Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mahusiano ya Jamii

Unataka Kumjua Rafiki Atakayekusaliti? Soma hapa

Picha
PICHA: Recycle Coach Katika nyakati kama hizi za Pasaka, mara nyingi, tunasikia marehemu Yuda Iskariote akijadiliwa kama jitu ovu lisilo na maadili lililokuwa tayari kumsaliti Bwana wetu Yesu Kristo. Binafsi naamini, pamoja na ubaya wake, usaliti wa Yuda ulikuwa muhimu katika kuwezesha mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Wakati mwingine Mungu hutumia mabaya kuwezesha mazuri. Hata hivyo, kwa maoni yangu, Yuda hakuwa na nia mbaya kivile. Kwanza, alikaa na Yesu kwa muda wa kutosha na hivyo alifahamu Yesu hakuwa mtu wa hivi hivi anayeweza kuchezewa kienyeji. Yesu alifanya miujiza mingi na Yuda alishuhudia. Yesu alitembea juu ya maji. Yesu alifufua wafu. Si mara moja. Tena kuna wakati Yesu alimfufua mtu aliyekuwa kazikwa siku tatu. Unamkumbuka Lazaro. Aidha, kuna nyakati washikadini na wanafiki walitaka kumshughulikia Yesu, wakashindwa kwa sababu Yesu aliwaponyoka. Yuda aliyafahamu yote haya. Kama baadhi yetu tunavyofanya leo, Yuda aliutazama uwezo huu wa Yesu k...

Mambo Sita Mwanao Anayohitaji Kuyasikia

Picha
PICHA: houstonpress.com Watoto wadogo ni watu kamili wenye hisia kama sisi watu wazima. Hata kama wakati mwingine hawawezi kusema wazi wazi, ukweli ni kwamba akili zao ni kama dodoki linalonyonya kimya kimya yale wanayoona tukiyasema na kuyatenda. Unaweza, kwa mfano, kusema jambo dogo kwa mtoto tena bila kumaanisha lakini jambo hilo likawa sumu itakayoharibu kabisa maisha ya mwanao. Unaweza kuwa na nia njema ya kumlazimisha kufanya kitu fulani sahihi kabisa, lakini kwa sababu hujaweza kuelewa na kujali hisia zake, jambo hilo likakosa nafasi kwenye moyo wa mtoto. 

Tabia Saba Zitakazokuwezesha Kutekeleza Malengo Unayojiwekea

Picha
KUANZA kwa mwaka mpya kunaambatana na matarajio mengi. Tunapoingia mwaka mpya tunamani kubadili maeneo mengi katika maisha yetu. Tunatamani kuwa na maisha bora yenye tija kiuchumi, kijamii, kiimani na kwenye maeneo mengine. Hata hivyo, katika kutekeleza malengo yako, ni dhahiri kuwa zipo baadhi ya tabia ulizonazo zinazoweza kuwa kikwazo katika kutekeleza malengo ya mwaka huu. Unahitaji kubadili tabia ili uweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza malengo yako.

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke -2

Picha
Katika makala iliyopita , tuliona kuwa mwanamke anahitaji kujua anavyopendwa na mwenzi wake kwa maneno na vitendo. Kadhalika, tuliona mwanamke anatamani kuwa na uhakika wa nafasi ya kwanza kwa mwenzi wake. Hatamani kuona akishindana kwa umuhimu na chochote kile kinachoweza kuchukua nafasi yake kwa mwenzi wake.

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Picha
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.

Namna Michezo Inavyomsaidia Mtoto Kujifunza

Picha
Wazazi wengi wanaichukulia michezo ya watoto kama shughuli isiyo na maana. Kimsingi, ipo imani inajengeka kuwa kucheza ni kupoteza muda. Matokeo yake wazazi hujitahidi kuwazuia watoto wasicheze kwa matumaini ya kuwasaidia wapate muda wa kufanya mambo ya maana zaidi kama vile kusoma na kukamilisha kazi za shule. Pamoja na umuhimu wa kufanya hivyo, hata hivyo, michezo  inabaki kuwa shughuli yenye umuhimu mkubwa katika ukuaji wa jumla wa mtoto kimaarifa, kimahusiano, kimwili na kihisia.

