Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mahusiano Kazini

Unataka Kumjua Rafiki Atakayekusaliti? Soma hapa

Picha
PICHA: Recycle Coach Katika nyakati kama hizi za Pasaka, mara nyingi, tunasikia marehemu Yuda Iskariote akijadiliwa kama jitu ovu lisilo na maadili lililokuwa tayari kumsaliti Bwana wetu Yesu Kristo. Binafsi naamini, pamoja na ubaya wake, usaliti wa Yuda ulikuwa muhimu katika kuwezesha mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Wakati mwingine Mungu hutumia mabaya kuwezesha mazuri. Hata hivyo, kwa maoni yangu, Yuda hakuwa na nia mbaya kivile. Kwanza, alikaa na Yesu kwa muda wa kutosha na hivyo alifahamu Yesu hakuwa mtu wa hivi hivi anayeweza kuchezewa kienyeji. Yesu alifanya miujiza mingi na Yuda alishuhudia. Yesu alitembea juu ya maji. Yesu alifufua wafu. Si mara moja. Tena kuna wakati Yesu alimfufua mtu aliyekuwa kazikwa siku tatu. Unamkumbuka Lazaro. Aidha, kuna nyakati washikadini na wanafiki walitaka kumshughulikia Yesu, wakashindwa kwa sababu Yesu aliwaponyoka. Yuda aliyafahamu yote haya. Kama baadhi yetu tunavyofanya leo, Yuda aliutazama uwezo huu wa Yesu k...

Hatua Tano za Kuandaa Wasifu Utakaokupa Ajira

Picha
Moja wapo ya sababu zinazochangia watu kukosa ajira wanazoomba ni uwezo mdogo wa kujenga wasifu wao katika maandishi.   Wasifu ni maelezo binafsi yanayolenga kumshawishi afisa mwajiri kuwa unazo sifa za kutosha kupata ajira unayoomba. Vyuo vyetu, kwa bahati mbaya, haviweki msisitizo katika ‘mambo madogo’ kama haya. Matokeo yake watu wengi wazuri wenye ujuzi wanashindwa kuonekana kwa waajiri.

Mbinu za Kukabiliana na Sonona, Hofu Mahali pa Kazi

Picha
Tuchukulie unafanya kazi muhimu inayotakiwa ndani ya masaa mawili yajayo. Wakati ukikimbizana kumalizia kazi hiyo, umeme unakatika. Ofisi haina jenerata na huwezi kutumia kompyuta bila umeme. Unajawa na wasiwasi lakini huna cha kufanya.

Mambo ya Kutafakari Unapoanzisha Uhusiano wa Kimapenzi Kazini

Picha
PICHA: Shalinii Choudhary   Sehemu kubwa ya maisha yako kama mfanyakazi unaitumia kwenye eneo la kazi. Ingawa inategemea na aina ya kazi unayoifanya, ni wazi muda mrefu kwa siku unaoutumia kutekeleza majukumu yako unakuweka karibu zaidi na wafanyakazi wenzako kuliko hata familia na marafiki. Mazingira haya ya ukaribu wa kikazi, wakati mwingine, yanatengeneza uwezekano wa uhusiano wa kimapenzi baina ya wafanyakazi.

Mazingira Yanayoweza Kuanzisha Mapenzi Yasiyotarajiwa Kazini

Picha
Dorcas, msichana wa miaka 30 anayefanya kazi kama Afisa Mikopo kwenye benki moja mjini, hakuwahi kufikiri ingetokea siku moja ‘achepuke’ kimapenzi na Johnson ambaye ni mfanyakazi mwenzake. Miaka mitatu iliyopita wakati anaanza kazi kwenye benki hiyo, Dorcas alikuwa na msimamo thabiti na aliheshimu ndoa yake.

Hatua za Kuchukua Unapojisikia Kuchoka Kazi

Picha
Kutokuridhika na kazi ni hali ya kujisikia hufikii matarajio yako kikazi. Matarajio yanaweza kuwa kiwango cha mshahara, kujisikia unafanya kazi ndogo kuliko uwezo ulionao, kazi kutokuendana na vipaji ulivyonavyo au hata kutokupata heshima uliyoitarajia.

Ukitaka Kuaminiwa Jenga Mazingira ya Kuaminika

Picha
PICHA:  PsyBlog “Nina mke asiyeniamini kabisa,” aliniambia bwana mmoja hivi majuzi. “Hana imani kabisa na mimi.  Juzi kati hapa nimemkuta anachunguza simu yangu. Tuligombana sana.” Nilimwuliza kwa nini anafikiri mke wake hamwamini. “Basi tu ndivyo alivyo. Hata ufanyaje hana imani.”

