Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Kuanzisha na Kuimarisha Urafiki wa Karibu

Picha
Katika zama hizi za maendeleo ya kidijitali, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki. Unaweza, kwa mfano, kuwa na ‘marafiki’ elfu tano kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja katika maisha halisi. Marafiki wa kweli na wa karibu ni moja wapo ya mahitaji muhimu katika maisha. Tunaweza kuwa na sababu nyingi kuhalalisha kwa nini hatuna (haja na) marafiki wa karibu.  Hata hivyo, zipo nyakati  hufika tukajikuta katika maisha yenye kujaa upweke  na msongo wa mawazo kwa sababu hatukutumia muda wetu kutengeneza urafiki wa karibu na watu tunaofahamiana nao.

Kujenga Tabia ya Kusoma kwa Watoto Wadogo

Picha
Kusoma si tabia nyepesi kuijenga katika mazingira ambayo masimulizi na mazungumzo ni vyanzo vikuu vya maarifa kuliko maandishi.   Tumelelewa katika utamaduni usiosisitiza sana umuhimu wa kusoma. Lakini, hata hivyo, hatuwezi kukwepa kusoma katika ulimwengu huu unaotulazimisha kuyasaka maarifa kwa njia ya maandishi.

Umuhimu wa Kujenga Tabia ya Kujitolea

Picha
Kujitolea ni kutoa sehemu ya muda wako, ujuzi na maarifa uliyonayo na wakati mwingine nguvu zako kufanya kazi ya watu wengine bila kupata malipo ya moja kwa moja. Kazi unayoifanya kwa kujitolea mara nyingi ungeweza kuifanya kwa kudai ujira lakini unaamua kuifanya bure.  Mathalani, mwajiriwa anayetamani kuleta mabadiliko nje ya ajira yake, anapotumia ujuzi wake kufanya kazi za jamii bila kudai malipo, anakuwa amejitolea. Tuangalie kwa mhutasari kwa nini ni muhimu kujenga tabia ya kujitolea.

Kipimo cha Kujitambua ni Tunavyowatendea Tusiowajua, Wasioheshimika

Picha
Mjema anaandika ripoti inayohitajiwa na mkuu wake wa kazi. Wakati muda wa kukabidhi ripoti hiyo ukikaribia, anapigiwa simu na mtu asiyemfahamu. Mjema hajui ni nani hasa anayemtafuta muda huo hivyo anaamua kupokea simu. Bahati mbaya aliyempigia simu hasikiki vyema. Mjema anahisi labda ni tatizo la mtandao, anaamua kuikata mara moja.

Kujitambua ni Kushinda Ubinafsi, Kujali Mahitaji ya Wengine?

Picha
Tulianza kudodosa suala la kujielewa katika makala yaliyopita . Kama tulivyodokeza, kujielewa kunakwenda sambamba na kuelewa msukumo ulio nyuma ya yale tuyatendayo kila siku. Katika sehemu hii, tutaangalia kwa ufupi kwa nini kujitambua ni zaidi ya ule ‘ubinafsi’ unaoishi ndani yetu.

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Picha
Ingawa ni kweli tunazaliwa na sehemu ya tabia tulizonazo, upo ukweli wa kiutafiti unaothibitisha kwamba mazingira ya kimalezi yana nafasi kubwa katika kujenga tabia za mtu. Ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili, mathalani, unatawaliwa zaidi na uasili ambao kwa kiasi kubwa hatuna mamlaka nao. Hata hivyo, ukuaji wa kihisia na kimahusiano unatawaliwa zaidi na mazingira ya kimalezi ambayo tayari tuliyaona kwenye makala iliyopita .

Tuyafanyayo ni Matokeo ya Tujionavyo

Picha
Ungeulizwa swali, ‘wewe ni nani’ ungejibuje? Wengi tungetaja majina yetu kwa kuamini ‘sisi’ ni majina yetu. Wengine tungetaja kazi zetu kwa sababu kwetu majukumu ndio utambulisho wetu. Sisi ni nani basi? Kwa hakika swali hili si jepesi lakini linatuwezesha kuelewa tabia zetu. Karibu kila tunachofanya ni matokeo ya vile tujionavyo. Katika makala haya, tutaangazia  mitazamo michache inayoweza kutusaidia kutafakari swali hilo. 

Mazingira Manne ya Kimalezi Yanayotengeneza Tabia za Watoto

Picha
Watafiti wa makuzi na malezi wanasema mtoto anahitaji mazingira yanayomchangamsha kihisia, kiakili, kimwili na kimahusiano. Anapochangamshwa vyema, tunaambiwa, mtoto hujisikia utulivu wa moyo unaomfanya awe karibu na wazazi na watu wengine wanaomzunguka. Anapokosa kuchangamshwa, mtoto hujenga uduwavu unaojenga tabia za kujilinda na uchungu wa kujiona anapuuzwa. Katika makala haya, tunaangazia mambo manne yanayoweza kumchangamsha mtoto kihisia na kimahusiano na hivyo kutengeneza tabia na mitazamo yake.

Kuanza Kupotea kwa Desturi ya Ukaribu wa Kifamilia Kunavyoathiri Malezi

Picha
Malezi katika mazingira yetu ya ki-Afrika ni suala nyeti. Kwa kutambua umuhimu wa malezi katika kujenga jamii yenye ustawi, wa-Afrika tumekuwa na desturi ya kuelekeza nguvu zetu nyingi katika malezi ya wanetu. Kwa mfano, tangu mtoto anazaliwa, ilikuwa ni lazima alale kitanda kimoja na wazazi wake kwa muda unaozidi miaka miwili. Mtoto mchanga hakuachwa alale kwenye kitanda chake mapema kwa sababu za msingi zilizokubalika katika jamii zetu.