Machapisho

Malezi yanapokuwa ‘rasha rasha’ tuilaumu teknonojia?

Picha
PICHA: businessday.ng Kama ambavyo imeanza kuwa vigumu wengi wetu kumaliza siku bila usaidizi wa zana za teknolojia, ndivyo malezi nayo yanavyoanza kuchukua uelekeo wa kuhitaji usaidizi wa teknolojia. Saa nyingine mzazi usingependa watoto waangalie katuni muda mrefu. Lakini unafanyaje sasa kama wewe mwenyewe hata unapokuwepo nyumbani huna mengi ya kufanya na watoto? Ombwe, kwa kawaida, huwa ni muhimu lizibwe. Lakini pamoja na kusaidia kujaza ombwe la sisi wazazi kutokuwepo kwenye maisha ya watoto, bado teknolojia inayo mengi yenye manufaa. Kubwa zaidi ni kuwachangamsha watoto kiakili.  Nitumie mfano wa mwanangu. Hajakamilisha miaka mitatu. Ukikaa naye anayo mengi ya kukusimulia. Uwezo tu wa kusimulia jambo na likaeleweka katika umri wa miaka miwili sikuuona kwa dada yake waliozidiana karibu muongo mzima. Ingawa bado ni mapema mno kumpeleka darasani, anatambua herufi na tarakimu zote, ana uelewa wa awali wa kuhesabu, anafahamu majina ya rangi nyingi, anawafahamu majina na tabia za w

Tumeiachia teknolojia itulelee watoto wetu?

Picha
  Picha: reviewed.com Jijini Dodoma. Jioni ya Jumatano. Kikombe cha kahawa kinanikutanisha na maswahiba Gwamaka na Dk Mugisha. Tumezungumza mengi. Kisha mada inabadili uelekeo, “Unajua nikiangalia namna hawa wadogo zetu wanavyoyachukulia mahusiano sipati picha itakuwaje kwa watoto wetu.” Mada mpya ya malezi inachukua nafasi yake. Dk Mugisha anakiita kizazi hiki generation X , kumaanisha kizazi kilichozaliwa kwenye teknolojia. Kawaida, kila kizazi huona kilikuwa afadhali kuliko kizazi kinachofuata. Hata wazazi wetu, kimsingi, walikuwa na wasiwasi na sisi. Lakini ni ukweli pia kuwa mabadiliko makubwa ya kiteknolojia tunayoyashuhudia hivi sasa yamebadili kabisa namna tunavyoishi na kuchukulia mambo. Gwamaka anaona huu urahisishwaji wa kupata taarifa umeunda tatizo jipya tunalohitaji kulitazamwa. “Teknolojia imerahisisha mno watu kuyatangaza maisha yao mitandaoni. Tunajilinganisha mno na kuyatazama maisha kwa mizania ya vitu. Hili linaweza kuwasumbua sana vijana wanaochipukia hivi sasa

Unajua kugombana bila kufukua makaburi?

Picha
Picha: pixabay “Msitumie vibaya elimu zenu bwana,” Godi anaanzisha sogo kijiweni. Unamkumbuka?  Kaona kukaa haitoshi. Kasimama kabisa. Mikono inapepea hewani kusisitiza hoja, “Haya mambo yameanza leo? Ndoa zilikuwepo tangu enzi na enzi na hapakuwa na shida. Sasa nyie leo mnasema eti sisi wanaume ndio hatujui mahitaji ya wanawake? Mbona wazee wetu hawakujua hayo yote na bado ndoa zilidumu.”   Siku hizi ukitaka kuwachokoza wanaume ongelea matukio ya wanawake kunyanyasika. Salu kakaa pembeni anausoma mchezo. Tabasamu lake linaunga mkono hoja.   Hata hivyo, naona naye uvumilivu umemshinda. Kaamua kuulinda uanamue, “Hizi harakati zenu za kuwabeba wanawake zitatuharibia ndoa. Mie nawaambieni. Mnawatetea sana wanawake na watapata vichwa kweli. Wakitushinda tuwaleteeni basi.” Joto limepanda. Hisia hizi za akina Salu si za kupuuza. Mgogoro unapotokea kwenye ndoa, anayebebeshwa mzigo wa kutokufanya wajibu wake, mara nyingi, ni mwanamke. Msikilize Peki anavyogongea muhuri dhana hiyo:  