Hakuna Ulazima wa Kushinda Kila Majadiliano

Picha
PICHA: Elly Prior Chukulia mnajadiliana jambo na rafiki yako. Inaweza ikawa ni mtandaoni, nyumbani, ofisini au mahali kwingineko. Katika mazungumzo yenu unabaini hamuelewani. Kile unachoona ni sahihi, sivyo anavyoona mwenzako. Kila mmoja wenu anajaribu kutetea upande wake kuliko anavyoelewa mtazamo wa mwenzake. Unadhani kipi ni sahihi kufanya katika mazingira hayo? Je, ni busara kuendelea kuthibitisha ulivyo sahihi hata kama ni dhahiri mwenzako hayuko tayari kukuelewa? Unajisikiaje mwenzako akikuonesha haukuwa sahihi? Mara nyingi tunafikiri kushindwa na kutokuwa sahihi ni udhaifu. Tunapambana na wasiotuelewa kwa mabishano na majibizana kwa lengo tu la kuonesha tulivyo kwenye upande sahihi. Unazungumza ili kushinda? Nakumbuka siku moja nilishiriki mjadala mmoja kwenye mitandao ya kijamii. Katika mjadala huo, kulikuwepo na pande mbili zinazotofautiana kimtazamo. Kadri mjadala ulivyoendelea, niligundua hapakuwa na jitihada za pande mbili hizo kuelewana. Kila upande...

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Picha
Ufanisi kazini, kwa kiasi kikubwa, unategemea uwezo alionao kiongozi. Huyu ni mtu mwenye mamlaka yanayompa sauti ya kuhamasisha watu kujiwekea dira na utaratibu wa kuifikia dira hiyo. Kiongozi anatambulishwa na uwezo wake wa kuwavuta na kuwashawishi watu makini kutumia vipawa , ujuzi na uzoefu walionao katika kuwezesha kufikia malengo mapana ya kampuni, taasisi au kikundi husika.

Utaratibu wa Kufuata Unapoachishwa Kazi

Picha
Sheria ya ajira na mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inaainisha mazingira kadhaa yanayoweza kusababisha mwajiriwa aachishwe kazi na mwajiri. Kwanza, kama mwajiri amefuata masharti ya mkataba yanayohusiana na utaratibu wa kumwachisha kazi. Kufuata masharti ya mkataba kunategemea kama aina ya mkataba. Pale ambapo mkataba ni wa kudumu, mwajiri lazima awe na sababu halali za kuchukua hatua za kusitisha mkataba kwa kufuata utaratibu.

Fahamu Namna Ajira Inavyoweza Kukoma kwa Mujibu wa Sheria

Picha
Ufanisi wa ajira unategemea uhusiano mzuri uliopo kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mwajiri, kwa kawaida, huweka mazingira mazuri kumwezesha mwajiriwa kutekeleza kazi zake. Mwajiriwa naye, kwa upande wake, hutumia ujuzi na uzoefu alionao kufanya majukumu aliyokabidhiwa na mwajiri.

Unajengaje Uhusiano Mzuri na Viongozi Kazini?

Picha
Moja ya mambo yanayoweza kukusaidia kufanikiwa kazini ni namna unavyohusiana na mkubwa wako wa kazi. Huyu ni mtu anayekuongoza, anayetoa maelekezo ya nini kifanyike na wakati mwingine ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye taasisi, idara au ofisi unayofanya kazi. Kwa nafasi yake, kiongozi wa kazi ni mtu mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi yanayohusu kazi yako hata kama anaweza asiwe mwajiri wako moja kwa moja. Huyu ni mkuu wa ofisi, idara, kitengo, kampuni au taasisi unayofanyia kazi. Ndiye mtu anayekusimamia na kupokea taarifa za utendaji wako na labda kuzipeleka kwenye mamlaka za juu.

Hatua za Kuchukua Unapoamua Kuacha Kazi -1

Picha
Kuacha kazi si jambo dogo. Lakini zipo sababu kadhaa zinazoweza kukufanya uamue kuacha kazi. Mosi, kupata kazi mpya. Unapoitwa kuanza rasmi kazi uliyoomba, ni vigumu kuendelea na kazi uliyonayo. Kwa kuwa ni vigumu kuwa na ajira mbili kwa wakati moja, mara nyingi utalazimika kuacha kazi uliyonayo. Pia inawezekana umeshindwa kuendelea na kazi uliyonayo hivi sasa. Ingawa haishauriwi kuacha kazi bila kuwa na uhakiki wa kazi nyingine, hutokea mtu akafikiri kwa kina, akapata ushauri wa kitaalam na kujiridhisha kuwa ugumu wa mazingira ya kazi haumruhusu kuendelea na kazi aliyonayo.