Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya bweni

Tutafakari hatari ya ‘malezi ya bweni’

Picha
PICHA:  Aparna Wazazi hawaamui tu kuwapeleka watoto wadogo kusoma shule za msingi za bweni. Ukiwasikiliza, mara nyingi wanakuwa na sababu za msingi kufanya maamuzi hayo magumu. Masuala kama migogoro ya kifamilia, wazazi kutokupatikana nyumbani, kutokuaminika kwa walezi mbadala mfano, wadada wa kazi, ni baadhi ya sababu zinazowafanya wazazi waamue kulipa gharama kubwa ya kuwakabidhi watoto kwa walezi wanaoaminika shuleni. Nafahamu wapo wazazi wanaochukulia shule za bweni kama sehemu ya kuonesha uwezo wao wa kifedha. Kwa mfano, baadhi ya wazazi hususani wale wenye uwezo wa kifedha, huzifikiri namna nzuri ya kuonesha ‘kujali elimu ya mtoto’ ni kumpeleka kwenye shule ya gharama kubwa na hata ikibidi shule ya msingi ya bweni ‘ili mtoto akazingatie masomo na apate muda wa kutulia.’ Hawa ni wachache lakini wapo. Shule pia zinazowaaminisha wazazi kuwa taaluma inapatikana bweni nazo zipo. Saa nyingine ni mchanganyiko wa nia njema, biashara au basi tu kukosa uelewa. Ukweli unabaki kwamb...

Unampeleka mtoto mdogo bweni? Fikiria.

Picha
Miaka michache iliyopita, mtu ulikuwa ukisikia shule za msingi za bweni, tena kwa watoto wadogo, tafsiri unayopata kwa haraka haraka ni malezi mabovu. Unampelekaje mtoto wa miaka sita bweni? Kuna nini cha maana shule ya bweni kinachohalalisha mtoto kutengwa na wazazi wake? Kwa hiyo, tuliona bweni ni uamuzi wa mzazi asiyeelewa jukumu lake la malezi, mzazi asiyejali, anayeamua kumtelekeza mtoto kwa sababu zisizo na msingi. Lakini kwa hizi nyakati tulizonazo, tunapokabiliwa na mabadiliko mengi ya kijamii, saa nyingine tunahitaji kuwa na tahadhari tunapofanya mahitimisho ya haraka kwa namna hiyo. Sikiliza simulizi la Aisha, afisa wa benki, mama wa mtoto anayesoma shule ya msingi la bweni. “Sikuwahi kufikiri ningekuwa mama anayeona bora mtoto aende bweni. Ndugu yangu yamenikuta.” Aisha ana mgogoro mkubwa na mzazi mwenzake. Ugomvi wao, ananiambia, ulifikia ngazi ya uadui. Haikutosha wao kushindwa kuishi pamoja, lakini pia ikawa vigumu kukubaliana nani abaki na mtoto. “Tulivutana sana. Baad...