Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Msongo wa Mawazo

Mbinu za Kukabiliana na Sonona, Hofu Mahali pa Kazi

Picha
Tuchukulie unafanya kazi muhimu inayotakiwa ndani ya masaa mawili yajayo. Wakati ukikimbizana kumalizia kazi hiyo, umeme unakatika. Ofisi haina jenerata na huwezi kutumia kompyuta bila umeme. Unajawa na wasiwasi lakini huna cha kufanya.

Mwanaume Anayejitambua Hatishwi na Mafanikio ya Mwanamke

Picha
PICHA: Ayo Martins Upo ukweli usiosemwa wazi kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Wanawake waliosoma, wenye mali na fedha, wenye madaraka makubwa katika jamii, wanakuwa na mtihani mkubwa kuanzisha na kudumisha uhusiano na wanaume.

Unavyoweza Kutumia Mshahara Kujikwamua Kiuchumi

Picha
Wapo watu wanawakejeli wafanyakazi kwa kuajiriwa. Kwamba kama mtu asiye na elimu anaweza ‘kuosha magari mtaani’ na akakuzidi kipato kuna sababu gani kuishi maisha magumu ofisini? Upo ukweli wa namna fulani. Wafanyakazi wengi wanaishi maisha ya ukata. Kazi yao kubwa ni kupambana kuhakikisha kuwa mishahara inakutana. Katika mazingira ya namna hii, inakuwa vigumu kupiga hatua za maana kimaisha.

Kwa Nini Maazimio Mengi ya Mwisho wa Mwaka Huwa Hayatekelezeki?

Picha
Kila mwaka mpya unapoanza, ni kawaida kwa watu wengi kuweka maazimio fulani ya kutekeleza. Wapo ambao huazimia kubadili tabia wasizozipenda. Wengine huazimia kuanzisha mwenendo mpya wa maisha wanayoyatamani. Wengine hufikiria kutekeleza malengo fulani ya kijamii na kiuchumi yatakayobadili maisha yao kwa mwaka unaoanza. Ingawa ukweli ni kuwa mwaka unapoanza kinachobadilika huwa ni tarehe tu, watu huwa na imani kuwa wanaingia kwenye zama za maisha mapya. Imani hiyo huambatana na jitihada za kujaribu kubadili maisha yao yaendane na zama hizo mpya. Wanasema, ‘mwaka mpya na mambo mapya!’

Unaweza Kumfundisha Mtoto Adabu Bila Kumchapa

Picha
Mjadala wa fimbo na malezi una historia ya mjadala mkali. Fimbo, kwa hakika, zimekuwa kama sehemu ya maisha yetu . Takwimu zinathibitisha hali hii. Kwa mfano, asilimia zaidi ya 80 ya wazazi wa nchi zinazoendelea wanatumia fimbo angalau mara moja kwa mwezi. Ndio kusema, vipigo kwa watoto vimekuwa sehemu ya malezi katika nchi zetu hizi. Matumizi haya makubwa ya fimbo kwa kiasi fulani yanatokana na imani waliyonayo wazazi kuwa bila mtoto kusikia maumivu hawezi kurekebisha tabia wala kuwa msikivu. Ingawa hakuna ushahidi wowote kuwa viboko vinasaidia kujenga nidhamu kwa watoto, bado wazazi wengi wanaamini adhabu ya fimbo ndiyo jibu la kumnyoosha mtoto.

Mwaka Mmoja Bila Mama, Mkono wa Mungu Haujatuacha…

Picha
Nakumbuka mwezi Juni 2002, nikiwa mwanafunzi wa sekondari, eneo ni stesheni ya gari moshi (treni) mjini Singida nikiwa ninarudi nyumbani nikitokea Dodoma. Ilikuwa ni safari ya kuunga unga iliyoanzia Dar es Salaam kupitia Dodoma na kisha Singida. Wakati huo tulikuwa tunaondoka Dodoma saa nne asubuhi, Singida tunafika saa za jioni kuanzia saa kumi na moja hivi tukiwa taabani kwa uchovu wa kukaa kwenye mabehewa yaliyoonekana kuhangaika mno kupita kwenye mataruma katikati ya vichaka ya Dodoma na Singida. Jioni hiyo ninayoikumbuka vyema tulichelewa kidogo na hatimaye tulifika Singida stesheni saa kumi na mbili unusu hivi za jioni.

