemaanisha ubora wa mahusiano yangu na familia yangu. Hivyo, ningewajibika zaidi kujenga na kuilea familia yangu kwa karibu. Ningetumia muda mwingi na wanangu na mke wangu. Ningepunguza ukali usio  na sababu kwa mke wangu na wanangu. Ningewafanya wanangu wajisikie kuwa na baba anayewaelewa na anayejua mahitaji yao. Ningepatikana zaidi. Ningemfanya mke wangu ajione ni kipaumbele cha maisha yangu.

Makundi Makuu Matano ya Waislamu

Mchekeshaji mwenye asili ya Pakistani, Sami Shah, anachambua makundi makuu matano ya wa-Islam.  Pengine hujawahi kuyasikia kama mimi na ungependa kujua umeangukia kundi lipi. Bonyeza hapa kusoma makala hiyo , ambayo kimsingi imekusudiwa kukufanya ucheke na kufurahi wakati huo huo, ukitafakari kwa kina kile hasa kinachokuchekesha.

Kushinda Vikwazo vya Jitihada za Kumpa Mwenzi Anachostahili

Picha
KUYAELEWA mahitaji ya kihisia ya mwanamke ni suala moja, lakini kuuishi uelewa huo ni jambo jingine kabisa. Yapo mambo mengi tunayoyafahamu na tunajua kuyaelewa lakini hatuyaishi. Tujua kwa kina lakini hakuna tunalolitenda. Matokeo yake tunatenda tusiyoyajua na tunayoyajua hayatusaidii kubadili maisha yetu. Katika makala haya, ningependa kusimulia changamoto nilizokumbana nazo katika kupambana na utamaduni niliokulia wa kupuuza mahitaji ya msingi ya mwanamke.

Nilichojifunza katika maonyesho ya tatu ya wanasayansi chipukizi wiki hii

Picha
MAONYESHO ya wanasayansi chipukizi yaliyoandaliwa na T aasisi ya Young Scientists Tanzania yamefikia hatma yake wiki hii. Maonyesho haya ya siku mbili, yaliyofanyika kati ya tarehe 13 na 14 Agosti katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam, yameacha mafunzo makubwa kadhaa. Kwanza, yameweza kufanya ieleweke vizuri zaidi kwamba wanafunzi wanayo hamasa kubwa ya kufanya sayansi ikiwa watawezeshwa, kinyume kabisa na madai ya mara kwa mara kwamba sayansi haipendwi na wala haifanyiki mashuleni. Washindi wa kwanza wakikabidhiwa zawadi na Dk Bilal. Picha: @bwaya Katika muda wa siku mbili hizi, nimeshuhudia namna bongo za wanafunzi wa shule za sekondari, tena nyingi zikiwa zile za kata, zinavyochemka katika kujaribu kutatua changamoto zinazowakabili. Inasisimua kuwaona wanafunzi wakijaribu kutafuta mbinu za kupambana na vyanzo vya magonjwa, uharibifu wa mazingira na kutatua changamoto zinazowakabili watu wetu katika kujiletea maelendeleo kwa ujumla. Hilo limekuwa wazi kupitia maonyes...

Wanafunzi waonyesha namna teknolojia rahisi inavyoweza kurahisisha upigaji kura bila kufika kituoni

Picha
NIMEFIKA hapa Diamond Jubilee kama mwananchi anayetamani kujionea hamasa waliyonayo wanasayansi chipukizi kuonyesha kazi zao nzuri. Ni maonyesho ya tatu ya Sayansi katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambayo hatimaye hapo kesho yatawaibua wanafunzi wawili kama washindi wa tatu wa shindano la wanasayansi chipukizi hapa nchini linaloandaliwa na Young Scientists Tanzania. Baadhi ya washiriki kwenye ufunguzi wa maonyesho leo. Picha: @bwaya Kwa hakika hamasa ni kubwa. Wanafunzi wamejawa na msisimko wa aina yake kuonyesha matokeo ya tafiti zao walizozifanya tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Wamejawa na matumaini, hasa kwa sababu ya maneno ya ufunguzi yaliyosemwa na Mkurugenzi wa YST, Dk Kamugisha wakati akiwakaribisha asubuhi ya leo. "Tulipata maombi ya kushiriki kutoka shule zaidi ya 200...lakini ni maombi 100 pekee yalifanikiwa kupenya katika mchujo. Mpaka hapo ninyi ni washindi. Kilicho muhimu zaidi, ni kwamba pamoja na kwamba kazi zenu zitapitiwa na watu wanaoelewa vyema zaidi maene...

