Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Duru za Siasa

Tabora wamemsamehe Lowassa, au ni dalili za kukubalika kwa UKAWA?

Picha
Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa makala haya katika mitaa ya mji wa Tabora jioni ya leo, umeonesha kwamba kuna ushindani mkali kati ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Wilbroad Slaa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 10 – 12:30 jioni hii. Matokeo hayo yanaonesha kwamba Lowassa ana asilimia 28 na Dk Wilbroad Slaa angepata asilimia 22.

CCM ni maarufu Kigoma kwa 40.2%, ikifuatiwa na CHADEMA kwa 27.2%

Picha
Utafiti huru uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umeonesha kwamba mgombea yeyote wa nafasi ya Urais wa Chama cha Mapinduzi angeweza kuchaguliwa na wapiga kura wa Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa asilimia 40.2% ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu jioni ya leo.

[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV

Picha
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu. Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali. Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014. Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Hotuba ya Mhe Kikwete akizungumza na wa-Tanzania waishio Washington DC

Picha
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani. Kwa hisani ya Mubelwa Bandio.

Rais mteule atumia mitandao ya kijamii kuwaomba raia kumchagulia Baraza la Mawaziri

KATIKA kuthibitisha kwamba kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni kubwa, hivi majuzi, Rais mpya wa Indonesia Mhe Joko Widodo (maarufu kama Jokowi) amewaomba watumiaji wa mtandao wa Facebook kumsaidia kuteua baraza lake la mawaziri kwa kupendekeza majina ya watu wanaoweza kushika wadhifa wa kuwa Mawaziri. Hatua hiyo, ni mwendelezo wa kile anachokiita mwenyewe 'kuongeza  kwa ari ya kujitolea' miongoni mwa raia wa nchi hiyo, baada ya watu wengi kujitolea kumsaidia katika harakati zake za kuingia ikulu. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jokowo ametoa orodha ya nafasi 34 za Uwaziri , zenye majina matatu yanayopendekezwa kwa kila nafasi, huku kukiwa na nafasi ya nne wazi kwa wananchi kupendekeza wanayemtaka. Widodo anataapishwa ifikapo Oktoba 20, 2014 kuwa Rais. Joko Widodo (53) Gavana wa zamani wa Jakarta, amechaguliwa kuwa Rais wa Indonesia baada ya kumbwaga mpinzani wake Prabowo Subianto kwa asilimia 53 ya kura milioni 130 zilizopigwa tarahe 9 Julai, 2014. Kama ilivyo ...

Wakubwa wetu huko Ufaransa

Picha
Picha hii imechukuliwa kwenye ukumbi wa mijadala wa Jamii Forums ikiwaonyesha watawala wetu walipohudhuria mkutano huko Ufaransa.

Shule zisizo na elimu zifungwe!?

Picha
Ivan D. Illich ni mwanafalsafa aliyezaliwa mjini Vienna mwaka 1926. Katika kitabu chake cha Deschooling Society, Illich anazishambulia taasisi ziinazohodhi wajibu wa kuelimisha jamii. Anasema; “…kwenda shule (tofauti na kuelimika) imekuwa ndio utaratibu wa maisha…shule zimeshindwa kukutana na mahitaji ya mtu mmoja moja, na mbaya zaidi zinaendeleza uongo ule ule kwamba yale yanayoitwa maendeleo yanayotokana na uzalishaji, utumiaji na faida ndicho kipimo cha ubora wa maisha ya mwanadamu. “…Vyuo Vikuu (shule) vimegeuka viwanda vya kutengeneza vibarua kwa ajili ya matajiri, vikiwapa raia vyeti kwa ajili ya kutoa huduma, wakati huo huo vikionekana kuwanyang’anya leseni wale vinavyowadhania kuwa hawafai (waliofeli).” Tafsiri ni yangu. Illich anatoa mapendekezo ya kukomesha mfumo huu wa baadhi ya watu kujipa wajibu wa kuwaelimisha wengine wakati wao wenyewe hawajielimishi. Haoni haja ya kuwa na majengo yanayoitwa shule ambayo kazi yake inaonekana kuishia kutengeneza watumwa wa soko huria...

Familia ya Lowassa yachunguzwa Ughaibuni

Picha
MTOTO wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa anayeitwa Frederick Lowassa anachunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania, Raia Mwema limedokezwa. Kwa habari zaidi bonyeza hapa .