Mahusiano yenye ‘utulivu’ bila amani

Picha
Chanzo: stock.adobe.com Hivi umewahi kutaka kumwambia mtu jambo unaloona ni muhimu lakini ukakosa namna nzuri ya kumwambia?Unatamani ujumbe ufike lakini maneno sahihi ya kuubeba huna. Unafanyaje? Wengine huamua kuacha. Kuliko kumwuumiza mwenzako, huona bora mtu uugulie maumivu ndani kwa ndani. Mwingine hajali. Huamua bora ‘kutema nyongo’ hivyo hivyo bila kujali maumivu yatakayoyasababishwa na ujumbe. Wanachosahau, matokeo yanayotokana na k u jiumiza kwa kuuzuia ujumbe yanaweza kuwa sawa na madhara ya kuuachia ujumbe kiholela bila kujali maumivu ya atakayeupokea.   Mawasiliano ni sayansi yenye nafasi nyeti katika mahusiano. Ukikosea kanuni, mawasiliano yana nguvu ya kuleta uharibifu mkubwa unaoweza kugharimu afya ya mahusiano. M awasiliano ni sanaa pia.   Namna unavyosema jambo ni muhimu wakati mwingine kuliko hata ujumbe wenyewe. Ukishindwa kuchagua maneno sahihi na mazingira sahihi ya kusema jambo unaweza kufubaza uzito wa ujumbe wako. Thamani ya unachokisema inabebwa pia na namna

Unafanyaje kutathmini mabadiliko yako?

Picha
Picha: Mpiga picha simkumbuki. Mwaka ni 2004. Tunabadilika jamani. Sijui nyie wenzangu. Labda ni mimi peke yangu lakini saa nyingine ni vigumu kujiona tunavyobadilika. Usipopata mrejesho kutoka kwa watu unaweza kufikiri uko vile vile. Lakini ukweli ni kwamba tunabadilika. Tuanze na maumbile ya mwili. Mwili ukibadilika ni rahisi kuona. Hukuwa na kitambi, kwa mfano, sasa unacho. Tumbo nalo huwa halina-ga adabu. Badiliko lake linakuja taratibu sana. Halichomozi kwa siku moja. Unaweza ukawa unakula bila mpango, huoni ukibadilika. Unachukulia kawaida. Kuja kustuka, aloo kulitoa inakuwa shughuli. Ukiacha tumbo, kwangu kuna hili la macho. Ilinichukua muda mrefu kukubali kuwa sioni mbali. Nilikuwa nalazimika kufinya macho. Naona kawaida. Baadae sikuwa na namna. Ikabidi kukubali kuvaa miwani. Ushahidi mwingine huo. Mabadiliko hayana-ga haraka. Huja taratibu sana. Kingine mavazi. Tazama picha inayoambatana na maandishi haya. Hapo ni miaka 18 imepita. Huyo mwenye tai ni mimi. Sijui nini kilitokea

Mwanaume anapokimbia 'kelele' nyumbani

Picha
  Mwanadamu ana uwezo mkubwa wa kuficha tabia. Samahani. Namaaminisha mwanaume. Unajua, katika jamii zetu, ni aibu mwanaume kukiri mahusiano yamekushinda. Kuliko kuitwa kila aina ya majina saa nyingine tunalazimika kujenga taswira ya ukamilifu hata kama kiuhalisia tunaugulia maumivu makali. Jumlisha hapo dini, kwa maana ya hizi itikadi za ufuasi wa halaiki, kiwango cha kuonesha ukamilifu lazima kiwe juu zaidi.   Tumeaminishwa ndoa ni kielelezo cha ukamilifu. Hakuna kukosea. Ukishasema una changamoto na mwenzako, watu wanakupiga jicho la dhihaka, “Hukumwomba Mungu akupe mke? Humtegemei Mungu vya kutosha?” Nani yuko tayari kuonekana hana uhusiano mzuri na Mungu?   Kwa upande mmoja, ninamuelewa sana Godi. Hofu ya kuchafua jina lake inamfanya aigize amani ya ndoa isiyokuwepo.   Swali nililojiuliza, kwa nini sasa Godi amefikia mahali hajali watu wa nyumbani kwake? Kama ana tatizo na mkewe, inakuwaje anashindwa kujali hata watoto?    Kila tabia, kwa kawaida, haikosi historia.  “

Usidanganyike. Wema huanzia nyumbani.