Jenga Fikra Chanya, Uwe na Furaha

Picha
Kuwa na furaha ni uamuzi wako mwenyewe. Furaha ni matokeo ya namna ulivyoamua kufikiri. Kadhalika, kukata tamaa na kukosa amani mara nyingi ni matokeo ya kufikiri mambo yanayokatisha tamaa na wakati mwingine tusiyo na majibu yake. Tunatafsiri vibaya mambo tunayokutana nayo na ndiyo sababu tunapatwa na msongo wa mawazo.

Kuanzisha na Kuimarisha Urafiki wa Karibu

Picha
Katika zama hizi za maendeleo ya kidijitali, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki. Unaweza, kwa mfano, kuwa na ‘marafiki’ elfu tano kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja katika maisha halisi. Marafiki wa kweli na wa karibu ni moja wapo ya mahitaji muhimu katika maisha. Tunaweza kuwa na sababu nyingi kuhalalisha kwa nini hatuna (haja na) marafiki wa karibu.  Hata hivyo, zipo nyakati  hufika tukajikuta katika maisha yenye kujaa upweke  na msongo wa mawazo kwa sababu hatukutumia muda wetu kutengeneza urafiki wa karibu na watu tunaofahamiana nao.

Umuhimu wa Kujenga Tabia ya Kujitolea

Picha
Kujitolea ni kutoa sehemu ya muda wako, ujuzi na maarifa uliyonayo na wakati mwingine nguvu zako kufanya kazi ya watu wengine bila kupata malipo ya moja kwa moja. Kazi unayoifanya kwa kujitolea mara nyingi ungeweza kuifanya kwa kudai ujira lakini unaamua kuifanya bure.  Mathalani, mwajiriwa anayetamani kuleta mabadiliko nje ya ajira yake, anapotumia ujuzi wake kufanya kazi za jamii bila kudai malipo, anakuwa amejitolea. Tuangalie kwa mhutasari kwa nini ni muhimu kujenga tabia ya kujitolea.

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -2

Tuliona katika makala iliyopita  maana ya saikolojia na kuhitimisha kwamba kinachotazamwa zaidi katika saikolojia ni tabia. Kwa hakika matatizo mengi yanayoikabili jamii yetu chanzo chake ni tabia. Tabia ndio chanzo cha matendo tunayoyaona kama kukosekana kwa uaminifu, ubadhilifu wa mali za umma, ufisadi, migogoro ya ndoa, misuguano ya kijamii, chuki, upendo, ugaidi, unyanyapaa, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kidini, changamoto za kimalezi na kadhalika. Yote haya yanaweza kuchambuliwa na kupatiwa majibu yake kwa kutumia sayansi ya tabia (saikolojia). Katika makala haya nitatoa mifano mifano kadhaa kuonesha namna sayansi ya tabia, inavyoweza kutumika kutatua matatizo yanayoikabili jamii.

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Picha
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.

Mahusiano mazuri na watu hujengwa kwa kutambua na kuheshimu hadhi zao na sio kulinda hadhi yako

Picha
WATAFITI wa saikolojia ya jamii, wanakubaliana kuwa miongoni mwa sababu nyingi zinazosababisha hali ya mitafaruku katika mahusiano ya watu -iwe kazini, nyumbani, na kokote- ni kule kujisikia kushushiwa heshima. Kwa kawaida, binadamu hatupendi kushushiwa hadhi, ego, ambayo ndiyo hutufanya tupambane na yeyote anayetishia kuharibu namna tunavyojiona na pia tunavyoonwa na wengine. Tunaambiwa, watu wenye kuamini kuwa hadhi zao haziko salama , insecure, wenye kujihisi kama watu wenye hitilafu fulani, huwa ni wepesi zaidi kuhisi hadhi zao zinachezewa na hivyo kuhitilafiana na watu kirahisi. Hawa ndio watu ambao, unaweza kuwakosea kwa bahati mbaya huhisi kudharauliwa. "Acha dharau dada!" Ndio kusema hawaamini hadhi zao. Watu secure, wanaoamini kuwa hadhi zao hazitishiwi na wengine, si wepesi kukwaruzana na watu. Sababu ni kwamba hawaoni kirahisi threat ya heshima na hadhi zao, na vile vile wanao uwezo mzuri wa kulinda hadhi na heshima za watu wengine. Migongano ya kimahusiano...