Blogu inavyosaidia kujiona unavyokua na kubadilika

Nilianza kublogu mwaka 2005. Takribani miaka tisa. Wakati huo nilikuwa kinda. Kijana mdogo. Blogu kwangu ilikuwa kama sehemu ya kusema ninayofikiri bila kuhofu. Nimekuwa na utaratibu wa kurudia niliyowahi kuyaandika enzi hizo. Wakati mwingine ninacheka. Ninaweza kuona namna mtazamo wangu ulivyokuwa ukibadilika hatua kwa hatua hasa katika masuala ya dini na imani. Watu hutarajia mwandishi asibadilike. Maana kwao, mwandishi ni mlishaji. Hajifunzi. Mimi si mwandishi. Ni mwanablogu. Tofauti ya mwandishi na mwanablogu ni kwamba, wa pili anaingiliana sana na hao anaowaandikia. Anajifunza. Anabadilika. Mtazamo unabadilika. Wa kwanza sina hakika na yote hayo. Kwa hiyo, ninafurahia kubadilika. Zamani nilikuwa mbishi. Niliona raha kusumbuana na wabishi wenzangu. Siku hizi sibishani sana. Ninasikiliza zaidi. Zamani nilikuwa mwongeaji. Siku hizi nimekuwa na aibu. Nina haya. Yote hayo ni mabadiliko. Yawe chanya ama hasi. Lakini bado ni mabadiliko. Kufikia miaka ya 2010 hapa kumefumuka mitan...

Kurudi Bloguni

Habari za miaka wapenzi wana-blogu. Tafadhali karibuni sana kwenye blogu yetu iliyokuwa mapumzikoni kwa takribani miaka miwili. Sababu za kupotea zilikuwa za kijamii na nje kabisa ya udhibiti wa kawaida. Sasa tunaweza kuahidi kuwa blogu yetu imerejea rasmi kwa nguvu mpya na mtazamo mpya tangu dakika hii. Na masuala ya kijamii yanayohusiana na mahusiano yetu na nafsi zatu pamoja na mahusiano yetu na wanaotuzunguka, tabia zetu, mitazamo yetu, na kadhalika, yataendelea kupewa kipaumbele kwa sura mpya zaidi. Karibuni sana.

Unaionaje Dublin kupitia jicho langu?

Picha
Leo nimepata bahati ya kutembea kidogo katika jiji la Dublin. Gari linalotumika kumwezesha mgeni kusafisha macho. Picha: @bwaya         Majengo ya zamani yanayovutia. Picha: @bwaya Mitaa yenye majengo yanayoitwa ya 'King George' wa Uingereza. Ireland ilikuwa koloni kwa miaka mingi. Picha: @bwaya Mto katikati ya Dublin. Picha: @bwaya Mavazi ya wa-Irish Picha: @bwaya Magogoni ya Ireland. Picha: @bwaya

Kupanda na kushuka kwa dini nchini Ireland

Picha
Nimebahatika kutembelea Chuo Kikuu cha Taifa Maynooth, Dublin Ireland. Ni chuo cha zamani sana tangu enzi hizo kikiwaandaa makasisi, kikiitwa St Patrick College. Maynooth University, Ireland. Picha: Jielewe Jambo la ajabu, nimeona picha zinazoeleza idadi ya wanafunzi waliokuwa wanajiunga kuchukua masomo hayo ya Upadre kila mwaka. Idadi inaonekana kupungua kila mwaka, mpaka walipoamua kukigeuza kuwa Chuo Kikuu kifundishe mambo mengine. Madhari ya Maynooth, Dublin. Picha: Jielewe Kwa ujumla, msisimko wa dini haupo nchini humu. Makanisa mengi ya Kikatoliki yamefungwa au kugeuzwa matumizi kusaidia shughuli nyingine. Kanisa maarufu nikiwa jengo la makumbusho. Picha: Jielewe 'Nikiwa hapa, ndiyo kwanza kashfa za makasisi kudhalilisha watoto zinapamba moto. Mambo yamebadilika. Sanamu ya Papa John Paul II alipotembelea hapa. Picha: Jielewe Dublin, mji mkuu wa Ireland ndiko yaliko makazi ya makampuni makubwa ya teknolojia. Ndiko waliko Yahoo! Na makampuni meng...

Guiness: Alama ya Taifa la Ireland

Picha
Kiwanda kinacholinda heshima ya walevi, Dublin, Ireland. Picha: Jielewe Katika bidhaa wanayojivunia wa-Irish, ni pombe maarufu ya Guiness. Ukikatiza mitaa saa za usiku baada ya kazi, wanywaji (najua ni kosa kubwa kuwaita walevi) hawanywi pombe nyinine zaidi ya Guiness. Kila baa ni Guiness. Nawambia mwenyeji wangu sinywi pombe, wananishangaa. 'Utarudije kwenu hujanywa Guiness?' Alama ya Guiness ni nembo ya Taifa. Pombe ni urithi wa taifa. Picha: Jielewe Kitu kingine ambacho nimekigundua, kumbe ile nembo ya Guiness unayoiona, ndiyo nembo ya Taifa. Kwa maana nyingine, wakati sisi urithi wetu ni Ngorongoro na mbuga za wanyama, hawa jamaa, urithi wao ni pombe. Pombe ni urithi wa taifa. Natania. Mtaani kweli imepangwa. Hongereni. Nimekumbuka kwetu. Sisi ni wazalishaji wakubwa wa bangi na mirungi tena kwa wingi sana ingawa kwa siri. Wa-Irish ni wazalishaji wakubwa wa Pombe. Sote letu moja. Unalijua?