Wasemavyo wanablogu kuhusu Uchaguzi Mkuu

Ifikapo tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania zaidi ya milioni 19.6 watafanya uamuzi muhimu kuhusu hatma ya nchi yao. Watafanya hivyo kupitia uchaguzi mkuu wa nne chini ya mfumo wa vyama vingi. Wakati zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi huo, ulimwengu wa blogu wa Tanzania nao unafuatilia kwa karibu yale yanayotokea katika kampeni za vyama mbalimbali. Hapa Deogratias Simba wa Global Voices on line anatukusanyia habari kutoka kwa wanablogu. Bonyeza hapa kusoma makala nzima. Ukitaka kwa kiingereza bonyeza hapa . Unaweza pia kusoma makala nyingine kupitia ukurasa huu wa kiswahili wa Global Voices.

Mnalipwa kwa kushabikia upuuzi?

TULIWAHI kujadili wakati fulani tafsiri hasa ya msomi na usomi. Mimi bado ninaamini nchi yetu ina uhaba mkubwa wa watu wenye hadhi hiyo nyeti. Wengi wetu ni wasomaji kwa maana ya kuwa na uwezo kujua vitabu vimeandikwa nini na kwa kweli ninaamini ‘wasomi’ tulioanao hawatusaidii. Tunafahamu kabisa kwamba uchakachuaji/kughushi ni sehemu muhimu ya mfumo wa elimu yetu. Ndivyo tulivyojengwa. Ndio maana hata sikushangazwa na tafiti za hivi karibuni zilizokuwa na nia ya kubashiri nani na/au chama gani kinakubalika zaidi. Wewe fikiria kama, na si mara moja, mwanafunzi anaweza kabisa kuandaa ripoti ya kisayansi mezani (bila hata kutafuta data maabara) na ikatua mikononi mwa mwalimu wake naye aipitishe; ni nini cha ajabu kwenye tafiti hizi? Umekuwepo mjadala wa kuhoji uhalali wa kuwatumia sampuli ya watu 2000 ili kujua maoni ya watu milioni arobaini. Watu wanadai how comes? Pengine ni vyema kukumbushana kuwa ni kweli inawezekana kabisa maoni ya watu elfu mbili yakajirudia rudia ama kujenga p...

Ujumbe wa Juma: Wapiga kura waumbueni REDET

"...Wapiga kura wasianze kukata tamaa kuwa CCM wataiba kura. Of course wataiba lakini ili 'kura zitoshe' watalazimika kufanya wizi wa 'mchana mweupe' (day light robbery) jambo ambalo sio rahisi sana,japo linawezekana.Wanaweza tu kuchakachua matokeo kama,kwa mfano Dokta Slaa akipata asilimia 51 na Kikwete asilimia 49.Hapo watarejea uchakachuaji kama ule wa Zanzibar.Lakini kama ni tofauti ya double digits,wanaweza kupatwa na kigugumizi katika kufanikisha ujambazi huo. Ni muhimu kutovunjwa moyo na hujuma hizi.Yatupasa kufahamu kuwa Kikwete na CCM yake ni kama mgonjwa mahututi ambaye yuko tayari hata kuning'inia kwenye uzi ili asalimike.Tutashuhudia vituko zaidi ya huo uchakachuaji wa REDET..." Kwa makala nzima bonyeza hapa . Asante sana Ndugu Evarist Chahali wa kulikoni Ughaibuni .

Ujumbe wa wiki hii

Picha
NAANDIKA makala hii kwa moyo wa upendo, mtu unayempenda ni lazima umwambie ukweli. Ukimficha ukweli unakuwa humpendi; ni kweli ukweli unauma na mara nyingi hatupendi kabisa kusikia ukweli; hata hivyo hakuna wa kutengua kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa vile Mungu hatukutani naye uso kwa uso, bali tunakutana naye kupitia kwa binadamu wenzetu; ni haki kusema kwamba msema kweli ni mpenzi wa watu? Naandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania. (Picha ya Kijiji cha Mjengwa) Hii ni aina ya barua ya wazi kwa wale wanaotamani kuendelea kutawala wakati miaka ya kustaafu inakaribia. Labda kuna haja ya kuongeza miaka hii ya kustaafu. Miaka sitini ya sasa watu wanakuwa bado wana nguvu na kutaka kuendelea kutumika au kula “utamu” wa uongozi. Kwa vile sasa hivi umri huu haujasogezwa mbele, kuna haja kuwakumbusha ndugu zetu ambao bado wana “Ambition” ya kutaka kuendelea na mbio hizi za hata kukalia viti muhimu kama urais na uspika, kwa...

Ndivyo walivyoboresha Elimu?