Namna ya kuifanya huduma ya 'day care' imfae mwanao

Picha
TULIJADILI kwa kifupi sana hitaji la huduma ya malezi yasiyo ya mama (non-maternal child care). Anzia hapa kama hukuisoma . Tulisema, sababu kubwa ni kwamba akina mama wa kileo wanatafuta kipato nje ya nyumba, hali inayosababisha changamoto ya kimalezi. Tuliona pia kwamba katika jamii yetu, huduma isiyorasmi ya malezi ndiyo inayotumika zaidi. Changamoto yake kubwa kuliko zote ni ukweli kuwa akina dada hawa wengi hawana uelewa wa kutosha wa malezi. Ni kweli kuwa hata akina mama wengi hawana uelewa huo unaoitwa wa kutosha. Lakini angalau, tunafahamu kuwa mama anaweza kujibiisha kuhangaika na mahitaji ya mtoto kuliko house girl, ambaye wakati mwingine hata hatumjui vizuri, yeye mwenyewe, wala familia yake, wala undani wa tabia yake. Shauri ya changamoto hizo, pamoja na nyinginezo, familia zenye uwezo kidogo zinachagua kutumia huduma za malezi rasmi ya watoto. Day care. Mtoto mara nyingine wa miezi kadhaa hadi wa umri wa kuanza shule, hupelekwa kwenye vituo vinavyotambulika ili alelewe k...

Changamoto ya kumpa 'mtumwa wa ndani' jukumu la malezi ya watoto

Picha
SIKU ZA NYUMA, familia zilikuwa tofauti na ilivyo leo. Akina mama walikaa nyumbani kulea watoto. Waliitwa mama wa nyumbani. Kazi yao kuu ilikuwa ni kuitunza nyumba kwa maana ya familia. Ni baba ndiye aliyekuwa na wajibu wa kutafuta mkate wa familia iwe kwa ajira, kujiajiri au namna nyingine.  Ilikuwa hivyo kwa sababu watoto wa kike walionekana si sawa na wenzao wa kiume. Hawakuwa na haki ya kusoma, na hivyo kujikuta katika mazingira ambayo hawakuwa na uchagazi mwingine zaidi ya 'ajira' ya kutumika nyumbani. Ndivyo ilivyokuwa katika jamii nyingi hasa barani Afrika. Leo hii mambo yamebadilika. Wanawake wanahitaji, na kwa kweli wanastahili haki na fursa ya kama ilivyo kwa wanaume. Hii leo, watoto wa kike wanasoma sana. Sawa na, hata zaidi ya, watoto wa kiume. Na matunda ya fursa sawa kwa wote kielimu, yamekuwa ni fursa sawa kiajira pia. Haki zimekuwa sawa. Sasa hivi hata waajiri wametambua kuwa akina mama wanaweza. Akina mama ni waaminifu. Wanashika madaraka makubwa makazini, na...

‘Vijana waache kutumiwa’

Picha
JINA LA KAMALA si geni kwa wanablogu wengi. Yeye ni mwendeshaji wa blogu maarufu inayojadili (pamoja na mambo mengine) masuala ya kiutambuzi. Bonyeza hapa kuitembelea . Ndugu Kamala anajulikana pia kwa namna yake ya utoaji maoni huru katika blogu anazozitembelea ambayo hufikirisha na mara nyingine kuibua mijadala zaidi. Blogu hii ilipata fursa ya kuzungumza naye siku chache zilizopita kuhusu falsafa zake, blogu, dini, siasa na mambo yake binafsi. Karibu kujua zaidi kuhusu mwanablogu huyu anayeblogu kutokea kanda ya ziwa. ________________________________________ Ndugu Kamala, nashukuru kwa kukubali kutumia muda wako ili tuweze kujadiliana masuala mawili matatu. Labda tuanze na falsafa yako binafsi. Unaamini nini katika maisha ambacho ndicho kinachobeba utambulisho wako kama Kamala? Naamini katika utu, ubinadamu, upendo na umoja. Napenda kuelewa vitu na kudadisi na ndio maana natumia majina ya kihaya tu ninayoelewa maana yake na kwa nini yawepo… napenda kuacha maisha yaende na kuf...

Mazungumzo na Kamala Luta

Siku chache zilizopita nilipata bahati ya kufanya mazungumzo mafupi na Bw. Kamala Luta, mwanablogu machachari ambaye si mara moja amewahi kuibua mijadala mizito kupitia maoni yake huru ama makala kwenye blogu yake. Kaa mkao wa kula. Nitayachapisha mazungumzo yake mapema sana namalizia kuweka koma, nukta na funga semi.