Jenga Fikra Chanya, Uwe na Furaha

Picha
Kuwa na furaha ni uamuzi wako mwenyewe. Furaha ni matokeo ya namna ulivyoamua kufikiri. Kadhalika, kukata tamaa na kukosa amani mara nyingi ni matokeo ya kufikiri mambo yanayokatisha tamaa na wakati mwingine tusiyo na majibu yake. Tunatafsiri vibaya mambo tunayokutana nayo na ndiyo sababu tunapatwa na msongo wa mawazo.

Kwa Nini Tunapenda Kusikia Habari Mbaya?

Picha
Umewahi kujiuliza kwa nini habari tunazofuatilia kwenye vyombo vya habari mara nyingi ni matukio mabaya? Kwamba ili iwe habari yenye kuvutia watu wengi mara nyingi hulazimu iwe habari ya jambo lisilotarajiwa. Kwa mfano, habari za mbunge kulala wakati kikao cha bunge kikiendelea inaweza kuwa na mvuto kuliko habari ya namna mbunge huyo huyo alivyotekeleza wajibu wake kabla ya ‘kupitiwa na usingizi.’

Kuanzisha na Kuimarisha Urafiki wa Karibu

Picha
Katika zama hizi za maendeleo ya kidijitali, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki. Unaweza, kwa mfano, kuwa na ‘marafiki’ elfu tano kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja katika maisha halisi. Marafiki wa kweli na wa karibu ni moja wapo ya mahitaji muhimu katika maisha. Tunaweza kuwa na sababu nyingi kuhalalisha kwa nini hatuna (haja na) marafiki wa karibu.  Hata hivyo, zipo nyakati  hufika tukajikuta katika maisha yenye kujaa upweke  na msongo wa mawazo kwa sababu hatukutumia muda wetu kutengeneza urafiki wa karibu na watu tunaofahamiana nao.

Watoto Waliokosa Masomo Nchini Libya Wafundishwa kwa Njia ya Skype

Picha
Hali tete ya kiusalama nchini Libya imewafanya watoto washindwe kwenda shule tangu mwezi Oktoba. Kwa kuwa watoto hawawezi tena kuhudhuria masomo katika shule zao, El-Zahawi aliwaza ni kwa nini asisogeze madarasa karibu na huko walipo? Na hapa ndipo Shule ya Skype ya Benghazi ilipozaliwa rasmi.

Muhtasari na Hitimisho, 'Kanuni zinazoongoza mahusiano na migogoro ya wanandoa'

Picha
TANGU tulipoanza mfululizo wa makala za mahusiano , jambo kubwa nililojaribu kulionesha ni nafasi ya mahitaji ya hisia katika kuimarisha au kuvuruga mahusiano. Na msingi wa haya yote ni kusema kwamba mahusiano hayana miujiza. Mahusiano yanaongozwa na kanuni za kawaida sana ambazo ukifanikiwa kuzitambua na kuzitumia utapunguza kama sio kuondoa matatizo mengi. Kwa mhutasari, ningependa tuyapitie mambo makuu yaliyojitokeza katika mjadala wetu kwa kuyaweka katika makala moja inayojitegemea.

Tunapambana na UKIMWI kwa kupambana na utu wa watu wanaoishi na VVU?

Picha
Hivi majuzi nilipata fursa ya kushiriki mradi unaojaribu kudhibiti maambukizi ya virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa kuwasaidia watu wanaoishi na virusi hivyo kukabiliana na hali hiyo ambayo kwa hakika hugeuza kabisa maisha yao. Fursa hii adhimu ilinifungua macho kuona kile ambacho sikuwahi kukiona kwa muda mrefu. Nisingependa kutoa takwimu za tafiti za majumuisho zinazojaribu kuonesha hali ikoje kwa ujumla bali takwimu za hali halisi niliyoiona kwa macho yangu.