CCM inajigamba sana kwamba imepanua elimu katika nchi yetu. Katika ilani yake ya uchaguzi, CCM inatuambia kwamba shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 1745 mwaka 2005 mpaka shule zipatazo 4102 mwaka jana. Kwamba wanafunzi wanaosoma sekondari katika nchi yetu, wameongezeka kutoka 401,598 mwaka 2005 kufikia 1,401,559 hivi sasa! Kwa mtu anayehesabu mafanikio kwa kuangalia vitu na idadi, haya yanaweza kuonekana kuwa ni mafanikio makubwa sana kuwahi kufikiwa katika nchi yetu. Lakini tukitazama aina ya hao wanaoitwa wanafunzi wanaodaiwa kuwa mashuleni kwa wingi, utashangaa! Katika wanafunzi hao ni asilimia 17.8 tu ndio hufaulu kwa daraja la I. II na III. Umati mwingine unaobaki (yaani asilimia 82.2) wanaishia kupata daraja sifuri na lile la IV. Kwa maana nyingine, kwa kila wanafunzi 10 wanaofanya mtihani wa Taifa, ni wanafunzi wawili tu hupata angalau daraja la III. Hiyo ni elimu ya Sekondari hata baada ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Ukija kwenye elimu ya msingi ambayo n...

Kuvunjika kwa koleo...

Picha
Hivi kama watu mnapendwa na wananchi, mabango haya yote ya kazi gani? Kama kweli ninyi ni chaguo la wananchi, inakuwaje mnatumia mapesa mengi hivi kuwashawishi wananchi hao hao? (picha kutoka Kijiji cha Mjengwa)

Sisi ni nchi ya kaulimbiu?

Nimekuwa nikijiuliza: Hivi raia wa Tanzania tunatambulishwa kwa kitu gani hasa? Tuna mawazo gani ambayo tunaweza kusema, haya ndiyo mwelekeo wa Watanzania? Ni masuala yepi ambayo nje ya vyama vya siasa yanaongoza mwelekeo wa taifa letu? Maslahi ya taifa (ambayo si lazima yafananane nay a chama kimoja kimoja) ni yepi? Je, tunawafundisha nini wanafunzi wetu ambacho kinawafanya wajitambue kama Watanzania? Utamaduni wetu kama raia wa Tanzania ni upi? Tunajipambanuaje kama wananchi mahsusi wa Tanzania katikati ya bara zima la Afrika? Hivi falsafa hasa ya taifa letu ni ipi? Je, ni kasi zaidi na ari zaidi? Je, tumekuwa nchi ya "miaka mitano mitano"? Kwamba baada ya uchaguzi, viongozi wanajiandaa kwa uchaguzi ujao? Tumekuwa nchi ya kauli mbiu? Nchi yetu inaongozwa kwa mwelekeo upi? Ni nini ambacho kiongozi yeyote akishika mamlaka ndicho atakachopaswa kutusaidia tukifikie? Hakuna kitu kibaya sana kama kuishi bila dira. Hakuna ugonjwa mbaya sana kama ule wa kutokujua unakokwend...

Bongo inaumwa kisichoonekana (2)

TUMEKWISHA kuona namna nchi yetu inavyopiga hatua kubwa za kimaendeleo. Na sina shaka kwamba msomaji atakuwa amebaini kwamba hizo zinazoonekana kuwa hatua za kimaendeleo zina walakini. Aidha, tulikuwa tumeishia katika kuyatazama hayo yanayoitwa maendeleo katika sekta ya elimu yanavyolisaidia taifa. Muunganiko wa muhimu ukawa ni kwa vipi rasilimali watu ambayo taifa halikuwa nayo miaka iliyopita, inatusaidia katika kusukuma “maendeleo” mbele? Hapa tungependa kudodosa namna ambavyo ukuaji wa taaluma katika maeneo mbalimbali unavyosukuma mbele maendeleo yetu ili kujaribu kuona ulikolalia ugonjwa wa taifa. ******************************************************* Tumekuwa tukifundisha wanasheria kwa miongo kadhaa sasa. Hawatoshi, lakini wapo na wnafanya kazi zao katika maeneo mbalimbali nchini. Je, watu hawa wametusaidiaje kuondokana na unyanyasaji wa kisheria tunaoupata katika jamii zetu? Taaluma ya sheria imegeuka kuwa mashindano ya kupangilia hoja ili kushinda kesi zisizo na tija....

