Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Makuzi

Jifunze Uhusiano wa Malezi na Vilema vya Haiba (Personality Disorders)

Picha
Kizazi chetu kinakabiliwa na magonjwa mengi yasiyoonekana. Tunaumwa, na wakati mwingine taabani, lakini hatujui kuwa tunaumwa. Tunatembea, tunakutana na watu, tunapiga picha zenye nyuso zilizochangamka, tunaonekana kufurahia maisha lakini tunateseka na mahangaiko mengi tusiyoweza kuyasema.   Tazama kiwango chetu cha ukatili. Haiwezi kuwa kawaida, kwa mfano, kuona mwenzako anaumizwa na wala hujali. Unamuumiza mtu na bado unashangaa kwa nini analalamika. Unamtesa mwenzako kihisia na bado unamdhihaki anapougulia maumivu. Unajiuliza, tumefikaje mahali mwanadamu unaweza kumtesa mwenzako, ukamsababishia maumivu na hujisikii kujutia.    Mbaya, wakati mwingine, kiwango hiki cha ukatili kinakuwa kama nyenzo ya kupata tunachokitaka. Tunataka madaraka, tunataka umaarufu, mali na kila kinachotufanya kujione tunnawazidi wengine. Tunakuwa waraibu wa ukatili dhidi ya binadamu wenzetu na hatujisikii kujutia. Tazama kiwango chetu cha ubinafsi. Kwa nini tumepoteza uwezo wa kuafikiria hisia...

Ulionao ni watoto au mitoto?

Picha
  “Wenzangu nyie mnafanyaje watoto wawasikilize?” analalamika mama Rehema. “Hata sijui nilimkosea nini Mungu! Hii niliyonayo ni mitoto.” Namuuliza kwa nini? Kama mtu asiyeamini anaulizwa swali la kijinga ananijibu: “Haina akli, mijinga, mitundu, mikorofi, pasua kichwa kazi kunitia hasara tu,” anasema kwa hasira.    Kanisimuliza juzi kwenye mtihani wa nusu muhula mwanae mkubwa kawa wa thelathini na nane kati ya watoto arobaini darasani mtihani. “Huwezi amini hata sijashangaa. Mtoto wa Asha kapata A anawaongozea darasani!”    Kwa muda mfupi niliokaa pale kwake, watoto ni kama watumwa ni mwendo wa kelele na amri  kwenda mbele.  “Mama Rehema si ungerekodi tu amri ziwe zinatokea kwenye spika?” namwambia kwa kejeli baada ya kuona anatumia nguvu kubwa kutoa amri zile zile.  “Rehema! Unafanya nini?”  “Samweli? Hujanisikia?”  “We Rehema uko wapi hebu njoo nipe rimoti”   Mama Rehema anawakilisha tabia zetu wazazi wengi. Ingawa tunawaita ...

Changamoto za kuwanyima watoto kufurahia utoto wao

Picha
  Tunaishi kwenye dunia inayopitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya ya kijamii na kiuchumi, kwa kiasi kikubwa, yamezidisha matarajio tuliyonayo kwa maisha. Ukiacha matarajio mengi tuliyonayo kwetu binafsi, kuna matarajio mengi hata kwa wenzi wetu. Mke, kwa mfano, anatarajia mume awe kila kitu anachokifahamu kuhusu mwanamume. Mume ana kazi ya kuwa mcha Mungu, mtu wa sala, mtafutaji na mchapa kazi hodari, mcheshi, rafiki msikivu, kiongozi bora,     baba mzuri na mume mzuri asiyechelewa kurudi nyumbani. Matarajio haya makubwa yana faida zake lakini pia yana upande wa pili unaochanga migogoro mingi katika familia.   PICHA:  Wikimedia Commons   Hatuishii kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Tunazidisha pia matarajio kwa watoto wetu kiasi cha kuwanyima fursa ya kufurahia utoto wao. Hebu fikiria mtoto asiyeruhusiwa kufanya makosa. Kila analojaribu kufanya, anapodadisi mazingira yake,  anakuwa anatafsirika kama mtoto asiye na nidhamu na adabu kwa wa...

Tumeiachia teknolojia itulelee watoto wetu?

Picha
  Picha: reviewed.com Jijini Dodoma. Jioni ya Jumatano. Kikombe cha kahawa kinanikutanisha na maswahiba Gwamaka na Dk Mugisha. Tumezungumza mengi. Kisha mada inabadili uelekeo, “Unajua nikiangalia namna hawa wadogo zetu wanavyoyachukulia mahusiano sipati picha itakuwaje kwa watoto wetu.” Mada mpya ya malezi inachukua nafasi yake. Dk Mugisha anakiita kizazi hiki generation X , kumaanisha kizazi kilichozaliwa kwenye teknolojia. Kawaida, kila kizazi huona kilikuwa afadhali kuliko kizazi kinachofuata. Hata wazazi wetu, kimsingi, walikuwa na wasiwasi na sisi. Lakini ni ukweli pia kuwa mabadiliko makubwa ya kiteknolojia tunayoyashuhudia hivi sasa yamebadili kabisa namna tunavyoishi na kuchukulia mambo. Gwamaka anaona huu urahisishwaji wa kupata taarifa umeunda tatizo jipya tunalohitaji kulitazamwa. “Teknolojia imerahisisha mno watu kuyatangaza maisha yao mitandaoni. Tunajilinganisha mno na kuyatazama maisha kwa mizania ya vitu. Hili linaweza kuwasumbua sana vijana wanaochipukia hivi ...

Mabadiliko ya Kijamii Yanavyoathiri Malezi -1

Picha
PICHA:  The Conversation TUNAISHI katika nyakati ambazo maarifa kuhusu malezi ya watoto vinapewa umuhimu. Sambamba na ongezeko la mijadala ya malezi katika majukwaa mbalimbali, malezi yamevutia hisia za watafiti wengi kuliko ilivyopata kuwa. Kila siku, kwa mfano, zinachapishwa tafiti nyingi kuchunguza changamoto za malezi ya watoto.

Desturi Zetu Zilivyosaidia Malezi Bora ya Watoto -2

Picha
PICHA: The Community Voice NIMEJARIBU kubainisha baadhi ya desturi zilizosaidia kukuza watoto wanaojitambua. Unaweza kusoma makala ya kwanza hapa . Kwa kuanzia, tuliona namna familia zilivyowajibika kumtunza mama aliyejifungua. Mtoto na mama walipata muda wa kutosha kujenga mahusiano ya karibu.