'Usawa wa kijinsia' unavyoweza kuharibu mahusiano

Picha
Wanawake wanatafuta haki ya kuwa sawa na wanaume. Na wamefanikiwa. Katika makala haya tunajaribu kuonesha hatari ya wanawake kudhani wanaweza kuwa sawa kijinsia na wanaume na bado waweze kuwa na mahusiano imara na wanaume. Ni salama zaidi kwa wanawake kuelewa kwamba usawa wa kijinsia haumaanishi kufanana kwa wanaume na wanawake. Ingawa ni kweli tunapigania usawa wa fursa, bado twapaswa kutambua haitawezekana wanaume wakageuka kuwa wanawake na wanawake kadhalika wakageuka kuwa wanaume.

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Picha
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.

Namna ya kukopeshwa kirahisi na kuchangiwa michango ya harusi na marafiki

Picha
WALA usishangae hata kidogo. Umesoma vyema kabisa kichwa cha habari. Tunataka kujifunza namna bora kabisa za kuwapiga watu mizinga. Kukopa na kuchangiwa michango ya harusi. Vyote hivi vinafanana kimsingi kwa sababu vyote vinategemea hisani ya watu wanaoitwa ndugu, jamaa na marafiki. Kwako usiyekopa, nikuambie mapema kabisa, hapa si mahali pako. Makala haya ni mahususi kwetu sisi wakopaji maarufu ambao (ni kama vile) haiwezekani kabisa kumalizia mwezi bila kuongezea na za watu. Sasa ili nieleweke nawalenga watu gani, niseme awali kabisa kwamba hatuzungumzii mikopo ya taasisi za fedha kwa ajili ya maendeleo. Nazungumzia mikopo kutoka kwa watu kwa ajili ya kusukuma siku, au misaada ya kufanikisha harusi. Wazo la kuandika mikakati hii madhubuti ya kukopa, nimelipata jana baada ya kusoma taarifa ya google kuhusu kile hasa kilichotafutwa na watumiaji wa mtandao (netzens) kupitia kwenye google, kilichowaongoza na kujikuta wakiwa kwenye blogu yangu. Hapa nanukuu sentensi mbili nilizoziona:...

Tunawezaje kujinasua na matatizo ya msongo wa mawazo?

Hivi sasa imekuwa ni kawaida kukutana na mtu anayezungumza mwenyewe. Na si tu kuzungumza mwenyewe, bali hata kurusha rusha mikono huku na kule. Waweza kukutana na mtu anayetazama lakini haoni, anayesiki lakini hasikilizi, na anayesema asichojua anachokisema. Si hivyo tu. Imeanza kuzoeleka kukutana na mtu ofisini mwenye hasira za mafungu dhidi ya kila anayehitaji huduma yake. Hasira zinazoambatana na kufoka, kusema pasi mpangilio, na hata kutukana watu wasio na makosa ya moja kwa moja hovyo hovyo. Vile vile, ni kawaida kukutana na watu wenye ghadhabu katika sehemu za umma, kama kwenye usafiri wa wote, foleni za benki na kadhalika. Watu wanaonekana kuwa na hasira ambazo kimsingi chanzo chake si hapo alipo.  Hizi ni dalili za msongo wa mawazo. Na zipo nyingi. Kuyasema haya hatujaribu kuonyesha kuwa msongo wa mawazo/stress ni kitu kibaya moja kwa moja. Hapana. Kwa hakika kiasi fulani cha stress kinahitajika ili kutufanya tuhimizike kupiga hatua fulani. Hata hivyo, msongo huu ...

Kuwa mwenye furaha ni uamuzi wako mwenyewe!

Picha
Ni mara ngapi umewahi kukutana na mtu aliyekukwaza kiasi cha kumtupa katika kapu la “watu wa hovyo” wasiostahili heshima kama binadamu? Umewahi kupatwa na tukio ambalo lilibadili kabisa mtazamo wako kuhusu maisha, watu na maisha kwa ujumla? Kwa nini watu kukata tamaa? Umewahi kuwaza kwa nini kinachomkwaza huyu si lazima kimkwaze yule? Umewahi kuonana na mtu anayeshangaa inakuwaje “huyu bwana achukue uamuzi wa ajabu namna ile” wakati kilichotokea kinachukuliwa na wengi kuwa “ni jambo la kawaida”? Natamani ukimaliza kusoma hapa uelewe kwamba sehemu kubwa ya matatizo tunayokabiliana nayo kama binadamu kila siku, tunayasababisha wenyewe. Na kwa yale tusiyo naudhibiti nayo, tunaweza kubadili mtazamo wetu kwayo, na hilo linaloonekana kuwa tatizo ama likawa si tatizo au likabadilika kuwa changamoto. Wengi wetu tunapokumbana na vikwazo (ambavyo mara nyingi huwa ni watu, vile mambo yalivyo na matukio yanayokuwa katika namna tusiyoitegemea) hujenga mawazo kwamba vitu hivyo vi vibaya. Mato...

