Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2022

Tumeiachia teknolojia itulelee watoto wetu?

Picha
  Picha: reviewed.com Jijini Dodoma. Jioni ya Jumatano. Kikombe cha kahawa kinanikutanisha na maswahiba Gwamaka na Dk Mugisha. Tumezungumza mengi. Kisha mada inabadili uelekeo, “Unajua nikiangalia namna hawa wadogo zetu wanavyoyachukulia mahusiano sipati picha itakuwaje kwa watoto wetu.” Mada mpya ya malezi inachukua nafasi yake. Dk Mugisha anakiita kizazi hiki generation X , kumaanisha kizazi kilichozaliwa kwenye teknolojia. Kawaida, kila kizazi huona kilikuwa afadhali kuliko kizazi kinachofuata. Hata wazazi wetu, kimsingi, walikuwa na wasiwasi na sisi. Lakini ni ukweli pia kuwa mabadiliko makubwa ya kiteknolojia tunayoyashuhudia hivi sasa yamebadili kabisa namna tunavyoishi na kuchukulia mambo. Gwamaka anaona huu urahisishwaji wa kupata taarifa umeunda tatizo jipya tunalohitaji kulitazamwa. “Teknolojia imerahisisha mno watu kuyatangaza maisha yao mitandaoni. Tunajilinganisha mno na kuyatazama maisha kwa mizania ya vitu. Hili linaweza kuwasumbua sana vijana wanaochipukia hivi sasa

Unajua kugombana bila kufukua makaburi?

Picha
Picha: pixabay “Msitumie vibaya elimu zenu bwana,” Godi anaanzisha sogo kijiweni. Unamkumbuka?  Kaona kukaa haitoshi. Kasimama kabisa. Mikono inapepea hewani kusisitiza hoja, “Haya mambo yameanza leo? Ndoa zilikuwepo tangu enzi na enzi na hapakuwa na shida. Sasa nyie leo mnasema eti sisi wanaume ndio hatujui mahitaji ya wanawake? Mbona wazee wetu hawakujua hayo yote na bado ndoa zilidumu.”   Siku hizi ukitaka kuwachokoza wanaume ongelea matukio ya wanawake kunyanyasika. Salu kakaa pembeni anausoma mchezo. Tabasamu lake linaunga mkono hoja.   Hata hivyo, naona naye uvumilivu umemshinda. Kaamua kuulinda uanamue, “Hizi harakati zenu za kuwabeba wanawake zitatuharibia ndoa. Mie nawaambieni. Mnawatetea sana wanawake na watapata vichwa kweli. Wakitushinda tuwaleteeni basi.” Joto limepanda. Hisia hizi za akina Salu si za kupuuza. Mgogoro unapotokea kwenye ndoa, anayebebeshwa mzigo wa kutokufanya wajibu wake, mara nyingi, ni mwanamke. Msikilize Peki anavyogongea muhuri dhana hiyo:  

Mahusiano yenye ‘utulivu’ bila amani

Picha
Chanzo: stock.adobe.com Hivi umewahi kutaka kumwambia mtu jambo unaloona ni muhimu lakini ukakosa namna nzuri ya kumwambia?Unatamani ujumbe ufike lakini maneno sahihi ya kuubeba huna. Unafanyaje? Wengine huamua kuacha. Kuliko kumwuumiza mwenzako, huona bora mtu uugulie maumivu ndani kwa ndani. Mwingine hajali. Huamua bora ‘kutema nyongo’ hivyo hivyo bila kujali maumivu yatakayoyasababishwa na ujumbe. Wanachosahau, matokeo yanayotokana na k u jiumiza kwa kuuzuia ujumbe yanaweza kuwa sawa na madhara ya kuuachia ujumbe kiholela bila kujali maumivu ya atakayeupokea.   Mawasiliano ni sayansi yenye nafasi nyeti katika mahusiano. Ukikosea kanuni, mawasiliano yana nguvu ya kuleta uharibifu mkubwa unaoweza kugharimu afya ya mahusiano. M awasiliano ni sanaa pia.   Namna unavyosema jambo ni muhimu wakati mwingine kuliko hata ujumbe wenyewe. Ukishindwa kuchagua maneno sahihi na mazingira sahihi ya kusema jambo unaweza kufubaza uzito wa ujumbe wako. Thamani ya unachokisema inabebwa pia na namna

Unafanyaje kutathmini mabadiliko yako?

Picha
Picha: Mpiga picha simkumbuki. Mwaka ni 2004. Tunabadilika jamani. Sijui nyie wenzangu. Labda ni mimi peke yangu lakini saa nyingine ni vigumu kujiona tunavyobadilika. Usipopata mrejesho kutoka kwa watu unaweza kufikiri uko vile vile. Lakini ukweli ni kwamba tunabadilika. Tuanze na maumbile ya mwili. Mwili ukibadilika ni rahisi kuona. Hukuwa na kitambi, kwa mfano, sasa unacho. Tumbo nalo huwa halina-ga adabu. Badiliko lake linakuja taratibu sana. Halichomozi kwa siku moja. Unaweza ukawa unakula bila mpango, huoni ukibadilika. Unachukulia kawaida. Kuja kustuka, aloo kulitoa inakuwa shughuli. Ukiacha tumbo, kwangu kuna hili la macho. Ilinichukua muda mrefu kukubali kuwa sioni mbali. Nilikuwa nalazimika kufinya macho. Naona kawaida. Baadae sikuwa na namna. Ikabidi kukubali kuvaa miwani. Ushahidi mwingine huo. Mabadiliko hayana-ga haraka. Huja taratibu sana. Kingine mavazi. Tazama picha inayoambatana na maandishi haya. Hapo ni miaka 18 imepita. Huyo mwenye tai ni mimi. Sijui nini kilitokea