Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

Jenga Fikra Chanya, Uwe na Furaha

Picha
Kuwa na furaha ni uamuzi wako mwenyewe. Furaha ni matokeo ya namna ulivyoamua kufikiri. Kadhalika, kukata tamaa na kukosa amani mara nyingi ni matokeo ya kufikiri mambo yanayokatisha tamaa na wakati mwingine tusiyo na majibu yake. Tunatafsiri vibaya mambo tunayokutana nayo na ndiyo sababu tunapatwa na msongo wa mawazo.

Kumfundisha Mtoto Kuwajibika, Kufanya Kazi

Picha
Kumjengea mtoto uwezo wa kuwajibika ni wajibu muhimu sana wa wazazi. Bila kuweka mkazo mapema katika kukuza uwezo huu, mtoto anaweza kuwa mtu mzima asiyefahamu kufanya majukumu mengi ya msingi na ya kawaida. Mtoto aliyefundishwa kuwajibika hujiona ana wajibu wa kushiriki shughuli za ndani bila kujali jinsia yake.  Katika makala haya, tunaangalia namna unavyoweza kumsaidia mtoto wako kujifunza kuwajibika angali mdogo na hivyo kujenga uwezo wa kumudu majukumu ya msingi kadri anavyoendelea kukua.

Kujenga Uwezo wa Kufanya Maamuzi kwa Mtoto

Picha
Unajisikiaje mzazi unapogundua mtoto ameanza kujifunza tabia zisizofaa? Inaumiza, kwa mfano, kuona mtoto anaanza kujifunza wizi, kudanganya na hata kutokuwa na uwezo wa kujisimamia mwenyewe bila uangalizi wa karibu.   

Kumsaidia Mtoto Kujifunza, Kumudu Lugha -2

Picha
Makala yaliyopita yalipendekeza njia nne za kumsaidia mtoto mdogo kujua kuongea. Kadhalika, tuliona hatua kuu anazopitia mtoto katika kujifunza lugha. Katika makala haya, tunamtazama mtoto anayejua kuongea na tunaangalia mapendekezo kadhaa ya kumsaidia kuwa mtumiaji mahiri wa lugha katika mawasiliano yake ya kila siku.

Tunavyoweza Kuacha Tabia ya Kuhukumu Wengine

Picha
Majuzi nikiwa kwenye mgahawa mmoja mjini, waliingia watu wawili wanaume waliokuwa wamevalia mavazi yanayoashiria imani yao ya kidini. Wote wawili walipamba vichwa vyao kwa vilemba nadhifu, mmoja wao akibeba mfuko mdogo mweusi. Nyuso zao, kwa hakika zilipambwa na tabasamu pana la kirafiki lililofanya ndevu zao ndefu ziwe na mwonekano wa kupendeza. Miguu yao ilivaa viatu vya wazi na juu yake zilining’inia suruali fupi mithili ya kaptula ndefu zilizojitokeza ndani ya kanzu fupi nadhifu.

Kwa Nini Tunapenda Kusikia Habari Mbaya?

Picha
Umewahi kujiuliza kwa nini habari tunazofuatilia kwenye vyombo vya habari mara nyingi ni matukio mabaya? Kwamba ili iwe habari yenye kuvutia watu wengi mara nyingi hulazimu iwe habari ya jambo lisilotarajiwa. Kwa mfano, habari za mbunge kulala wakati kikao cha bunge kikiendelea inaweza kuwa na mvuto kuliko habari ya namna mbunge huyo huyo alivyotekeleza wajibu wake kabla ya ‘kupitiwa na usingizi.’

Kumsaidia Mtoto Kujifunza na Kumudu Lugha

Picha
Lugha ni nyenzo muhimu sana tunayoihitaji katika maisha. Hatuwezi kufikiri vizuri, kuongea kwa ufasaha, kusikiliza, kueleza mambo tuliyokutana nayo na hata tunayoyatarajia siku zijazo bila kuhitaji lugha. Ni wazi tunalazimika kutumia maneno au ishara kuwasiliana na wanaotuzunguka. Mjadala wa namna gani mtoto hujifunza lugha ya mama una historia ndefu. Kwamba mtoto huzaliwa na asili ya lugha inayoongoza namna anavyojifunza lugha au ni mazingira anayokulia ndiyo yanayomwezesha kujifunza, ni vigumu kuhitimisha kwa hakika. Hata hivyo, kuna ukweli kwamba ili mtoto ajifunze lugha ipasavyo anahitaji kuwa na uwezo fulani anaozaliwa nao unaomwezesha kuelewa kanuni muhimu za lugha bila msaada mkubwa. Lakini pia mazingira, anayokulia mtoto, nayo yana nafasi kubwa ya kumwezesha kujifunza na kumudu lugha ya kwanza kirahisi.