Michael Jackson na athari za malezi

Si muda mrefu nilikuwa nikitazama ibada ya maziko ya Michael Jackson. Kwa wengi, Michael ni alama ya watu wasiojikubali. Wengi wanamlaumu kwa uamuzi wake wa kujifanyia marekebisho sura yake. Wengine wakamwita 'Wacko' yaani chizi. Kama umefuatilia historia ya uhusiano wake na wazazi wake utabashiri nini kilikuwa chanzo cha yote hayo. Uhusiano wake na baba yake haukuwa mzuri. Mzee si tu kwamba alikuwa mkali sana, lakini pia alikejeli maumbile ya mwanae huyo. Nadhani yapo zaidi ya haya yasiyosemwa wazi. Maana fikiria hata wosia aliouacha Michael umeonya kuwa wazazi wake wasihusishwe na mirathi. Hata katika maziko, wazazi hawakuongea! Inasemwa, wakati Michael anaanza kujikwatua, mzee alimwonya sana pasipo mafanikio. Kisiki kwa wazazi wengi: Wanadhani kumwonya mtoto msiyehusiana nae kwa karibu, mtoto aliyekufuta akini mwake, kunasaidia...! Mzazi usifanye kosa la Mzee Joseph Jackson.

Kamwe usikate tamaa

Haya tena. Siku zinakimbia kama nini vile. Ni juzi tu mwezi umeanza. Leo eti masaa machache yajayo mwezi unakatika hivi hivi. Mwaka ndio usiseme. Mwezi wa kumi na moja huu. Bado mwezi tu na mwaka ukatikie mbali. Sijui kinachosababisha siku kukimbia namna hii. Muda ni mfupi kuliko matarajio. Mambo mengi kuliko dakika zilizopo. Kazi kweli kweli. Binafsi mwezi huu umepita vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale. Nafurahi nimeweza kuzitazama changamoto hizo kwa jicho la kujisahihisha. Nawe ndugu msomaji bila shaka mwezi umekuendea vyema. Hata kama inawezekana umekumbana na changamoto mbili tatu hakuna haja ya kukata tamaa. Usikate tamaa. Kuna mtu aliwahi kuniambia picha nzuri kusafishwa kwenye chumba cha giza. Giza ni muhimu ili kusafisha picha. Maana yake yake unapojikuta kwenye hali inayofanana na giza vile, kwa maana ya changamoto, kukatishwa tamaa, chukulia hiyo kama mchakato wa kukutengenezea picha nzuri mbeleni. Usikate tamaa. Pigana kiume. Songa mbele. Anza mwezi wa kumi...

Naanza kublogu dini, imani, sayansi na kadhalika

Katika blogu hii natarajia kuwa naendesha mijadala kadha wa kadha. Moja, dini na imani kwa lengo la kuangalia undani wa imani zetu. Je, inawezekana kuishi bila dini? Je, kuna dini ya kweli? Je, Yesu ni Mungu? Mtume Muhammad aliuanzisha Uislam? Na maswali mengine mengi. Pili, nitapitia mara kwa mara masuala ya saikolojia na falsafa nikiamini kwamba ili tuishi vizuri na nafsi zetu lazima tujitambue. Tuzifahamu nafsi zetu na kisha tuwatambue wengine. Tatu, nitarajibu kujipenyeza kwenye mijadala ya sayansi. Ningependa kuona namna sayansi inavyohusiana au kugombana na imani.. Yapo maswali lukuki. Je, sayansi inaweza kufanya kazi bila kuwepo imani? Na je imani bila sayansi, inafaa kwa lolote? Vipi sayansi na dini vinavyoweza kufanya kazi pamoja na kadhalika na kadhalika. Changamoto kubwa, sina kompyuta wala mtandao. Tutafika tu