Sisi ni nchi ya kaulimbiu?

Nimekuwa nikijiuliza: Hivi raia wa Tanzania tunatambulishwa kwa kitu gani hasa? Tuna mawazo gani ambayo tunaweza kusema, haya ndiyo mwelekeo wa Watanzania? Ni masuala yepi ambayo nje ya vyama vya siasa yanaongoza mwelekeo wa taifa letu? Maslahi ya taifa (ambayo si lazima yafananane nay a chama kimoja kimoja) ni yepi? Je, tunawafundisha nini wanafunzi wetu ambacho kinawafanya wajitambue kama Watanzania?

Utamaduni wetu kama raia wa Tanzania ni upi? Tunajipambanuaje kama wananchi mahsusi wa Tanzania katikati ya bara zima la Afrika?

Hivi falsafa hasa ya taifa letu ni ipi? Je, ni kasi zaidi na ari zaidi? Je, tumekuwa nchi ya "miaka mitano mitano"? Kwamba baada ya uchaguzi, viongozi wanajiandaa kwa uchaguzi ujao? Tumekuwa nchi ya kauli mbiu?

Nchi yetu inaongozwa kwa mwelekeo upi? Ni nini ambacho kiongozi yeyote akishika mamlaka ndicho atakachopaswa kutusaidia tukifikie?

Hakuna kitu kibaya sana kama kuishi bila dira. Hakuna ugonjwa mbaya sana kama ule wa kutokujua unakokwenda. Hakuna nchi yenye hasara kama ile isiyo na maono ya kitaifa. Hakuna kiongozi mbaya kama yule anayeongozwa na kauli mbiu zenye maneno matamu yenye hewa ndani yake. Hakuna. Hakuna kitu kibaya kukubali tuwe nchi ya kauli mbiu za miaka mitano mitano! Na kama wanataka kutupeleka huko, tukatae. Ndio! Tukatae kuwa nchi ya uchaguzi na kauli mbiu zisizo na maana yoyote kwa maendeleo ya mtanzania!

Maoni

  1. Hakika Kaka, huu mchanganuo wako wa leo umenigusa sana.
    Kauli mbiu zisizosimamiwa. Tusubiri nyingine tena...

    JibuFuta
  2. Mkuu, falsafa ya nchi ilikufa na Nyerere. Sasahivi ni bora liende chini ya Kikwete na wenzake. Kasi zaidi eti ndiyo falsafa? CCM wanatenda dhambi mchana kweupe

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Pay $900? I quit blogging