Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2015

Watoto Waliokosa Masomo Nchini Libya Wafundishwa kwa Njia ya Skype

Picha
Hali tete ya kiusalama nchini Libya imewafanya watoto washindwe kwenda shule tangu mwezi Oktoba. Kwa kuwa watoto hawawezi tena kuhudhuria masomo katika shule zao, El-Zahawi aliwaza ni kwa nini asisogeze madarasa karibu na huko walipo? Na hapa ndipo Shule ya Skype ya Benghazi ilipozaliwa rasmi.

CCM ni maarufu Kigoma kwa 40.2%, ikifuatiwa na CHADEMA kwa 27.2%

Picha
Utafiti huru uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umeonesha kwamba mgombea yeyote wa nafasi ya Urais wa Chama cha Mapinduzi angeweza kuchaguliwa na wapiga kura wa Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa asilimia 40.2% ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu jioni ya leo.

Kujenga Nidhamu kwa Mtoto wa Miaka Miwili hadi Mitatu

Picha
Kiini cha mahusiano ya mzazi na mwanae asiyezidi miaka mitatu, ni upendo. Kupitia upendo mzazi anaweza kufikiri vizuri zaidi kile anachokihitaji mtoto na kukishughulikia ipasavyo. Hata hivyo, si wakati wote mtoto wa umri huu hutaka kilicho sahihi. Wakati mwingine kile kinachoonekana kuwa hitaji la mtoto, kina hatari ndani yake na hakiwezi kuachwa kifanyike kwa kisingizio cha kulinda uhusiano wa mtoto na mzazi. 

Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Wakati wa Majanga ya Kitaifa?

Picha
  "TWITI TENA kama unadhani PNoy alipaswa kuhudhuria mapokezi ya heshima badala ya tukio la Kiwanda cha Magari. #NasaanAngPangulo" alitwiti @BobOngWords. Alama habari #NasaanAngPangulo, yenye maana 'Rais yuko wapi' katika lugha ya Kitagalog, ilikuwa mada maarufu zaidi kwenye mtandao wa Twita duniani wakati Wafilipino walipokuwa wakionesha hasira zao kwa Rais Noynoy Aquino kufuatia  kukosekana kwake  kwenye mapokezi ya heshima ya miili ya polisi waliouawa wakiwa kwenye operesheni maalum.