Blogu zakutanisha wanablogu...!

Picha
(picha mali ya Mtanga wa Mwananchi mimi) Habari za kukutana kwa wenzetu watano nilizipokea kwa furaha kubwa. Hii kwa hakika ni hatua kubwa na ya kupigiwa mfano. Bila shaka, kama wanavyofikiri wanablogu wengine, huu utakuwa mwanzo mzuri kwa wengine wetu tukukutana mmoja mmoja na hatimaye wote kwa wakati mmoja kama walivyofanya wenzetu hawa. Hongereni sana Mwananchi mimi , Hadubini , Mtambuzi , Lundunyasa na Chacha Wambura kwa kutuonyesha njia. Wapo watu wanadhani matumizi ya majina bandia yanawasaidia. Niliona mjadala fulani kwenye mtandao wa Jamii forums ambao kwa kweli ni vigumu wanachama wake kukutana kama walivyofanya wenzetu. Bonyeza hapa uone na utafakari. Tuachane na hao wasitaka kufahamika. Turudi kwa wenzetu waliweza kuutumia mtandao mpaka wakaweza kukutana siku ile. Hivi ndivyo Ndugu Fadhy anavyosimulia tukio hili: "Muda huu hapa hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. Tunamshukuru sana Mungu kwani leo tumeweza kukutana tena bloggers kama unavyotuona...

Ya Santiago na nguvu za Kiraia

Mkutano uliokusanya wanablogu, wanahabari, wanaharakati na wanateknolojia watokao katika nchi mbalimbali umemalizika. Siku mbili za mwanzo zilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali kutoka hapa Chile na sehemu nyinginezo ikiwa ni pamoja na Kampuni za google, Yahoo, You tube na wengineo. Kilichokuwa muhimu sana katika siku hizo mbili za mwanzo, ni kutizama mifano ya namna uandishi wa kiraia (mablogu, twita, facebook, simu nk) ulivyoweza kushika kasi katika nchi mbalimbali zinazoendelea. Unaweza kusoma muhtasari hapa kuona namna blogu zinavyoleta mageuzi nchini Madagaska kupitia jumuiya ya wanablogu iitwayo Foko . Nilizungumza na Lova Rakotomalala juzi na nilishangazwa na jinsi jamaa wanavyoweza kufanya mambo makubwa katika mazingira magumu yanayofanana na yetu. Madagaska wamekuwa mfano mzuri wa nguvu ya uandishi wa kiraia. Siku zile mbili za mkutano zilitupa ushahidi wa wazi wazi wa namna uandishi wa kiraia unavyopamba moto katika nchi zinazoendelea. Bofya hapa uone mifano mic...

Upweke wa kutokublogu

BAADA ya kimya cha muda mrefu kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, namshukuru Mungu wa Israeli nimerejea tena. Sijaja na kipya. Ila nimekuja kusoma mengi ya mtandaoni. Ukweli ni kwamba mtandao ni moja ya burudani zangu muhimu sana kama ilivyo mpira kwa wenzangu fulani. Kwa wenzangu na mimi tusiopenda kujua hata matokeo ya mechi za Uefa, wapi zaidi ya kwenye blogu? Nilikosa kusoma posti na maoni ya wanablogu. Nimekuwa kwenye kipindi cha upweke fulani hivi nisioweza kuueleza. Kila siku nijakosa kujiuliza: hivi Baba Mtakatifu Simon kasemaje leo? Da! Watu kama akina Mubelwa, Subira, John Mwaipopo, Yasinta, Maprofesa Mbele (bora hata ninakisoma kitabu chake kwa kukirudia na kukirudia) Matondo, akina Evarist, Kamala, Mbilinyi, Dada Vukani, Kisima, Lundu Nyasa (msee jibu lako nakuja nalo), akina Shabani Kaluse (pole na shule), wazee wa Strictly gospel (hee yale majadiliano nitayarudia mapema sana), na wengine wengi ambao nimebaki nao kichwani mwangu. Nilikosa kusoma mawazo motomo...

Posti bora ya mwaka 2009

Kabla sijapotea kwenye blogu (kwa siku mbili tatu nne)nitakushirikisha posti bora kabisa nilizozisoma kwa mwaka mzima 2009 ambazo kwa hakika zilinipa mtazamo mpya wa mambo. Nitarudi kama Shaka Ssali anavyosema-ga "Don't go away!", naja.