Unajua kugombana bila kufukua makaburi?
Picha: pixabay “Msitumie vibaya elimu zenu bwana,” Godi anaanzisha sogo kijiweni. Unamkumbuka? Kaona kukaa haitoshi. Kasimama kabisa. Mikono inapepea hewani kusisitiza hoja, “Haya mambo yameanza leo? Ndoa zilikuwepo tangu enzi na enzi na hapakuwa na shida. Sasa nyie leo mnasema eti sisi wanaume ndio hatujui mahitaji ya wanawake? Mbona wazee wetu hawakujua hayo yote na bado ndoa zilidumu.” Siku hizi ukitaka kuwachokoza wanaume ongelea matukio ya wanawake kunyanyasika. Salu kakaa pembeni anausoma mchezo. Tabasamu lake linaunga mkono hoja. Hata hivyo, naona naye uvumilivu umemshinda. Kaamua kuulinda uanamue, “Hizi harakati zenu za kuwabeba wanawake zitatuharibia ndoa. Mie nawaambieni. Mnawatetea sana wanawake na watapata vichwa kweli. Wakitushinda tuwaleteeni basi.” Joto limepanda. Hisia hizi za akina Salu si za kupuuza. Mgogoro unapotokea kwenye ndoa, anayebebeshwa mzigo wa kutokufanya wajibu wake, mara nyingi, ni mwanamke. Msikilize Peki anavyogongea muhuri dh...