Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya adhabu

Malezi yanavyochochea ubabe katika jamii

Picha
Natamani tutafakari jambo hili kwa kina. Nyumbani tumemzoesha mtoto fujo —fimbo, makofi, matusi na aina nyingine za ubabe. Sisi wazazi tunaamini hatuwezi kulinda mamlaka yetu bila kumsababishia mtoto maumivu iwe kwenye mwili wake au hisia zake. Ukiangalia yanayoendelea nyumbani hakuna mazungumzo yenye upendo na mtoto. Tunaamini amani na utulivu kwenye ngazi ya familia ni pale tunapokuwa na watoto wasiofikiri, wasiouliza, wasiothubutu kutofautiana na wazazi ambao ndio mamlaka katika familia.     Shuleni mtoto anakutana na mwalimu anayeamini njia pekee na ya uhakika kulinda heshima na mamlaka yake darasani ni vitisho, fimbo na kila aina ya ubabe kwa mwanafunzi. Ukiangalia mbinu za ufundishaji wake huoni wapi anaamini katika ushirikishwaji wa mwanafunzi. Tangu asubuhi mpaka jioni zoezi linalotawala ni wanafunzi kupokea maelekezo na kuyakariri.    Mwalimu anaamini nidhamu ni pale amani na utulivu vinapotawala darasani. Hii, huenda ndio sababu shule zinahangaika na wapiga...

Unalea watoto au unafuga watoto?

Picha
Kila siku saa 12 jioni, Mah’mood mwenye miaka 12 hutoka shule anakosoma moja kwa moja kwenda nyumbani. Mah’mood  anawajua wazazi. Hawawezi kuthubutu kumruhusu kuchelewa nyumbani hata dakika tano. Jaribio lolote la kuchelewa litakaribisha matusi, ukali, na ikibidi kiboko bila maelezo yoyote.  Mah’mood anatamani kuwa mchezaji hodari wa mpira. Ndoto hii imekatishwa baba yake alimwambia, “Hutakula mpira, soma uwe mwanasheria. Hutaki acha shule. Kila Mah’mood anapouliza swali, jibu huwa ni kama limerekodiwa mahali, “nyamaza, wewe ni mtoto.” Kadiri miaka inavyoenda, Mah’mood alizidi kuwa mnyonge na kujiamini kwake. Ukiongea na Mah’mood unaweza kuhisi ni jasiri. Lakini ukisikiliza vizuri unagundua ana unyonge unaoua utu wake, ndoto zake, na uhuru wa kuwa yeye. Je, haya ni malezi au ufugaji? Je, Mah’mood analelewa au anaishi na wazazi wake kama mfugo? Jamii zetu zinaamini mno katika utii na nidhamu. Tunafikiri bila nidhamu iliyopindukia, utii usiohoji basi mtoto hawezi kufanikiwa...

Tujitathmini Kabla Hatujamhukumu Mtoto Mjamzito

Picha
PICHA: AboveWhispers Matukio ya watoto wa kike kupata ujauzito yanaongezeka. Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu (BEST) wanafunzi 4,718 wa sekondari kwa mwaka 2012 na 3,439 mwaka 2015 walikatishwa masomo yao kwa sababu ya ujauzito. Takwimu kamili hazipatikani lakini kwa elimu ya msingi hali haina tofauti kubwa. Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) linadai kwamba msichana mmoja kati ya sita wenye umri wa miaka 15 mpaka 19 wakiwemo wasiokuwepo shuleni hupata ujauzito kila mwaka hapa nchini. Ni wazi kuwa mimba za utotoni ni tatizo kubwa katika jamii yetu.

Unavyoweza Kumfundisha Mtoto Kuwa Mkweli

Picha
PICHA: Heaths Haven Fikiria uko jikoni ukiandaa chakula cha jioni. Watoto wako wawili wadogo Fred na Joe wanacheza sebuleni. Salome yuko mezani akifanya kazi za shule. Mara unasikia mlio wa kitu kuvunjika sebuleni. Unapatwa na wasiwasi. Unakwenda haraka kujua kilichotokea. Maji yanatiririka sakafuni. Chupa ya chai imedondoka na kupasuka. Unakasirika.

Yatambue Madhara ya Adhabu ya Bakora

Picha
INGAWA wazazi wengi huwachapa watoto wakiamini wanafanya hivyo kwa lengo la kuwaadabisha, tulibainisha sababu zilizojificha. Kwa ujumla, tunaweza kusema mzazi aliyelelewa kwa fimbo hujikuta na yeye akiamini fimbo ndio suluhu ya matatizo ya kinidhamu anayoyaona kwa mwanae.