Bongo inaumwa kisichoonekana

Ni wazi kuwa nchi ya Bongo ya miaka kadhaa iliyopita, si hii ya leo. Mambo mengi ya msingi yanabadilika na kwa kweli yanabadilika kwa kasi kubwa. Hata hivyo, ningependa kuonyesha kwamba tatizo tunalokabiliana nalo katika nchi yetu limejificha katikati ya haya tunayoyaona kama maendeleo. Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa kusogeza zaidi maendeleo kwa wananchi wala wala kwa kuanua demokrasia zaidi wala kukusanya kodi zaidi wala kwa kuongeza wasomi zaidi. Tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa kupembua upotofu wa aina ya maendeleo yetu tunayoonekana kuyataka zaidi na tukiyapata tunayatangaza kupitiliza. Tutazame maendeleo katika sekta ya mawasiliano. Nchi hii haijawahi kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa hii leo katika teknolojia ya mawasiliano. Tuko juu katika nyaja ya mawasiliano baada ya kuwa tumefungua milango yote miaka ya tisini. Yapo makampuni kibao yenye wateja wanaokaribia milioni ishirini kati ya raia milioni arobaini. Na wote hao wanapigiana simu na kuandikiana ujumbe mfupi wa m...

Kwa nini wewe tena Oktoba hii?

Picha
Unatusumbua! Kadiri siku zinavyosonga wajikomba sa-na Salaamu mpaka unaboa! Eti ‘mmeamkaje wapenzi wangu niwapendao…’ Fataki mkubwa wewe! Ulikuwa wapi siku zote? Kisa cha kumsalimia mtu barabarani? Umejua maana yetu eh? Hivi hukutujua siku za nyuma? Unadhani tumesahau… Sikia, Tunakumbuka nyodo zako mara chache ulizokuja Tunakumbuka kauli zako za maudhi Eti sie wako tu iwe isiwe Tukupe tusikupe haikusumbui Ukasema hata ukiwa kule sie wa hapa ni wako Sasa babu sikiliza Mwaka huu ni wa hapa hapa Wote ‘twajua huna uumini wowote Unatafutaga nini kipindi hiki? Ni hivi hivi tu waja majisidi? Wenzio ‘twaswali weye unadipu Kisa? Eti ule mpango wa mlo huko nje Unachekesha… Yaani mie mwenye njaa nikulishe wewe unayebeua! Yaani unitumie fasta, kama kondomu sina maana tena? Umesahau ulivyotufanyia siku zile? Tumekupa ukala ukaondoka? Shukrani yako sitasahau: vumbi la fo wili mjini Kama hunijui vile… Nashangaa umenirudia...

‘Vijana waache kutumiwa’

Picha
JINA LA KAMALA si geni kwa wanablogu wengi. Yeye ni mwendeshaji wa blogu maarufu inayojadili (pamoja na mambo mengine) masuala ya kiutambuzi. Bonyeza hapa kuitembelea . Ndugu Kamala anajulikana pia kwa namna yake ya utoaji maoni huru katika blogu anazozitembelea ambayo hufikirisha na mara nyingine kuibua mijadala zaidi. Blogu hii ilipata fursa ya kuzungumza naye siku chache zilizopita kuhusu falsafa zake, blogu, dini, siasa na mambo yake binafsi. Karibu kujua zaidi kuhusu mwanablogu huyu anayeblogu kutokea kanda ya ziwa. ________________________________________ Ndugu Kamala, nashukuru kwa kukubali kutumia muda wako ili tuweze kujadiliana masuala mawili matatu. Labda tuanze na falsafa yako binafsi. Unaamini nini katika maisha ambacho ndicho kinachobeba utambulisho wako kama Kamala? Naamini katika utu, ubinadamu, upendo na umoja. Napenda kuelewa vitu na kudadisi na ndio maana natumia majina ya kihaya tu ninayoelewa maana yake na kwa nini yawepo… napenda kuacha maisha yaende na kuf...

Mhe. Zitto ni mwanablogu

Picha
Pamoja na kutumia nyenzo za uandishi wa kiraia kama twitter, facebook na majamvi ya kijamii kama Jamiiforums nk, Mhe. Zitto Kabwe ni mwanablogu. Na blogu yake imesheheni elimu na maarifa ambayo tunayahitaji kwenye majikwaa haya ya kiraia. Ameitambulisha blogu yake siku chache zilizopita (tarehe 25 Mei) kwa maneno machache yafuatayo: "Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi kama invyostahili. Nimeamua kuanzisha blogu hii mpya ili liwe jukwaa la kujadiliana jinsi ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Karibu kwa maoni, ushauri na hata makatazo!" Bonyeza hapa kumsoma , halafu uone namna mwanasiasa huyu kijana alivyotofauti na wanasiasa wazee wasiojua kingine zaidi ya redio na magazeti ya kila wiki. Hawajui kwamba zama hizo zilishapita na hazitarudi tena. Karibu sana Mhe. Zitto.