Picha
Umewahi kukutana na mtu mwema kiasi kwamba unawaonea ‘wivu’ familia yake? Unajiuliza, “kama huyu jamaa anaweza kuwa mkarimu hivi kwa sisi wapita njia tusiomhusu kivile, nyumbani kwake si watakuwa wanamfaidi sana?” Sasa usinielewe vibaya. Silengi kukukatisha tamaa. Ni vile tu nimeshangazwa hivi majuzi.   Godi ni rafiki yangu wa siku nyingi. Kwa hulka, ni mtu mchangamfu mwenye wingi wa bashasha. Kaa na Godi mzungumze utapenda namna yake ya kuzungumzia masuala. Godi anajua aseme nini wapi na kwa nani.   Halafu kuna wema. Godi hasubiri umtafute. Haipiti wiki hajakupigia na wala hatakuuliza kwa nini humpigii. Hivyo. Ukiwa na shida, Godi huyu hapa. Hana uwezo sana kifedha. Maisha yake ni haya haya kama ya wengi wetu. Sema ni ule utajiri tu wa roho ya mtu. Usha’nfahamu? Godi. Ukiniuliza mtu mwema nimewahi kukutana naye, nitakwambia Godi bila hata kupepesa macho.   Jamaa yetu mmoja aliwahi kumsifia kiutani lakini alikuwa sahihi. Kwa jinsi alivyo mwema, jamaa alisema, Godi anaweza a

Jinsi ya kumlinda mtoto na tofauti zenu

Picha
Simulizi la Renee limenikutanisha na wadau wa ushunuzi mjini Moshi. Tunapata kahawa jioni baada ya shughuli za siku. Hatujaonana muda. Tunasalimiana na kisha mada inageuka ghafla. Rebert anarejea mfano wa Renee, “Suala la mgogoro wa wazazi kumuathiri mtoto hilo halina mjadala.” Robert ‘anavuta’ kahawa kidogo kama mtu anayesikilizia ladha ya kinywaji cha moto sana na kisha anaendelea.   “Ukimsoma huyu dada ni dhahiri migogoro ya kifamilia ilikuwa na nguvu ya kuchora mwelekeo wa maisha yake ya kimahusiano.” Robert anasita. Wajumbe wamepotelea kwenye vioo vya simu zao. Kajihisi anaongea mwenyewe. Natingisha kichwa kumwitikia.   “Inasikitisha sana namna maamuzi yetu kama wazazi yanavyoweza kumnyanyasa mtoto kwa kiasi kile. Sitamani niwe mzazi nitakayemfanya mtoto awe na kazi kubwa ya kurekebisha tabia alizojifunza kwangu,” anajitahidi kujieleza Robert lakini kakatishwa tamaa. Wanaume hawamsikilizi wanacheka na simu zao. Hata mimi pia ninahisi huenda ninamsikiliza mwenyewe.   K

Usiyempenda anaweza kuwa baba wa mwanao?

Picha
  Watoto wanahitaji uwepo wa mzazi. Simulizi la Slaquara lilitukumbusha hakuna muujiza kwenye malezi. Mzazi unavuna ulichopanda. Renee anakazia funzo hilo. “Umeongelea athari za umbali kati ya mzazi na mwanae. Nayajua maumivu yake,” anasita na kufafanua, “Sikumbuki lini niliongea na mama yangu. Siwezi kusema ni adui yangu lakini sio mtu naweza kumtegemea kwa lolote.”   “Mara ya mwisho kuonana naye ni miaka miwili iliyopita alipokuja kusuluhisha mgogoro wangu na mzazi mwenzangu,” leso anayoitumia kujifutia inalowa machozi. Renee anaikunjua na kuigeuza kutafuta penye ukavu. “Nilimpa nafasi ya pili akaitumia vibaya. Badala ya kusikiliza upande wangu anielewe, aling’ang’ania kuwa upande wa yule mwanaume akinilazimisha kuishi naye. Hakutaka kabisa kuelewa kwa nini nilichagua abaki kuwa mzazi mwenzangu na si zaidi ya hapo.”   Mgororo huu mkubwa wa mzazi na mwanae umeanzia wapi? Renee anasimulia, “Nimekuzwa kama mtoto yatima. Nasimuliwa baba alipofariki nikiwa mdogo sana, mama alinipe